Preta siku hizi simuoni oni humu ndani. Naye keshaenda kuhiji nini? Mnasafiri kwenda wapi kama tayar uko Rombo? Au unaelekea moshi mjini?
Ebwana eeeeee huwenda siku tukikutana kwenye Party ya JF patakuwa hapatoshi. Huenda tumepishana sana tu kwenye makorido ya chuo bwana.
Hujaona ile thread ya sisi wana JF tikiongozwa na mwenye nyumba wetu Maxence tunaelekea mbuga za wanyama tarehe 27?
Ndugu yangu paulo hiyo Party kama itakuwepo mi naona itakuwa balaa maana Humu ndani mtu anajiita Rural Swagga unakuta ni baba yako mdogo,Kwa ufupi mimi sintakwenda kwanza nahisi kutakuwa na mashushu wakutosha 2
Ndugu yangu paulo hiyo Party kama itakuwepo mi naona itakuwa balaa maana Humu ndani mtu anajiita Rural Swagga unakuta ni baba yako mdogo,Kwa ufupi mimi sintakwenda kwanza nahisi kutakuwa na mashushu wakutosha 2
Cjaiona mkuu hebu nipe link yake. Leo nimekuwa busy kweli kazini hata JF sijaivinjari vzr leo.
Unapokumbuka uzuri wa mabibo hostel, do not forget the other side of the coin...Usafiri kutoka na kuenda chuo ulikuwa ni wa msoto mno na mi namshukuru Mungu hilo lilinipita kushoto.
Ha ha ha yalikukuta bwana weee..... Basi sisi mwaka wetu ndo tuliokuwa wa kwanza kupangiwa mabibo hostel mwaka 2001. Mi nikatupwa mabibo na marafiki zangu wakabaki main campus. Lakini nikawa bado natokea home (mbezi beach) naenda chuo kwa karibu kama miezi miwili hivi basi ndo maclass mate zangu wa mabibo wakawa wanaeleza mambo ya mabibo yalivyokuwa hot hot na mabinti kama kina kitimoto na wengine kama mtakumbuka. Basi mi nikaona nikienda mabibo basi nitachakachua uadilifu wangu, so nikaswitch na jamaa mmoja mshamba mshamba akaenda mabibo na kunipisha campus. Basi tangu mwaka huo hadi 2005 sikuwahi kukosa accomodation main campus.
Pia nakumbuka cc ndo tuliokuwa wa kwanza kufanya matriculations ili kujoin chuo.... Challenges zilikuwa kibao kwa wwale tulio ingia 2001.
Weeeeeeee, Ncha umepitiwa Mkuu, tuliingia 2001/2002 naku-graduate 2005. Ina maana tulifanya matriculation 2000. Sisi ndo wa KWANZA kufanya MATRICULATION na waKWANZA kutumia mabibo hostel ingawaje wengine tuling'ang'ania campus. Please revisit documents zako utaona ilivyo kaa.[/B]
Matriculations ilianza 1999 ila 2000 nadhani hawakufanya.
@ Mopao na Jack mmenichekesha na kunikumbusha mengi nyie watu tunafahamiana sio siri, mnakumbuka yule jamaa alieenda sijui block C akakuta kuku aliyemnunulia demu wake apike wale nakumbuka ilikuwa sku ya J2 jamaa kutoka church akakuta mafupa na jamaa kavaa taulo yake kajitandaza kitandani na nilibaunsa kumpiga hawezi kulia hawezi ikabidi achukue Maliboro aweke kichwani kwa vile jiko lilikuwa na moto bado likayeyusha mnailoni ikaanza kumchoma kichwa