Maisha ya depo

mi natamani kujuwa hayo maeneo ambayo umnaulizwa mnasema hampajui je mngesema wote kwa pamoja mnapajuwa nn kingetokea KURUTA..??
Mnhhh! mmmh, hili swali naomba nilitupe kwa doja la muda wote kutoka 835kj Aiylan wasalan huenda akatusaidia maana mimi limenipalia🤧 kwakweli

Ety mkuu mateso ayo yote c mnasema kwa pamoja TUNAPAJUA alafua haoooo mnakula utawala 🙂🙂🙂
Kupanga ni kuchagua mkuu ngoja tusubiri ushuhuda kutoka kwa Aiylan wasalan 😊atuambie kwao ilikuwaje.
 
ivanmark714 we mzalendo,hupaswi kuijua kambi ya jeshi,ukiijua utaambiwa beba dunia,roli na utafanya ma ovyo ovyo yote ili maafande wakuvune kwa ujuaji wenu.
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 06

Kwa kiasi kikubwa topic ilikuwa ikieleza kuhusiana na milango ya fahamu nilichokikumbuka hapa ni mlango wa fahamu uitwao sikio.

Najua wengi tunaweza kulielezea sikio kama mlango wa fahamu wenye kazi moja ambayo ni ile ya kusikia lakini kuna kazi nyingine mwalimu alitufundisha ila ni kama tunaipuuza.

Mwalimu Msuya aliniambia kuwa mbali na kusikia lakini pia sikio hutumika kuwezesha uwiano wa mwili kwa lugha ya role model wangu mfalme Charles wa tatu wanasema Body balance.

Huo ni ukweli ambao nilikutana nao kwa wakati huo ni kwamba sikio likipata hitilafu unaweza ukashindwa hata kutembea kwani kipindi masafa yanatafutana sikioni mwangu nilijaribu kusimama mbona niliipata fresh.

Nilijihisi kutetemeka nikajifanya nalazimisha kusimama ebwana ee nilipiga bonge la mwereka na kwenda chini.

Sijajua kilichotokea ila nilijikuta napepewa na KURUTA wenzangu huku afande Kalaghe akiwa pembeni.

Kwa mbali nililiona kundi lililongozwa na afande Mochiwa likipotea huku likitembea ubatabata yaani fahamu zilinipotea kiasi kwamba wale jamaa sikuona walivyoondoka nilikuja kuwaona wakiishia.

“Vipi KURUTA uko poa” aliniuliza afande Kalaghe
“Ndiyo afande”
“Kabisa KURUTA”
“Ndiyo afande”
“Kama hujisikii vizuri sema tukuitie gari la wagonjwa”

“Hapana afande niko sawa kabisa” Looh! hata sielewi ni kwanini sikuitumia hii nafasi sijui ndiyo ubongo ulikuwa umeshachanganyika na makamasi haikuwa akili yangu kabisa ona sasa nimepishana na huu UTAWALA.

Afande alijaribu kunionesha vidole kama kipimo cha kujua niko vizuri ama bado sijielewi maana kuna kitu alikiona jichoni kwangu.

Baada ya kujiridhisha afande Kalaghe alisema “Kweli KURUTA uko vizuri haya simama tuendelee na zoezi” tulisimama tukajipanga mistari miwili yenye askari wawili wawili yaani KURUTA wenzangu watatu waliokuwa wakinipepea na mimi mwenyewe.

Afande Kalaghe alikuwa akinisisitiza kunyoosha mstari na kunitobolea siri kuwa sababu ya yeye kunipiga lile kofi ni kwamba nilikuwa nje ya mstari kwa maana kwamba niliupindisha mstari hivyo ikapelekea yeye kunibutua banzi lile jamii ya mama mkanye mwanao.

Baada ya kunipa tahadhari hiyo akatuambia tuweke mikono kifuani kisha akasema “KURUTA zoezi la kunyakua”.

“Chini kuna miba juu kuna moto tunaondoka afande uup up up up” tulimjibu afande na kuanza kukimbia huku akituimbisha.

“Afande: Soja nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Wee nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Soja yaue
Sisi: Yaue
Afande: Wee yaue
Sisi: Yaue
Afande: Yaue yaue
Sisi: Yaue
Afande: We soja nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua nyakua
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua kushoto
Sisi: Nyakua
Afande: Nyakua kulia
Sisi: Nyakua
Afande: Wee nyakua nyakua
Sisi: Nyakua”.

Tuligonga zetu mwendo huo wa kunyakua mpaka tulipowakuta wenzetu tuliowakuta wakitembea mwendo wa nyoka.

Tulipofika afande Mochiwa akawa wa kwanza kuropoka “Baba vipi mmezika mmesafirisha”
“Hamna baba marehemu amegoma kufa” alijibu afande Kalaghe.

