Maisha ni mtihani mkubwa

Maisha ni mtihani mkubwa

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,046
Reaction score
1,473
Mitihani ya maisha omba isikupate asee kuna story nimetoka kuangalia, mama amepoteza lori lake mto Mwami. Just imagine gari ilikuwa mpya ndio imepata trip ya kwanza inaenda kutumbukia mtoni, mama wa watu analia na mengi, kapoteza gari, kapoteza dereva na bado anamajeruhi hospitali.

Mshukuru Mungu kwa uzima ulionao hata kama kuna changamoto za kawaida lakini kwa sababu unapumua seam Asante Bwana
Best wishes
 
Katika Maisha kuna mambo unapitia paka unaweza fika mahali ukasema MUNGU kakusahau lakini kiukweli kabisa MUNGU yu hai na anaokoa tunajisahau kwakuwa tu binadamu na hivyo ndivyo tulivyo

Lakini katika maisha pia kuna jambo ambalo binafsi nilijifunza katika hali ngumu ya maisha yangu

#there is no accident every thing has a purpose#
#the no bad news but there is news the way we take make them bad or good#

Mungu amtie nguvu mama huyo

Lakini maisha lazima yaendelee
 
Kwanza nampa POLE. Ila pia kwa yule ambaye alikuw na uwezo wa kununua loti, basi alikuwa ameshajipanga kimaisha kwa yanayofuata.

So, anasikitika kupoteza lori, japo naamini alikuwa amelikatia BIMA, so kapata maumivu, japo yatapunguzwa kidogo na bima aliyokata.

Ugumu wa maisha, muwazie mama ambaye anapanga nyanya, na vitunguu barabarani na bado anasomesha, hata uwezo wa bodaboda hana. Muwazie mzee anayepita njiani nauza manati (wapo, binafsi nakutana nao), huwa nabaki kuwaza HIVI KWA WIKI ANAWEZA AKAUZA MANATI NGAPI..??

So, mwenye uwezo wa kununua lori, HUYO TAYARI AMESHAJIPANGA KIMAISHA. Narudia tena NAMPA POLE, ila nyuma yake wapo wengi sana wenye shida nyingi sana kuliko yeye. Ambao kwao wanatamani wawe na genge la kupanga bidhaa zao hata mtaani kwa sababu USHURU WA SOKONI, hawawezi kulipa...!!!
 
Binadamu wote duniani wana shida ila zimetofautiana. Hata Tajiri mkubwa duniani Bill Gates kuna wakati anaweza kukuambia mambo ni magumu au.hayaendi sawia.

Kama vile vidole havilingani ni sawa pia na tajiri na umaskini una tofauti kubwa sana. Pia duniani haiwezekani watu wote wakawa matajiri.
 
Pole kwake. Maisha ni safari ndefu na imejaa changamoto za aina mbalimbali.
 
Yani wee acha tu mkuu.Kuna baadhi ya siku nakata tamaa sn.Ila namshukuru Mungu kwa afya na uhai,maisha yatasonga tu
 
Kama alikata bima comprehensive wala siyo ishu kwake. Kesho utamwona na lori jipya tena barabarani

Luckman1
 
Back
Top Bottom