Maisha ya connection yanatutesa vijana.

Habari ya kupata kitu kwa connection inaweza kuwa nzuri au mbaya. Kwenye kazi tunaaswa kutengeneza "professional network", kujuana an watu tutakaoweza kusaidiana nao kitaaluma, kibiashara na kadhalika.

Jambo hili likifanywa kwa nia na njia nzuri, si jambo baya. Maisha hayawezi kuepuka kabisa connection.Kuna watu uliosoma nao, ulioishi nao, uliokua nao, unawajua vizuri.Ukiwa na nafasi ya kufanya kitu unaweza kuwafikiria zaidi kuliko watu ambao huwajui.Hususan nakusudia kuzungumzia watu wenye sifa.

Tatizo linakuja pale connection ndiyo inayokuwa sifa kubwa inayoangaliwa, hata mtu hana sifa anapewa pande kwa sababu ana connection tu.

Hapo tunaharibu kazi.

Katika kitabu chao wasomi wa uchumi Daron Acemoglu (MIT) na James A Robinson (Chicago) "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity and Poverty" wamechambua sana sababu nyingi zinazofanya nchi nyingine ziwe masikini na nyingine ziwe tajiri.

Sababu walizozitaja ni nyingi, na chambuzi zao ni ndefu na za kisomi sana kwa mimi kuzifupisha hapa, hivyo kufaidika kabisa kama hujasoma kitabu, kitafute. Ila kitu kimoja kikubwa kabisa walichoandika ni kwamba, nchi zinazokuwa masikini mara nyingi zinakuwa hivyo kwa kuwa na mfumo wa watu kupata fursa kwa connections.

Mfumo huu una tabia hizi.

1. Unapendelea watu kwa connection, si kwa uwezo.
2. Kwa sababu ya 1 hapo juu, unanyima watu wenye uwezo fursa
3. Watu wenye uwezo wakinyimwa fursa, na wasio na uwezo wakipewa fursa kwa upendeleo, mfumo mzima wa uchumi unadorora.
4. Kupendelea watu kwa connections tu, bila kuangalia sana uwezo, kunafanya watu wengi waone kuwa na uwezo hakuna maana na hivyo kutokuwa na nia ya kuwa na uwezo zaidi. Kama watu wanapata kazi kwa kujuana, na wewe hata usome mpaka Ph.D utaachwa tu, watu wengi ambao hawana connection wataona hakuna haja ya kuongeza uwezo.
5. Kupendelea watu kwa connection bila kuangalia uwezo kunaleta matabaka ya walio ndani ya mfumo na walio nje, walio nje wakijiona wametengwa sana, watauhujumu mfumo uanguke ili "malaika waishi kama mashetani..."
6. Mfumo huu unawanyima hata watu ambao wana connections fursa za kujiendeleza zaidi, kwa kuwa wengi wanabweteka kwa kuona hakuna haja ya kujiendeleza kama wanachohitaji ni connections tu. Hata ambao wangeweza kuwa na uwezo zaidi wanabweteka.
7. Mfumo huu unatengeneza matajiri wachache wenye hela nyingi na masikini wengi wanaopigania "hela ya kula". Kiuchumi hii ni hali mbaya, kwa sababu uchumi unategemea sana mzunguko wa fedha unaofanywa na watu wengi. Kama fedha zimefungiwa kwa watu wachache, hazizunguki, uchumi wa nchi utadorora.
8.Mfumo huu ukiendelea sana, under ceteris paribus, unakuja kuzaa maisha mafupi, magonjwa, umasikini, vifungo vya jela zaidi, kukosa elimu, matatizo ya afya ya akili, mimba za utotoni na mapinduzi ya nguvu ya kijamii.
9. Mfumo huu husababisha kutowiana kimilinganyo kwa kiuchumi miongoni mwa jamii (social and economic inequality)
10. Hatima ya mfumo huu ni kwamba hauna manufaa hata kwa wale ambao mwanzoni huwa wananufaika nao. Ndiyo maana matajiri wakubwa wenye akili kina Bill Gates na Warren Buffet wanafanya juhudi za kupunguza inequality.