“Aaah kwahiyo mko naye hapo”
“Ndiyo baba”
“Mna uhakika mmekuja naye kweli”
“Ndiyo afande na mbona tuko naye hapa”

“Duuh ama kweli marehemu kafufuka mi simuoni ujue nawaona KURUTA watatu tu hapo huyo mwingine msije mkawa mmekuja na mzimu wake mjue” Moyo ulipiga paaah nikapatwa na mshtuko mkubwa.

Maneno ya afande Mochiwa yakawa yanajirudia rudia kichwani mwangu nilianza kusikia kizungu zungu na ilibaki kidogo nianguke nikaishia kuinama.

“Vipi tena KURUTA” aliniuliza huku akinisogelea afande Kalaghe ambaye ilimbidi awe na mimi bega kwa bega kuhakikisha anasafisha matapishi yake kwani ni kofi lake ndilo lililokuwa likinishughulisha wakati huo.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba lolote baya likinitokea ni yeye ndiye mwenye kuwajibika ingawaje bado walikuwa na majibu mepesi kama vile “ajali kazini” ama “kafa kizembe”.

Nilimjibu kwa sauti ya chinichini yenye unyonge wa hali ya juu “Ina maana afande ndo nimekufa kweli” alitabasamu afande huyo huku akiniangalia usoni kusema ukweli ugonjwa nilionao wakati huo haukuwa sikio wala jicho lilikuwa ni swala la saikolojia kifupi maneno ya afande Mochiwa yalianza kuivuruga saikolojia yangu.

Kwa sauti ya chinichini yenye upole mwingi akanijibu “Usiogope KURUTA hujafa afande anakutania tu si unamjua ni mtu wa masihara yule”.

“Kweli afande” nilimuuliza huku nikimtizama usoni ili kupata uhakika kutoka usoni mwake maana maneno pekee nilikuwa siyaamini kwa wakati huo.

“Ndiyo au wewe unajihisi uko tofauti na mwanzo”
“Hapana afande”
“Kama vipi subiri niwaite wale wenzio wakusimulie kilichotokea kama mimi huniamini” aliniambia afande na kuwaita wale jamaa zangu waliokuwa wakinipepea kule RESORT nilipozima.

Wakati anawaita nilimsikia afande Mochiwa akisema “Vipi baba anataka nini tena” aliposema hivyo kwa mbali nikaanza kuyaamini maneno ya afande Kalaghe aliponiambia kuwa mwamba alikuwa akinitania tu.

Nasema hivyo kwa sababu mwanzo alisema hanioni mimi isipokuwa anawaona wale wenzangu watatu ila awamu hii alipomuuliza afande kuwa nataka nini ina maana alikuwa akiniona kwa mbaaali nilikasikia kale kamhemo hfuuuu.

Wale jamaa walikuja kisha afande akawauliza “Eti nyie KURUTA kilitokea nini kule kabla hamjaenda kumpempea huyu jamaa”.

“Alianguka chini ghafla na kupoteza fahamu tukabaki kusha… kusha… kushangaa” alikuwa akielezea mmoja wa wale KURUTA huku akisitasita.

“Usiogope KURUTA mwambie ukweli usimfiche chochote ongea kila kitu” alisisitiza afande Kalaghe.

“Afande akatuambia tuache kushangaa badala yake tukupepee ndiyo wengine wakaondoka tukabaki sisi tukiwa tunakupepea ndiyo baada ya muda ukazinduka nafikiri baada ya kuzinduka kila kitu ulikiona” aliendelea kunisimulia KURUTA yule aliyefanikiwa kunirejeshea hali yangu ya kujiamini kutokana na maelezo yake.

“Enheeh umesikia sasa KURUTA au unataka kuwasikiliza hawa wengine” aliniuliza afande Kalaghe.

“Hapana afande inatosha nishaamini” nilimjibu poti huyo aliyekuwa amechuchumaa huku ameweka mkono wake begani kwangu.

Aliinuka afande Kalaghe akanishika mkono na kuniinua kisha akaenda kwa afande Mochiwa wakateta kwa sekunde kadhaa kabla ya kumuona afande Mochiwa akinitazama huku akitabasamu.

“We NGURUTU hembu njoo” alisema afande Mochiwa huku mkono wake ukiashiria kuwa alikuwa akiongea na mimi.

Nilimsogelea akaniongelesha “Dogo vipi”
“Safi”
“Haya niambie unakuonaje kuzimu” duuh sijajua waliongea kitu gani na afande Kalaghe maana pamoja na yote yaliyoendelea sikutegemea kama angeendelea kuniuliza maswali magumu kama hayo nilibaki kumkalia kimya nisijue ni kipi cha kumjibu. ,,,,,,,,,,,,,

...........................Itaendelea…………............………...
 

