Come27
JF-Expert Member
- Dec 1, 2012
- 7,500
- 7,104
Wenye Pesa, ndio hao hao ukiwatajia shida wanakutemamambo ya kuombana hela hakuna anayeyataka siku hizi... mimi mwenyewe sina hela hapa ila nakufa na roho yangu tu
Wenye Pesa, ndio hao hao ukiwatajia shida wanakutemamambo ya kuombana hela hakuna anayeyataka siku hizi... mimi mwenyewe sina hela hapa ila nakufa na roho yangu tu
unakubaliana na hoja?Good
Kama Yule mwanaume baada ya kumwona mkuu Na kuanza kulia Lia ety hana nauli.Shikamooni wakibwa zangu wa hapa JF......
Hii issue niliwahi kuambiwaga na mama yangu nikiwa mdogo sana ya kwamba watu wengi wa hali ya juu kiuchumi huanza kuwakwepa wale wenye uwezo wa chini kwa maana hawa wenye uwezo wa chini wakikutana na hawa wenye pesa cha kwanza kukimbilia ni kuwaomba hela, kutangaza shida walizonazo pamoja na kuwalaumu mbona siku hizi hawawatembelei kama zamani. Aliniambia ukitaka marafiki wa high class, kwepa sana kuwalaumu na kuomba omba pesa. Keep your problems in your heart. Sio umeenda kwenye msiba umekutana na mjomba anafanya kazi UN baada ya salamu ushaanza kutiririka shida zako. Mtachokwa.
Jamani mbona kuna mambo mengi sana yanayohusu maisha, siasa za ndani na nje ya nchi mnaweza kuzungumza pamoja na masuala ya kijamii badala ya kukimbilia kutangaza shida na kuomba hela?
Kama kuna jambo linaloweza kumjengea heshima mtu wa kipato cha chini kisha akapendwa na kupata marafiki wale wa high class basi ni kujiwekea mipaka ya mazungumzo na kujua ni kipi cha kuongea na kipi si cha kuongea mbele ya watu wa namna fulani. Hiyo inajenga sana heshima and they won't feel bored around you.
KIJANA KUWA MZALENDO. IPENDE TANZANIA. USITUMIKE KUICHAFUA NCHI YAKO.
Tatizo ni ccm.Marhaba mleta mada. Inanikera sana jamaa tumepotezana miaka zaidi ya 10 bahati nzuri tumerudisha mawaliano,siku moja baadaye unanipiga mzinga. I hate this
Tena wenye majumba, biashara, kazi na magari ya kifahariHumu wote sisi ni high class
Wapo mkuu ukiishiwa, hata ndugu waaina hiyo wapo ukiishiwa huwaoni tena.Ivi kuna marafiki walokua marafiki sababu ya pesa???
kukopa ni tofauti na kuomba, hata hivyo huko bank hauendi kusema tu nikopesheni, ni lazima uwe unakitu kinachozidi mara mbili au tatu, cha kuweka ili upewe mkopo.kuomba hela ni jambo la kawaida sana kwa kuwa hata hao matajiri wanaomba kwa kukopa benki.
Labda kitu ambacho sikipendi ni lawama tu lakini kuombwa napenda sana, kama ninacho nitakupa hata kama siyo ndugu yangu. Siyo vizuri kumtenga mtu kwa sababu ya shida zake. Kutoa ni jambo jema sana, hata Mungu anapenda. Kama hutaki kumsaidia basi kaa na mali zako na uchoyo wako lakini siyo kumchukia mtu kisa kakuomba jamani!!!