Kwa wabongo ni ngumu sana hatuna descipline na mpangilio na maisha yetu. wenzetu wadhungu wanaweza. Ndio maana unasikia wameenda summer holiday na vitu kama hivyo ili kuwa karibu na familia. Nina promotor wangu huyo hata siku moja hawezi kukujibu e mail ulotuma week end, na sidhani kama anafungua e mails zake za kiofisi jmosi na jpili. Akina sie hapa tunafanya kazi 24/7 hamna jmosi wala jpili na bado hatuna maendeleo. Well nachojitahidi kufanya kati ya hayo ni kutoisahau familia.
Kweli kabisa MJ1 hahahahaha lol! na mitihani ile ilivyo migumu Mhhhhh! Jamaa mmoja jana hapa jamvini alikuwa analalama kisharudia sijui CPA ipi kama ni one or two more than 5 times na kila wakati anatoka kapa sasa hitimisho lake ni kwamba NBAA ni bomu. Mbu hebu acha hizo Mkubwa za kufanyia bajeti hata sekunde chache tu! hahahaha lol!
Hapo umesema 100%, ni kweli sisi ni wazembe katika kujali maisha ya familia. Ninakataa kukubali ya kwamba anachofanya mdhungu sisi tutashindwa kama tutabadili msingi wa maisha yetu. Kwa wenzetu J2 na Jumamosi ni family days..mara nyingi moja kati ya siku hizo hakuna kupika home..familia nzima inatoka na kubadili mlo kwenye restaurant. Lakini sisi baba na mama hawaoni kama ni sahihi kwani kila siku wanasimama Pub na kujichana kila siku wakisingizia foleni barabarani.
Nyumbani kuna utitiri wa Pub hadi jioni watu wanafunga barabara za uswazi na kupanga viti nje..Hebu tujaribu kukaa na watoto nyumbani tuone kama hivyo vipub vitapata wateja..Tunajifanya ni wafanyakazi..wakati tunamaliza kila siku 4 hours kwenye matanuzi kati ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku.. Kama tunapenda kazi kwanini tusiendelee kufanya kazi hadi saa 4 usiku na kumaliza viporo vya kesho ili tuwe free Saturday?
Mfumo mzima wa kutojali familia na sisi wenyewe ni uzembe wetu ambao tuna-uhalalisha na mambo ya uchumi, foleni, shule etc..Hatukai pamoja kama baba na mama na kujadili mambo ya family; hatukai na watoto wetu ku-observe channel gani za TV wanaangalia. Parental Control banners kwenye vipindi vya TV havina umuhimu kwetu..kwani hakuna atakayekuwa nyumbani ku-observe, kazi hiyo tumewaachia ma-house girl ambao hata kusoma hawajui..
Mimi nadhani tuanze kujibadili.. All in all, tukumbuke kuna familia ambazo tumeshavuka haya tunayoyasema..hata kwa macho tunaziona na maneno tunasikia ..kama vile .."hao wanajifanya wadhungu..yaani utamwona baba yuko busy anawaogesha watoto halafua anafua nguo...kama sio udhungu basi amerogwa na mkewe"... Basi Ndugu yangu ..ukisikia majirani wanakusema hivi..ukenue meno..ume-win game! Wewe` unaishi perfect life..na sio maisha ya uzandiki!
Hii sred hadi nimeiota kabisa LOL!
BaK naona hapo kwenye red, kuna umuhimu wa kuanza time management course maana nsijepewa ofa ya outing na bwana Mbu na mie na uafrika wangu nkachelewa kwenye miadi..........ntakuta keshasepa wallah!!
Tunakimbia kabisa majukumu ya kifamilia. Watoto na ndoa zimegeuka mzigo,...kuwajazia ma X-box, na video games nyumbani unaamini ushawapa cha kuwa kep busy. Kumbe mnazalisha taifa la 'coach potatoes'...hakuna physical activities kuanzia baba anayefanya ibada zake pub, mama anayefanya ibada zake kwenye saloon za urembo, na watoto wanaobudu screens... baada ya siku chache baba ana kitambi, mama ana kitambi, watoto wana vitambi...wenyewe mnajiona mmenona kumbe mnalea magonjwa!
lol...hilo la time management course wengine wata exaggerate eti hawana fees.