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 07

“Alafu jichoni umefanya nini NGURUTU mbona jekundu hivyo au mlikuwa mnavuta bangi nini” aliniuliza afande Mochiwa ambaye alikuwa akionekana kunizingatia sana usoni.

“Eti afande pale tulipowaacha kumbe mlikuwa mnapiga msuba” afande Mochiwa alikuwa akimuuliza afande Kalaghe.

“Hakuna afande kwani vipi”
“Unasema hakuna wakati mwenzenu jicho nyanya huku”
“Hamna afande litakuwa ni vumbi tu hilo la pale alipodondokea” akijibu afande Kalaghe aliyekuwa ameinama akizifunga vizuri kamba za viatu vyake.

“NGURUTU unaona vizuri?”
“Ndiyo”
“Kweli?”
“Ndiyo afande” alikuwa akiniuliza afande Mochiwa ambaye baada ya kumjibu alinifanyia lile zoezi la utambuzi wa idadi ya vidole kama alivyonifanyia afande Kalaghe tulipokuwa RESORT.

Baada ya kunifanyia zoezi hilo na kujiridhisha alimwambia afande Kalaghe “Poti chukua watu wako mkatusubiri mbele kule”.

Afande alituchukua watu wake wanne tuliokuja naye kutoka RESORT tukaondoka naye mpaka sehemu moja iliyokuwa na kidimbwi cha maji tukasimama kuwasubiri wenzetu.

Kwa mbali tuliwaona wenzetu wakisimama na kupanga mistari iliyofuatiwa na mbio ndefu huku wakiimba.

“Afande: Usinitege dada nimeokoka mwenzio

Sisi: Usinitege dada nimeokoka mwenzio

Afande: Haleluya
Sisi: Ameeeeeen amee
Afande: Haleluya
Sisi: Ameeeeeen amee”.

Walipofika tulipo walisimama kisha afande Mochiwa akamwambia mwenzake “Afande na watu wako lianzisheni basi”.

Afande Kalaghe alituambia tulalie tumbo karibu na kile kidimbwi niliyasoma mazingira kisha nikafanya reference ya kauli nilizozisikia siku za nyuma kisha nikajifanya bado sijakaa sawa hali iliyopelekea kutojumuishwa kwenye zoezi hilo.

Najua ungependa kujua ni kauli ipi niliirefer wakati huo ilikuwa ni ile ya karani wetu siku tukishangilia baada ya moja ya zoezi kusitishwa tukiwa UWANJA WA DAMU.

Nakumbuka jioni tukiwa KOMBANIA karani huyo alisema “Eti mchana WAZALENDO mlikuwa mnafurahia mvua kunyesha mkiona mmeikwepa introduction acheni kujidanganya hakuna kipindi makamanda wanaenjoy kozi kama kipindi cha mvua”.

Kauli ambayo niliruka nayo ni hapo aliposema “Hakuna kipindi makamanda wanaenjoy kozi kama kipindi cha mvua” hivyo basi nilipokiona kile kidimbwi ni kama kuna alarm iligonga kichwani na kuniambia “mtego huo”.

Sasa sikia kilichowakuta ndugu zangu ambao kwa hiari yetu tulijileta kwenye tanuri hilo tukisubiria matokeo ya kidato cha sita.

“Nimewaambia lalieni tumbo KURUTA kipi hamjaelewa au mnataka niwakande banzi kama mwenzenu kule RESORT” afande Kalaghe alikuwa akiwaambia wale jamaa zangu watatu waliokua wakinipepea nilipozima kule RESORT.

“Haya pita pale kwa mwendo wa nyoka” afande Kalaghe aliwaambia wale watu huku akinyoosha kidole kwenye kile kidimbwi.

Form six wale wastaafu ni kama walikuwa hawaamini walichokuwa wakiambiwa walisizi kwa muda mithili ya wagonjwa waliodungwa sindano ya ganzi.

“KURUTA ni kipi hamjakielewa hapo haya KROO KROO pale” awamu hii afande Kalaghe alikuwa akiwaelekeza huku akiwaburuza kwenye kile kidimbwi.

Baada ya kumaliza kupita kwenye kile kidimbwi wale jamaa watatu nikamsikia afande Mochiwa akiwaambia wafuasi wake “Nyie WADUDU mnasubiri picha ya pamoja nendeni pale” aliwaambia huku akiwasambazia mabanzi migongoni mwao.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani mpaka wanaisha wote yaliyotokea hapo kati siwezi kuyasimulia yote na kuyamaliza ila kwa uchache ni kuwa sikuwahi kupokea tuzo ya mwanafunzi msafi tangu niko chekechea lakini kwa wakati huo nilikuwa tayari kupokea tuzo ya KURUTA msafi endapo ingekuwepo kwa kweli nililitumia vizuri desa la karani wetu apewe maua yake.