Binafsi nilikuwa napiga vita sana mfumo huu, ambao nilivyoanza kazi Tanzania ulikuwa umeshika moto.

Kiasi kwamba, nilivyopata kazi yangu ya kwanza, watu wote walianza kuniambia "Mzee (baba yangu) kakuunganishia eeh". Wakati yeye alikuja kuambiwa baada ya mimi kupata kazi.

Nikaona isiwe tabu.

Nikajikata Marekani ambako hanijui mtu na kazi nitakayofanya itatokana na mimi kusimama mwenyewe, wala hakuna mtu wa kuniambia "Mzee kakuunganishia eeh"
Hutendei haki hii kuwa reply tu. Embu post kwenye thread yake kabisa.
 
Sasa mkuu kutongoza demu Kuna uhusiano gani na interview ya kazi.
Kama wako fair wangekupa tu kazi,shuleni ndio kosa kutongozana lkn uraiani au kazini sio kosa kumtongoza mtu.
Blaza kazi nilikosa halafu wakaja kulirudia tangazo tena nikapotezea sikuomba ila sasa hivi nakula kuku kwa mrija maisha juu ya mstari
 
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!
.
Kila mmoja ana experience yake katika kuhustle, kashapitia yote hayo uliyoyasema na maana katambua kilichomkwamisha yeye ni connection. Hivi unajua kwamba hata katika usaili ule wa mwaka Jana/juzi wa TRA kuna watu walikua wana ile screening test kabla ya usaili.
La msingi ni kumuambia azidi kupambana this is the jungle and not ridiculing him/ her.
 
Seem nyingi bila conection hutoboi, mwaka huu kunakaz zilitangazwa mahali nilikua lile eneo, watu wakatuma maombi weee, kumbe hata kabla ya deadline interview ikafanyika kimya kimya hapo ndo nilichoka, yaani lile tangazo lilikua bosheni tu, pata picha interview imefanyika kimya kimya kabla hata ya deadline ya tangazo siku tatu kabla, madogo wakawa wanaendelea kupeleka maombi wahusika wanawachora tu, kunadada alitoka mwanza kufika kuambiwa interview ilishafanyika hata kabla ya deadline kidogo azimie

Nakuna dogo hakuitwa interviw flan mwez wa 4 hakua na vyeti HR alimtimua sijui simu ilipigwa toka wapi dogo akaitwa, dogo alikuja kavaa iv vijinsi vya kubana na kobazi za kuogea kama kwake vile, akagonga interview bila hata vyeti na yupo mzigoni, ndo nikajua bongo bila connection ni msoto mkubwa, tena kwa awamu hii vinafasi vya ajira vinavyokua kiduchu ndo vimeongeza huu urasimu
 
Yes wewe ndio umeongea point.
Kupata kazi mtu mmoja kirahisi haiwezi kuwa reference kwa watu laki saba waliokosa kazi na wapo mtaani.
Kuna watu wengi wamejawa na maswali kichwani kwamba zile interviews za serikalini unatakiwa ufaulu kwa kiwango gani ili upewe kazi.
Maana mtu unafanya interview maswali yote unayapiga kwa uhakika na confidence kabisa halaf mwisho wa siku kimya tu.
 
Kuna wanangu nilikuwa nawakimbiza chuo wengi wao sasa wameshapata kazi na ni vilaza balaa kila siku wananipigia simu mimi nilie mtaani nawaeleleza concept kibao huko makazini mwao mpaka nawaonea huruma. Nimewasaidia mwaka wa kwanza mpaka kuandika dessertations zao ni vilaza haswa ila ndo hivyo connections zimewapa kazi huwezi amini mm mtoto wa maskini ndo nimewaandikia cv zao na barua za kuomba kazi kimbembe sasa wao wana kazi mm nipo mtaani nakomaa na biashara. Nakumbuka kuna interview moja nimeingia mpaka mwisho nimejibu vizuri maswali sijakaa ata sana naona kabisa hapa nimepita kmake majina yanatoka hola nilikata moto na kutuma cv kwa mda kwanza mpaka mama akanionea huruma aisee.Sio wote walio na kazi ni smart na sio wote walio mtaani jobless sio smart sometimes inahitajika mkono kidogo wa mtu wa ndani akuinue. Nashukuru mungu mtaani sio kugumu kiviile hustle zinaendelea huku tukiendelea kutafta kazi mdogomdogo. Ila ushauri wangu jitahidini kuwa smart kichwani pia mjichanganye na watu uwe na network kubwa. Your network is your networth.
Jah Bless
Pole sana mkuu.
Hicho ndicho anachokiongelea mtoa mada ila Kuna viazi hawaelewi kwa sababu waliitwa na kupewa ofisi kichwani maji matupu.
 