Hilo ni tatizo sugu bana 'Bongo'...watu mnapeana ahadi mkutane kikaoni saa kumi, hapo
mpaka saa moja ndio mmoja mmoja anaanza kufika, Kikao cha ususluhishi kilichokua kiishe mbili usiku kinaisha tano usiku!---kesi inazua kesi muendako!
Hatuna utaratibu wa kufika kwa muda, ...utakuta mtu ana tiketi ya bus muda wa kuondoka saa moja kamili,
yeye moja kamili ndio anataka afike kituoni...ndio wale wakichelewa na foleni kidogo hawachelewi kukodi teksi eti ilifukuze basi!...
Airport siku zote utakuta last minute mtu anapiga mabio kuwahi check in kabla hawajafunga gati. By the time anafika departure lounge, wenzake wesha board....hapo ni mabio mengine, akiingia kwenye ndege ana tweta utasema alikuwa anafukuzwa. Treni na zile boats za Zanzibar ndio kiboko yao, ikishang'oa nanga Dar ndio safari imekufa hiyo!
Mwj1, asante kwa hili neno Time management. Lina maana kubwa maishani. Nikikupa miadi ya outing mbili na nusu usiku, ina maana nauhakika ukifika utakuta flower Bouquet haijanyauka, Glass ya Red wine haijapoteza Aroma, na hata appetite ya chakula na muda wa ku digest utakuwamo compared na 'muendelezo wa itifaki nyinginezo' usiku huo, lol!
Mkuu hapo umegusa penyewe..nadhani tukichimba zaidi tutapata starting point..Mimi binafsi nafikiri tumechangia valid points ambazo ni outcomes lakini bado hatujagusa chanzo.
Nadhani tuanze na matumizi ya familia. Hivi ni familia ngapi huwa zinakaa chini na kupanga bajeti ya mwezi mzima? Ni wangapi wana-review matumizi ya mwezi iliopita. Je? Ni wangapi tunajua kiasi kilicho katika account za partner zetu au wake au waume zetu? Ni wangapi wanaona umuhimu wa kuwa na joint account? kuna wengine wala hawajui mshahara wa baba au mama..hiyo ni siri kubwa. Nashangaa, Kama ninyi mmekubaliana kuwa kitu kimoja mbona vingine mnafanya siri.
Mimi nadhani.. (may be I am wrong) kuwa wengi wetu hatuzingatii kujipima kila mwisho wa mwezi tumeingiza kiasi gani; tumetumia kiasi gani na kwa sababu gani. Kama tutajua hili tutaona udhaifu wetu ambao unaweza kutufanya hata tukimbie ile michango ya harusi ambayo mimi binafsi siifagilii ikizidi kiasi fulani. Tukikaa chini kama "bunge" la nyumbani na kupitisha budget ya mwezi ujao ndio tunaweza kujua mama anatumia 60% ya mshahara wake salon na baba 60% kusaidia mapato ya Rose garden, Pub etc..Bunge ili la nyumbani ndio linaweza ona matumizi ya magari matatu ni ufujaji na ufisadi wa mali za familia na kumkaripia baba wa uongozi mbovu. Wengi wetu najua wanaona ni nadharia but it can be done.. ni discipline tu inatakiwa na uaminifu wa kweli na wala si ngojera za I love you.
Anyway, swali bado liko pale pale. Je tuko tayali kuwa transparent na mapato yetu hata kama ni madogo, tuko tayali na monthly family budgets, plans etc au tunaendelea kupiga ngonjera za I love you! Naamini mapenzi ya kweli ni kufunua sio kwa mwili tu bali kwa roho, mapato na kujua sio matumizi ya shilingi 1 bali thamani ya shillingi 1 kwa familia.
...Balancing the wheel of life means, kuwa pia na uwezo wa kumshawishi mwenzako nae akashawishika kujua umuhimu wa kusaidiana gharama. Bahati mbaya, maisha ya sasa yanaelemewa sana na External Influences. Yaani mke/mume akishaingia kwenye ndoa tu, tayari anaambiwa.."..haraka haraka tengeneza chako kwanza, usimuamini mke/mume kwenye nyumba yake, ...jenga yako kwanza!" Matokeo yake, yanaanza mashindano ya nyumba yangu, gari yangu, na blah blah nyingine as if hampo kwenye ndoa!
