GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
MAISHA Plus on Azam TWO: Mabinti 9 wakesha Mtini wakisaka 30M
Jana majira ya saa 3 usiku nikitazama mfululizo wa makala ya Maisha halisi kutoka Kijiji cha Maisha Plus kupitia Runinga ya Azam TWO nilijawa na mchanganyiko wa fikara kinzani huku roho ya imani na ghadhabu vikikinzana kwa wakati mmoja.
Nilitafakari sana juu ya tukio la adhabu ya kushinda kutwa nzima na baadaye kulala usiku kucha juu ya mti kwa mabinti 9 waliofanikiwa kuvuka hatua ya 16 bora katika Shindano Hilo linaloelekea Ukingoni.
Nilijiuliza hii inakuwaje Kama mti ule utavunjika? Na wanapata wapi nguvu ya kuwepo juu ya matawi kwa kipindi kirefu kiasi kile? Nini Hasa matarajio yao baada ya kunasa muda wote huo juu ya matawi ya Miti? Kwa nini hawakugomea adhabu ile? Je alikuwepo wa kuwatetea? Au ndio sehemu ya andiko la muandaaji wa kipindi kile cha Maisha ya uhalisia (Reality Show)?
Maswali hayakuwa kidogo na yote hayakuwa na majibu ya moja kwa moja ila dhana zikaanza kufunguka ambazo hasa ndo msingi wa kusukuma Uzi huu;
Hawa ni mabinti ni mbegu pevu na bora; ukiipanda itamea na kutoa lishe kwa wengine. Ile dhana ya Mwanzo ya kulitazama tukio Hili kwa jicho la Huruma na ghadhabu inanisukuma kuamini Taasisi za Kiharakati kwa akinamama na watoto wa Kike, wakwasi na wapenda maendeleo katika Jamii hapa ukiwekeza mtaji Mdogo wa Milioni 3 - 5 itawanufaisha Vijana wengi katika mataifa wanayotoka hasa wale walionasa katika kusaka japo wazo la kumuonyesha nini cha kufanya.
Hawa ni Mabalozi Wema bila Shaka kwa ujasiri ule; wakitumwa watafikisha salam, na wakipewa mbegu itazaa na kulisha wengine.
Shime watetezi wa haki na wapenda maendeleo
Wakatabah; Adios
UPDATE: usiku Huu Maisha Plus
GR
Duh Mchezo huu hauhitaji Hasira; ila ingependeza sana viunzi hivi ili kuthibitisha vimepimwa wangeonyesha mfano waandaaji ili kuhakikisha hakuna mashaka kwa washiriki katika kutimiza wajibu wao vinyinevyo inazua mashaka mazito juu ya mipango ya waandaaji.

- Bila Shaka wala chembe ya hofu mabinti Hawa wameonyesha utayari mkubwa sana wa kuzikabili changamoto za Maisha kwa kitendo kile.
- Wako tayari kwa jaribio lolote ambalo halitazima ndoto zao katika Maisha
- Tatizo la Ajira na Mitaji ya Biashara ni pana sana kwa Vijana wengi Ukanda huu wa Maziwa Makuu
- Hakuna aliyetayari kuikosa Milioni 30; na hapa ndio naliona tatizo kubwa na la msingi kwa ujasiri ule; Mwisho wa siku mshindi atakuwa mmoja tu. Lakini hawa wote Tisa hawako tayari kuikosa fedha hii.