Seem nyingi bila conection hutoboi, mwaka huu kunakaz zilitangazwa mahali nilikua lile eneo, watu wakatuma maombi weee, kumbe hata kabla ya deadline interview ikafanyika kimya kimya hapo ndo nilichoka, yaani lile tangazo lilikua bosheni tu, pata picha interview imefanyika kimya kimya kabla hata ya deadline ya tangazo siku tatu kabla, madogo wakawa wanaendelea kupeleka maombi wahusika wanawachora tu, kunadada alitoka mwanza kufika kuambiwa interview ilishafanyika hata kabla ya deadline kidogo azimie

Nakuna dogo hakuitwa interviw flan mwez wa 4 hakua na vyeti HR alimtimua sijui simu ilipigwa toka wapi dogo akaitwa, dogo alikuja kavaa iv vijinsi vya kubana na kobazi za kuogea kama kwake vile, akagonga interview bila hata vyeti na yupo mzigoni, ndo nikajua bongo bila connection ni msoto mkubwa, tena kwa awamu hii vinafasi vya ajira vinavyokua kiduchu ndo vimeongeza huu urasimu
Mmeona ushuhuda huu wadau.
Halaf wale mbulula wataendelea kubisha tu ili mradi aonekane kucomment.
 
Tatizo ukianzisha biashara vilaza mliopewa connection tra mnakuja kutukadiria kodi isiyo na kichwa wala miguu matokeo yake mtu unafirisika.
Lakini ingekuwa wanaajiriwa watu kwa usmart wa upstair pengine wangetoa ushauri mzuri na sera za taasisi mbalimbali zingebadilika.
Wapo fasta kuweka kufuli kwenye biashara za watu.. Kweli wahenga walikuwa sahihi kusema mwenye shibe amjui mwenye njaa.
 
Mkuu hizo categories zote za kiubaguzi zipo wala usikatae.
Kwa mfano watoto wanaoishi masaki au mbezi beach automatically anakuwa na connections nyingi ukilinganisha na watoto wa tandika, gongolamboto,tandale hata Kama wote ni wa kabila moja.
Nadhani haujaelewana. Racism maana yake ni ubaguzi unaohusisha rangi baaaaasi si vinginevyo.

Kuna nepotism, huu ni ubaguzi kwa misingi ya kiundugu nadhani ndilo neno ulitakiwa utumie.

Zipo nyingi sana so kabla haujatumia neno jaribu kujifunza ukajua maana yake.....
 
Sasa racism inaingiaje wakati wote tunaochangia hii mada ni waswahili.
Mimi nilihisi yeye aliyetumia Hilo neno amechanganya ndio maana nikajiongeza na si kwamba sijui maana ya hilo neno.
 
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!
Bila connection hata tangazo la ajira unaweza usilione wala kulisikia.
Kumbuka sio vijana wote wanamiliki smartphone au pc
 
Acha mambo ya kulia lia. Hakuna cha connection. Serikali inatangaza ajila na watanzania wote wanaomba na mchujo, interview na selection zinafanyika kulingana criteria na vigezo. Wee kalia kuti na mkeka wa bibi na kulalamika eti kuna upendeleo. Mengine masikini wamefungwa na ujinga wa kutojiamini, kukosa hata 1000 ya kuingia internet na kufanya application au kutype na postal charges za barua, kuzungukwa na masikini wanakujaza ujinga wa kimasikini, kulogana, n.k. pambana struggle for existence and survival for fittest!
Kwahiyo hapo kwenye kuzungukwa na masikini unamshauri nini huyo mlalamikaji
 
Back
Top Bottom