Mimi nadhani watu mkiingia kwenye relationship na kukubaliana kuoana hakuna haja tena ya mmoja wenu kumshawishi mwenzake kusaidiana gharama za familia ..ni jukumu lenu wote at par. full stop! Hata kama mmoja wenu kipato chake ni kidogo lakini thamani ya hiyo hela ni kubwa na sawa ya yule mwenye kipato kikubwa.
Nakubaliana nawe 100% on External influences lakini si tunasema mapenzi ya kweli yasiingiliwe na external influence? au tunaimba? Kama tunapendana kikweli basi uamuzi wa familia ni wetu either uwe mtamu au mchungu. kama tutakuwa na nidhamu za woga na kusilikiza watu wengine basi hapo hatuna familia. Hi sawa na kuwapa ndugu na jamaa remote control ya kuendesha maisha yetu. Siku moja watachukua hiyo remote control na ku-switch off maisha yetu.
Mimi naona suala la gharama za familia inabidi watu wakubaliane kabla ya kuwa na relationship au ndoa. Suala la baba ni kichwa limepitwa na wakati. Kama mmeoana na mmoja wenu anaanza ku-save ajenge kwao hizo ni dalili mbaya..hakuna maisha hapo ni heri safari iishie hapo hapo mapema kabla ya kuwa na watoto. Uaminifu na kuaminiana ni msingi wa maisha.
...kwa mtazamo wangu, Tatizo linaanzia na hili suala la kujiamini, kujiaminisha na kuaminiwa.
Ni wangapi miongoni mwetu tunajiamini ku reveal mshahara kwa wetu kwa wenza wetu.
Kisha ukajiaminisha kuelezea matumizi yako yote, na mwisho ukaaminiwa?
Vice versa ya hilo huzua mtafaruku mzima. Usipoaminiwa matumizi yako, kunazalisha kupoteza uaminifu na kutojiamini.
Kuepusha shari, utakuta mtu anakuwa mkali, "nyie nipeni LUKU nitalipia!..."
Kiukweli, hakuna kitu mbaya ndani ya nyumba kama mmoja wenu anakuwa muwazi kwenye map[ato na matumizi, ilhali mwingine hajulikani chenji zote anazichimbia wapi.
Ngumu sana kumuelewa mwenza ambaye, kama wewe mwatoka kwenda kazini kila siku, Una uhakika naye anafanya kazi inayolipa, lakini mwisho wa mwezi, anakupiga vibomu vya hapa na pale. Mbaya zaidi, linapokuja suala la kuchangia gharama za ndani aka ("pato la taifa!") mwenzio anapiga kalenda....au anajifanya mkali (wanaume hao,) kama ni mwanamke anajidai kujiliza eti unamuonea, "wewe ni mume unastahiki ulipie gharamna zote!"
Balancing the wheel of life means, kuwa pia na uwezo wa kumshawishi mwenzako nae akashawishika kujua umuhimu wa kusaidiana gharama. Bahati mbaya, maisha ya sasa yanaelemewa sana na External Influences. Yaani mke/mume akishaingia kwenye ndoa tu, tayari anaambiwa.."..haraka haraka tengeneza chako kwanza, usimuamini mke/mume kwenye nyumba yake, ...jenga yako kwanza!" Matokeo yake, yanaanza mashindano ya nyumba yangu, gari yangu, na blah blah nyingine as if hampo kwenye ndoa!
Hilo linaponza wengi, haswa wala wenye 'akili za kushikiwa!'
...ndivyo inavyotakiwa lakini utekelezaji wake sivyo!...miaka ya sasa na kizazi cha kileo watu wanaingi kwenye ndoa kwa uoga mkubwa!
Vigezo vya kuchagua mchumba, malengo na misingi ya kusimamisha ndoa kwa kiasi kikubwa imewaekwa pembeni. Kwa kiwango fulani, hii institutional inageka kama SACCOS/Upatu fulani...watu wanaingia mguu ndani mguu nje...
Ili kuweza ku balance haya maisha, lazima baba achukue sehemu ya uongozi ndani ya nyumba. Hapa nitaita kichwa cha familia, hata kama mama mwenye nyumba ndio atayekuwa mwingi wa kusuggest alternatives, lakini baba mwenye nyumba ahakikisha usimamizi na utekelezaji wa final decisions. Kuzidiwa "kifedha" kumo, lakini male pride nayo isitawale to the point kila anachofanya mke waona anakunyanyapaa...!...
