Nimekuwa bahili sasa nafurahia maisha

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,972
3,511
Sijui nianzie wapi mim tokea nikiwa mdogo miaka 14 nilikuwa nashika pesa na watu wazima wakawa wananiomba 200, 500 nawapa.

Nilipofikisha 17 nikawa nafanya mishe za utalii naingia baa nakutana na vijana wa miaka 30-40 wananiomba niwanunulie bia, viroba, fegi, mbege, sukari natoa.

Ikawa ni tamaduni wakiniona wanaomba nikiwa nacho nawapa. Mtihani mimi sina tabia ya kuomba omba nikiwa sina natulia.

Pia hao naowanunulia, kusaidia kila siku wapo kifukara hata huwezi kufikiria kuwaomba kitu...Na wakiwa na pesa wanaenda kutumia mitaa ya mbali kwa kujifichaa.

Mrejesho mwaka jana nimerudi mtaani kwangu nikiwa na pesa nyingi sana. Watu mtaani kama kawaida watu wakawa wananiambia, vipi hata bia moja, mwingine buku, buku 2.

Hakiyanani sijasaidia hata mmoja pesa nilikuwa nawapa tu ahadi baadae, badae tukikutana baaa akiomba bia namwambia subiri akiendelea natulia anajikataa hivyo hivyo.

Kuna mshkaj classmate alishazoea nampaga ten na mabia kila siku msimu huu kanicheki nikamtolea nje kabisa aliambulia buku 2 tu tena kwa taabu sana na nilikuwa na zaidi ya laki mfukoni ya kutumia siku hiyo.

Hakuna faida utakayopata kwa kuendekeza kusaidia watu pesa za jasho lako...wakati wewe pia unazihitaji. Ukifulia hakuna hata mmoja wa kukukopesha ata kwa riba...

Nimejifunza tena ukiwa mbahili ndio utapata heshima kwa jamii...... Kuna watu walishazoea nilikuwa nawasaidia hivyo akiniona tu cha kwanza ni kulia shida mwaka jana wamekiona cha MTEMA KUNI

Vibibi na vibabu nilikuwa navinunulia sukari, mbege, buku buku. miaka nenda rudi sijaona faida yake kila mtu ale kwa jasho lake ....labda itokee nimeamua saa msimu huu hii laki kadhaa nitatoa msaada ama kununua na sio kutoa sababu wahusika wameniomba eti sukari ama mjani ya chai.

Jiulize usipotoa huo msaada wako tena wa vitu vya anasa je watakufa? Usingetokea wasingeishi? Kabla waliishije!! Tabia ya kuonekana unasaidia sana ama kununua vinywaji hovyo kwa majirani au baa ni mbaya na inakutofautisha na baraka

Ubahili unaheshima yake, lazima uwe tajiri. Ukizoea kuwa bahili tabia inakuvaaa yaani saivi ata kumnunulia demu kinywaji sio jambo dogo naona kama ni fedheha.

Sio utani nauona utajiri mbele yangu, nikicheki ndani chenji kila kona sikosi vilaki au vimilioni kadhaaa.

Kunywa nakunywa tena baa kubwa ambazo zinawatu wa hadhi fulani, siwezi ombwa na ata wakizungusha sizungushi na pesa nakuwa nazo sio za mawazo.

Zamani nilikuwa nanunua mapombe bei ya jumla naweka ndani, then naweza ita washkaji tunakunywa zote, natoka nawanunulia saivi ni shida.

Nanunua mapombe yanakaa ndani miezi simpi yeyote. Nafurahia kuwa bahili siishiwi hovyo tena.

Karibuni chamani
 
Saivi naona raha kuwa bahili yaani nafurahi kama chizi nikiingia chumbani nikiona pesa zangu ....nafurahi nalalalaaa.

Akili ilinikaa siku mtoto alirudi shuleni akaniambia baba leo Mwalimu kasema ninyoe nywele!!!!

Nikacheki kabatini sina hata buku, nikawaza hapa mtaani nani anaweza kuniazima buku ya chap chap .... Nikapata jibu wale wasioniomba msaada kama boda boda, maduka ndio msaada wa kwanza ilihali naowapaga buku zangu hawana msaada...

Bahati nzuri nikakutana na jero 2 nikampa dogo siku ikapita..... Tokea siku hiyo nikitoa pesa yangu bila kazi roho inauma. Akili ilinipaa sana.

Nitawafundisha wanangu kua bahili kwa masikini watoe pesa, au hongo kupata kitu lakini sio kusaidia bila mpango.
 
Na huo ubahiri wako
Sure nasikia raha sana kuwa kaka mkuu wa chama cha wanaume bahili

Unajua pesa tunapata lakini shida matumizi hewa, nineishi china na japan wana utamaduni tofauti sana.

Date, sio jambo dogo ni kipengele mtu kumpenda mwenzie yaani mfano hadi mimi nikuelewe sio jambo dogo. Kulala na wewe haimanishi umeeleweka
 
Ubahili mbona ni kitu kizuri sana...

Yaani mie hata dem akitokea kuniomba hela tu au vocha mwanzoni kabisa katika mikakati ya kumtongoza natemana nae mazima.

Siwezi kuwekeza kwa limtu linalotaka yeye lipewe tu kisa anategemea mbususu yake.

Au kufanya mambo yasiyo nihusu napenda ku deal na mambo yanayonihusu mimi kwanza.

Kumbuka binadamu walio wengi hawana shukrani.
 
Back
Top Bottom