Baada ya kumaliza tulipanga mistari yetu ya kijeshi tukanyakua zetu huku afande Mochiwa akituimbisha.

“Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Ewiih
Sisi: Ewaah
Afande: Elewii
Sisi: Elewaa
Afande: Babu wa mababu
Sisi: Ana demu na nyeto anapiga
Afande: We babu wa mababu
Sisi: Ana demu na nyeto anapiga
Afande: Nasema baaabu
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua
Afande: Haya baaabu
Sisi: Utamuua
Afande: Kakosa chiga
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua
Afande: Kakosa ugoro
Sisi: Utamuua
Afande: We babu wee
Sisi: Utamuua”.

Sikuwa nikicheza mbali na desa la karani Jala na kama wasemavyo waswahili “za kuambiwa ongeza na zako” basi nami sikuacha kujiongeza.

Tulikuwa tukikimbia lakini mimi nikawa najifanya sina mbio yaani nilikuwa katikati ya mstari lakini nikajivuta mpaka nikawa nyuma haikutosha nikawa napunguza mwendo na ilifika hatua nikawa natembea mpaka wenzangu wakawa wameniacha umbali fulani.

“We KURUTA tunakusubiri wewe ujue FANYA GHAFLA” alikuwa ni afande Mochiwa ambaye alikuwa akinisisitiza kufanya haraka kuwafuata pale walipo.

Nilijivuta kisanii nikafika pale walipo ambapo niliwakuta KURUTA wenzangu wamewekwa kitako.

“We staff KURUTA vipi hujisikii vizuri tukurudishe ukalale zako” aliniuliza afande Mochiwa aliyenivisha cheo cha ustaff kwasababu walichokuwa wakikifanya wenzangu sikuwa nikikifanya.

Yaani kama ni kwenye gari wote tunapanda tukiwa abiria lakini abiria wengine hawalipi nauli kwa mgongo wa kuwa wao ni staff na mara nyingi hukaa ile siti nyuma dereva ama hii ya mlangoni kwa mabasi ya mkoani.

“Daah kichwa kinagonga afande na nikiwa nakimbia naona kama kinazidi yaani nakisikia kinavuta balaa”

“Basi sawa kula maisha hapo ukisikilizie”
“Poa afande”
“Umenijibuje wewe? sema sawa afande unanichukulia poa KURUTA” alinikaripia afande huku akiwa ameniwekea uso wa mbuzi.

“Sawa afande” nilimjibu kwa unyenyekevu wa kiwango cha kupokea upako kisha nikajisogeza pembeni kwa ajili ya kutizama kinachotakiwa kutokea nikajikuta nimekuwa kama U.S.A mbele ya mataifa ya ulaya kwenye Berlin Conference.

“Haya KURUTA tano zimeisha saa juu uuuup” kumbe bwana kile kitako walichojikalisha walikuwa wamepewa TANO binafsi nilishangaa kuwakuta kwenye hali kama ile nilitarajia kuwakuta wamekunja ngumi ama wakinywa VIROBA.

“Uuuup” walikuwa ni KURUTA waliokuwa wakisimama juu baada ya kupewa amri hiyo na afande Kalaghe.

Afande Kalaghe akaamua kuwarudisha utotoni kidogo nikamsikia akiimba “Simaama kaa! Simaama kaa! Ruka ruka rukaaa simaama kaa” najua hatuna ugeni na wimbo huu hivyo ni rahisi kuelewa kwamba kama wimbo unavyozungumza na ndivyo KURUTA walivyokuwa wakifanya.

Kwa tafsiri hiyo mpaka afande anaweka kituo hawa binadamu wenye muonekano wa kizombi walikuwa wamekaa chini na ndipo balaa likawa limeanzia hapo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

................................Itaendelea……….………………...
 
ivanmark714 we mzalendo,hupaswi kuijua kambi ya jeshi,ukiijua utaambiwa beba dunia,roli na utafanya ma ovyo ovyo yote ili maafande wakuvune kwa ujuaji wenu.
Kifupi mzee wa You will never walk alone ivanmark714 sisi siyo wajinga tulikuwa tunatembea na hili desa👇👇👇👇
👇👇

Uzuri maswali tuliyosolve kabla ndiyo tuliyokutana nayo.

Au ungekuwa wewe pepa imevuja na unaingia chumba cha mtihani unakuta maswali ni yaleyale ungeacha kujibu ulichosolve ili ubeti kama utafeli ama utafaulu?
 
Braza umenirudisha pale kanembwa filimbi ilivyopigwa mfululizo, Yani ilikua patashika nguo kuchanika. Tulipifika kwenye dimbwi la maji jamaa mmoja akauliza afande tuvue viatu? Alisokomezwa kule na Kofi Moja dah ila alituokoa hatukuingia maana ilibidi aende akatolewe alikua afie mule. Watu mishino iliachia eti.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…