Mwanaume ukishajiondolea kujiamini, kujiaminisha na kuaminiwa,kidogo kidogo hiyo nyumba hata kama ilijengewa kwenye msingi wa mapenzi motomoto, heshima ikishaondoka humo ndani mtakuwa hamkaliki. BTW, kwanini familia nyingi kipato ndio kinakuwa shetani mkuu wa kipimo cha mafanikio ya Mume au anguko lake?...
Tulizo umenichoma sana mkuu duh kwa kweli tunaweza na tubadilikeHapo umesema 100%, ni kweli sisi ni wazembe katika kujali maisha ya familia. Ninakataa kukubali ya kwamba anachofanya mdhungu sisi tutashindwa kama tutabadili msingi wa maisha yetu. Kwa wenzetu J2 na Jumamosi ni family days..mara nyingi moja kati ya siku hizo hakuna kupika home..familia nzima inatoka na kubadili mlo kwenye restaurant. Lakini sisi baba na mama hawaoni kama ni sahihi kwani kila siku wanasimama Pub na kujichana kila siku wakisingizia foleni barabarani.
Nyumbani kuna utitiri wa Pub hadi jioni watu wanafunga barabara za uswazi na kupanga viti nje..Hebu tujaribu kukaa na watoto nyumbani tuone kama hivyo vipub vitapata wateja..Tunajifanya ni wafanyakazi..wakati tunamaliza kila siku 4 hours kwenye matanuzi kati ya saa 10 jioni hadi saa 4 usiku.. Kama tunapenda kazi kwanini tusiendelee kufanya kazi hadi saa 4 usiku na kumaliza viporo vya kesho ili tuwe free Saturday?
Mfumo mzima wa kutojali familia na sisi wenyewe ni uzembe wetu ambao tuna-uhalalisha na mambo ya uchumi, foleni, shule etc..Hatukai pamoja kama baba na mama na kujadili mambo ya family; hatukai na watoto wetu ku-observe channel gani za TV wanaangalia. Parental Control banners kwenye vipindi vya TV havina umuhimu kwetu..kwani hakuna atakayekuwa nyumbani ku-observe, kazi hiyo tumewaachia ma-house girl ambao hata kusoma hawajui..
Mimi nadhani tuanze kujibadili.. All in all, tukumbuke kuna familia ambazo tumeshavuka haya tunayoyasema..hata kwa macho tunaziona na maneno tunasikia ..kama vile .."hao wanajifanya wadhungu..yaani utamwona baba yuko busy anawaogesha watoto halafua anafua nguo...kama sio udhungu basi amerogwa na mkewe"... Basi Ndugu yangu ..ukisikia majirani wanakusema hivi..ukenue meno..ume-win game! Wewe` unaishi perfect life..na sio maisha ya uzandiki!
Mabusara matupu
[/FONT]Nakubaliana na wewe mkuu..ukiondoa masuala ya kiuchumi ni ni wajibu wetu kuwaambia wadogo zetu njia hiyo si nzuri ..ndio maana magonjwa hayaishi na vizazi tunavyozalisha vinataambaa kuelekea kwenye maendeleo badala ya kukimbia..kwani hawana msingi wa malezi bora..
Dada zetu inabidi wajiamini.. ni tamaduni zetu zinawaweka nyuma..kama watajenga confidence za kuwa mwanaume ni sawa na mwanamke basi dhana hii itapungua.. dalili zake tutaanza kuona divorce nyingi kama Europe ..halafu tutaanza kuwaheshimu..
Nakubaliana na wewe..lakini inakuwaje kama mama ndiye anachangia mkate wa familia kwa 90% na Baba only 10%? Tunarudi pale pale..Heshima ndani ya nyumba..na makubaliano kabla ya ndoa.. Kama mke alikubali kumuheshimu Mume ingawa hana uwezo..basi..kipato hakina thamani zaidi ya penzi..Lakini jinsi gani twaweza tambua hili?
