Maisha ukisha staafu kazi serkalini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ukisha staafu kazi serkalini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgen, Jan 28, 2011.

 1. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,194
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Mwanangu! Kwa sasa ni dhiki lakini ukistaafu kazi ni ziki KUU
  Kuna marafiki watatu watakuwa na wewe sambamba ukishastaafu hilo utake usitake wanakusubiri!

  1Kama uliwekeza kwa watoto wako nao wana akili na uchungu na wewe basi wanaweza kukusaidia kupata ugali wako wa kila siku!

  2Kama huna watoto wa kukusaidia inabidi urudi tena kwenye ajira tena. mf;Ulinzi kuokota machupa ya maji mitaani nk nk nk! Ili kupata ugali wako wa kila siku!

  3Kama kama huna watoto pia hukupata ajira LAZIMA UFE Mwanangu!

  Naomba mawazo yenu Great thinkers!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Aisee, usiongee maneno ya ukweli kiasi hiki bana!...Si ukweli wote unafaa kuusema!:A S 20:
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  NI kweli bongo ukistaafu ni balaa mwanangu. Inawezekana ndio maana wengi wanafanya ufisadi kwani hawana hakika na hatima yao baada ya kustaafu. System yetu ya social security is utterly poor.Ndio maana wengi wa wastaafu wanakufa miaka michache tu baada ya kustaafu. Kuna haja kubwa ya kurekebisha sheria katika mifuko ya pension ili imsaidie mstaafu kuliko sasa ambapo inasaidia vigogo katika mifuko hiyo na vigogo serikalini. Cha ajabu zaidi, muda wa kuishi wa mtanzania (life expectancy) haizidi miaka 55 kwa sasa, lakini muda wa kustaafu sehemu nyingi ni 60+, yaani ni bongo tu ambapo kwanza mtu anakufa then anastaafu.... maajabu haya!
   
 4. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu huu ni ukweli unaotisha! hebu twambie zaidi, unaongea 'with experience' au unakaribia hivyo unawaza itavyokuwa?
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,505
  Likes Received: 2,099
  Trophy Points: 280
  hapo blue nimecheka sana thanks for making me laugh:clap2:
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hebu toa solution sasa ni nini cha kufanya ili hayo yasikupate.

  Mimi nimejianda na some miradi ila sitataka kuwapa watoto wangu mzigo wa kunitunza. kama uko 35 years anza sasa kujiandaa usisubiri ufike 55 yrs la sivyo pressure au kisukari au kiharusi kitakumaliza ukiwaza. tumia akli yako angali uko kijana yaani tumia ujana wako kuandaa uzee wako. .
   
 7. M

  Matarese JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Suluhisho nimelitoa hao juu, kwa waajiriwa inabidi mifuko yetu ya pension iwe restructured kumsaidia mstaafu zaidikuliko ilivyo hivi sasa ambapo haina faida yoyoye kwa mstaafu. Labda kwenye hii katiba mpya linaweza kuingia hilo. Sina hakika kwa aliyejiajiri kuna kustaafu, labda staili yake ya maisha iwe na malengo ya siku za usoni kwamba kuna siku nguvu zitamwishia.
   
 8. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nionavyo maisha yalivyo hutakiwi kufikiria hizo solutions. Nahisi kuzaa kwa kutegemea kutunzwa na watoto ni mawazo ya zamani sana. Kuwa na watoto wachache... wawili au watatu..... wape elimu ya maana wajitegemee, badala ya kuwa na watoto wengi.... hela ambayo ungetumia kuwekeza for uzeeni, ukatumia for education, upbringing, fancy goods etc..... I stand to be corrected.
   
 9. L

  Leornado JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umeongea ukweli mtupu, usiombe ustaafu halafu watoto wako bado wadogo hata sekondari hawajamaliza ndio utaelewa tz ni ya nani.

  Nchi za wenzetu wastaafu ndio wana mafao mazuri na uhakika wa huduma za afya hadi wafariki.

  Ndio maana vibabu vingi vya kizungu vinakuja africa kuiba dada zetu wakawasidia kula pensheni na kuwaliwaza wakiusbiri kifo.....
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Great Thinker! Ukweli unauma na inatia uchungu haya yakikukuta kama hujajiandaa!
   
 11. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,194
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Uzoefu Mwana nilikuwa mjeshi nashukuru wanangu wananisaidia
  Nikiwaona wajeshi wenzangu tuliostaafu pamoja chozi litakutoka wapo waliokwisha kufa kihoro wapo waliochanganyikiwa wapo walioajiriwa na makampuni ya ulinzi!
  Fainali uzeeni!
   
 12. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usiangalie kwa karibu ivo. Kuwekeza kwa watoto siyo guarantee.Unaweza kufanya ivo na wakakutupa.Jiwekee mtaji wa kijamii zaidi.Ishi vizuri na watu hasa walio na umri mdogo zaidi yakO. Kama wewe una ujiko kama bosi mahali jitahidi kuangalia vijana wadogo kicheo, wainue, waangalie kama wanao au wadogo zako.Hii inalipa sana...( nakumbuka walimu wangu na hata wazee waliokuwa mbele kwenye nafasi hatuwasahau hata siku moja.)
  Pia unapoweza jiwekee akiba kama fixed deposits, nunua hisa kwenye masoko ya hisa, kata bima za afya na hata ajali, weka vitega uchumi vidogo vidogo mfano nyumba za kupangisha, frame za mafuka nk. Vyote hivi vitakusadia sana. Usithubutu kuanza biashara baada ya kustaafu kwa kutumia pesa ya pensheni hata siku moja. Hudhuria semina za kuwaandaa wastaafu.

  Mwisho lakini muhimu zaidi,hakikisha pia unaishi vizuri na mkeo/mumeo/mwenza maana fainali ni uzeeni
   
 13. R

  Rorya Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tausi hiyo unaongelea maisha ya nchi za watu kipato gani utakachopata na kuweka fixed deposit ya 4-5% interest alafu iweze kukutunza. hisa ukinunua hazipandi tokea zimefanya IPO
   
Loading...