Maisha ya Arusha sio

No ushost kila mtu na life lake, halafu bado wanapiga mizinga?
 
Jamaa wanaishi maisha ya ki primitive ambayo sehemu zingine watu washayaishi wakaona hayana maana wakaachana nayo
 
Kwanza nikuambie tu Sina uhakika Kama ww n mzawa wa Arusha ,naona Kama ni muhamiaji tu hapo ,
Mm ni mzawa kabisa wa Arusha hapo wilaya ya meru so huko ni kwetu kabisa ,
Sijui una lengo gani kuipaisha Arusha au kuichafua arusha kwa vitendo ovu na vya kikatili ulivyovisema ,mkuu unapotaja Arusha ,ujue unataja
Arusha jiji
Arusha manispaa/ Arumeru magharibi zamani
Meru/ east Arumeru zamani
Karatu
Longido
Ngorongoro
Monduli n.k
Sasa nikukanye au nikwambie tu acha kuichafua arusha kwa takwimu zako za matejo na ngalimitedi + kina ngarenaro na akina daraja mbili ,mkuu hyo cyo Arusha n vimitaa tu vya Arusha jiji nenda kauone uzur wa Arusha kwa kutembea wilaya zake ,zina watu Makini ,waungwana ,wachapakazi ,werevu ,na cyo hvyo vitabia vya mitaa tu ya Arusha jiji ,, arusha cyo mjini tu hpo ina wilaya zake na watu Makini Sana ,kwahyo biashara ya kuja hapa na ku genneralize arusha kwa data za vimitaa tu tafadhali acha Mara moja ,,
 
Yaelekea huyu aliondoka arusha 1995!! Anaongelea habari ya unga ltd na ujambazi leo? Haijui hata mitaa hatarishi kwa sasa,ngoja nimdokeze kidogo- pandisha barabara ya sanawari,panda juu kabisa hadi ukute daraja,ukishavuka hilo daraja sasa jiendee tu slow slow,maana muda wowote unakabwa,umeshaisikia kidin'ga? Basi bora usiisikie, (2)panda mianzini kutokea kwenye mataa pale, nenda juu kama kilometa 5 hivi,kuna mtaa kule wakaaji wote wanajuana,ukiwa hueleweki basi wenyeji wanakupora kila kitu mbele ya kadamnasi, in short Arusha ina washamba flani wachache tu (mleta mada akiwemo) ambao hawajawahi kutoka nje ya arusha na ambao wanadhani ni arusha tu ndiyo kuna vibaka,wanadhani ni arusha tu ndiyo kuna wavuta bangi,na wanafikiri ni ujanja kuvuta bangi huku unatembea barabarani,au kutembea na beto na bisibisi wanaona ni uselaaa! Hao washamba wachache ndiyo wanaotuharibia sifa ya kamji chetu!!! Najisikia salama mno kutembea unga ltd saa saba za usiku kuliko kukatiza temeke saa 12 jioni,
Labda Arusha ya zamani lakini sio ya sasa
Watu wamekuwa wastaarabu mno, sio kama kipindi cha nyuma
 
Mmasai ni Mmasai tu,.. Asili haiwezi badilika
 
Kwa hyo ishu ya bia hapo nadhani hata hyo Dar hujatembea vizuri
 
Mkuu hivyo visela mavi havijawahi kutoka nje ya arusha,niamini,mimi naishi hapa,nimezaliwa hapa!! Napajua,nawajua vizuri tu,ninafanya kazi mikoa mbalimbali na mara chache nje ya nchi,huwa nawachukua vijana kutoka arusha kunisaidia shughuli zangu,kwa sababu ukiondoa hao washamba ambao wengi wao ni wenyeji waliouza mashamba kwa wachagga na kuimalizia hela kwenye pombe vijana wa Arusha wanapiga kazi haswa!! Kila ninakoenda nao wanasifiwa
Huko chuga kawaida sana.

Embu waje dar watembelee sehemu hizi

Mburahati ,vingunguti, gongo la mboto, chanika , ukonga moshi bar, yombo buza, mbagala , keko kitoroli , nk.
 
Arusha matusi ni lugha ya kawaida na wenyewe haiwashtui hata kidogo,.. Mtu anatukana tusi zito akiwa na watoto wake na mkewe na wao wanachekelea tu, ni kawaida kabisa... Ila tumesahau kwamba hawa watu ni wamasai,.. Kwa asili yao na hizo tabia ni zao,.. Kwahiyo ndivyo walivyo hawatakaa wabadilike na kustaarabika.. Uhuni ndio sifa zao,.. Ndio maana ukiingia Arusha, na ubadilishe driving ya gari yako, hapa utaona vurugu nyingi barabarani na ni ngumu kuzizoea ila ndivyo walivyo... Taa za barabarani kila kukicha zinagongwa kwa ubabe wa kutofata sheria,... Awe mzee, mtoto au mke,. Tabia zao ni sawa,.. Tena wanawake wa Arusha ni wakorofi zaidi ya wanaume,.. Usidandie mke wa Arusha, wana roho mbaya sana hawa viumbe... Ila mimi naishi nao nikiwa najua ni WAMASAI.
 
Huko meru milimani si ndiko mnalima Bangi, mara nyingi sana polisi huenda kukata na kuchoma bangi mshamban huko,
Mzee Baba nikalie mbali usinletee mangetwa na Maniaje niaje😇😇
 
Waambie hao,
 
Maeleezoo meengiii halafu nehi
 
mtaa wa Ungalimitedi, huko balaa saa mbili asubuhi unaweza pigwa ngeta/kabali

Nilisoma huko shule inaitwa Edmund Rice sinon sec
 
Arusha jiji poa sana, kuna viwanja vya kitalii vya ukweli sana, wanawake wazuri sana, watu wanaendesha magar ya kisasa, nyumba nzuri, mzunguko wa pesa ni mkubwa, napapenda sana arusha
 
Yaani sehemu kama hizo siwezi kuishi hata siku 2..... sehemu ambayo haina usalama sio mahali pakuishi kabisa
Kwa hiyo mitaa uliyoitaja maisha ni ya ushetani kiwango cha juu kabisa tofauti sana na mitaa mingine

Huko wanaishi watu waliokata tamaa na maisha ....tsh 50 tu inaondoa roho ya mtu mitaa hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…