Maisha ni makubaliano kama mkataba..lazima kufanya utafiti na Swot za nguvu..Pesa anakuwa shetani kama makubaliano ya hapo mwanzo hayakuwa sahihi..Kama unajua mke ana pesa na hakuheshimu kwa nini unakubali kwenda..? Kama atabadilika hapo mbeleni..dalili za mvua ni mawingu..
kweli krolo tukijua majukumu yetu kama familia kwa ujumla wala hakutakuwa na matatizo yanayo tuface siku hizi, wadada wengi wanakuwa vichwa ngumu siku hizi, ukiuliza nini eti kasoma, ana uwezo wa kuishi hata peke yake na watoto wake, kwa hiyo mwanaume asimbabaishe, hii ndio inapelekea yote haya, majukumu ya kifamilia , mwanamke hata siku moja hajitumi kuingia jikoni, kuangalia watoto wake wanakula nini, yeye akisharudi ni chumbani kwake tu,hata hawezi kuwapa muda watoto kuangalia wanalala vipi, nakwambia siku hizi ni vita tu majumbani...lika mtu anajua haki yake, hapo hatufiki hata kidogo...wanawake wenzangu tukumbuke tu mwanaume ni kichwa cha familia na kamwe kichwa hakiwezi kuwa mkia, ukilazimisha ndio haya yanayotupata yanaibuka sasaMkuu Mbu hapa umeongea mbolea sana ingawa nitafafanua zaidi kwa uoni wangu, unajua kuna siku baada ya kukosa usingizi kutokana na "mbu" kuleta usumbufu chumbani basi nikajaribu kufikiria ni vipi wazee wetu waliweza kudumu na kufurahia ndoa zao, na katika jibu moja nililopata miongoni mwa mengi ni kwamba wazee wetu walifanikiwa sana kwenye kugawana "majukumu ya kifamilia", mwanamke alijua wajibu wake na wakati wake na mwanaume alijua wajibu wake na wakati wake, Kamwe la mwanamme hakubebeshwa mwanamke na la mwanamke hakubebeshwa mwanaume labda kwa dharura. Tatizo la familia zetu za leo, mwanamke anataka kuota sharubu na mwanaume na yeye anataka kuvaa sidiria.
Dah! Nafkiri nimemaliza.
MTM kumbuka career na family matters haziingiliani hata kidogo, ni lazima ubalance tu, sababu unaweza kuwa na mke yuko kiamily zaidi ila watoto wanahitaji ukaribu na wazazi wote wawili wether uko bize ku build your career or not wao hawajui wanataka tu ukaribu wakoaisee...
In just 48 hours the thread has gone this far.... sijui nianzie wapi
in short i can say muda hautoshi... we either have to chose career or family.. if we choose family then we will balance related areas and if we choose career then the chose the others
the best thing in life is to find a partner who complement what we have and not compete with what we have i.e. if i am a career man then i need a family oriented woman (hata kama anafanya akzi) and if i am a family man i can get along with a career woman
kweli krolo tukijua majukumu yetu kama familia kwa ujumla wala hakutakuwa na matatizo yanayo tuface siku hizi, wadada wengi wanakuwa vichwa ngumu siku hizi, ukiuliza nini eti kasoma, ana uwezo wa kuishi hata peke yake na watoto wake, kwa hiyo mwanaume asimbabaishe, hii ndio inapelekea yote haya, majukumu ya kifamilia , mwanamke hata siku moja hajitumi kuingia jikoni, kuangalia watoto wake wanakula nini, yeye akisharudi ni chumbani kwake tu,hata hawezi kuwapa muda watoto kuangalia wanalala vipi, nakwambia siku hizi ni vita tu majumbani...lika mtu anajua haki yake, hapo hatufiki hata kidogo...wanawake wenzangu tukumbuke tu mwanaume ni kichwa cha familia na kamwe kichwa hakiwezi kuwa mkia, ukilazimisha ndio haya yanayotupata yanaibuka sasa
pamoja na kuchomwa, i hope hujatobokaTulizo umenichoma sana mkuu duh kwa kweli tunaweza na tubadilike
Kweli kabisa, tena li baunca kabisa mwanamke akirudi home lishadaka pochi eti kuna nini humu loooo na ole wako usimpe hilo pochi imekula kwako.... all in all kila mtu abalance majukumu yake na family matters ili kuwe na uwiano mzuriHuo ni upande wa wanawake, na huku kiumeni utakuta jibaba lina kifua kama dari ya ikulu lakini limejipweteka linasubiria mama watoto akajitume alete cha mezani, Yaani ni kama tunaishi kwa kukomoana hivi. Na mbaya zaidi tunakomoana kinyumenyume, wa kike anakomolewa kiume na wa kiume anakomolewa kike. Balaa tupu wallahi.