Maisha na matukio/ Udini unatutenganisha sana

Mr sule

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
607
1,097
Miezi 2 miwili iliopita nilikuwa na binti wa kislam kwenye mahusano.

Before alijua mimi ni muislam kwasababu ya majina yangu yote mawili na hata majina ya ndugu zangu na marafiki niliowatambulisha kwake.

Nilienda zanzibar kwa lengo la kwenda kushangaa, nikajichanganya machimbo mengine nikakutana na huyu Binti anafanya biashara ndogo ndogo.

Kwa aina ya kazi yake ilivyokuwa na mavazi yake huwezi kujua kama bibie ni mzuri, mwenye mvuto.

Lakini niligundua hvyo na nikajichanganya kwake, nikajiongelesha tukaelewana nikamtoa Dinner na huko ndo upendo wetu ulipozaliwa.

Kutokana na alivyonipenda na jinsi upendo ulivyokuwa, unaweza kuzani tumekutana miaka 20 iliyopita.

Nilimwambia mimi nataka nimuoe na alikubali tena kwa furaha sana, lakini cos mimi naishi nje nilimwambie anipe muda niende nifungashe vya kwanvu alafu nirudi niamishie makazi Tz.

Tulikubaliana hilo, lakini aliomba akanitambulishe kwa wazazi wake kwanza kabla ya kuondoka, ili nikirudi mambo mengine yafanyike.

Hapo ndipo nikafikiria swala la DINI, niliamua kumwambia mwenzangu ukweli mimi ni mfuasi wa Yesu Kristo, alifikiri namtania, Nikamuonyesha picha nikiwa kanisani. ikawa hakuna namna.

Binti akashauri niwe muislam, nikamwambia haiwezekani, akaniambie basi niwaambie wazazi wake nitakuwa muislam ili tufanyikishe malengo ya kuwa pamoja na kama nitaendelea kufuata Yesu yeye hana shida na hilo.

Nilikubali cos mimi nae huyu bibie mzuri sana alafu hana mambo mengi, ni mpole sana mnyenyekevu, anasikiliza alafu ananipenda sana.

Bibie alikuwa amewaambia siku nyingi kuhusu mimi, bibie alichangia kubadili mazingira ya nyumbani kwao kupitia mfuko wangu.

kwaiyo hata nyumbani kwako nilikuwa na heshima yangu maana nilikuwa namtoa Zanzibar tunaenda mwanza, Arusha hata wiki mbili lakini ananiambia nisiwe na shaka kuhusu nyumbani kwako cos wanajua yuko wapi na nani,lakini bibie hakuwah kuniambia hilo.

Ukweni
Taarifa ya mimi kuwa kuwa mfuasi wa Yesu ilifika ukweni, lakini wazazi walimshauri bibie anishawishi niwe Muislam.

Nafika ukweni nakuta kundi la watu wamenisubur kunisilimisha.

Wakaniambia kuwa na mwanetu lazima uwe muislam na sheikh anaenda kukusilimisha leo.

Sheikh alinimbia niwe nafuatia maneno atakayoongea.

Alipoanza kuongea nikahisu ganzi. alafu ni kawaida nipohisi kitu mara nyingi nasema Jesus Christ kama kukemia kile kitu. ndo nikatamka Neno jesus Christ baada ya sheikh kutamka maneno ambayo mimi nilipaswa nifuate kuyaongea.

Kuanzia hapo nikaleta kizaa zaa.

Siku hiyo ilishindikana mimi kusilimu. kuna maneno mengine si lazima yote niweke hapo.

Licha ya yote, Bibie anasema hawezi kuniacha, wazazi wanataka tu nisilimu tu wanipe mwanao.

Kila ninapofikiri kukiri kuwa muislam ndo naishi kabisa kuchanganyikiwa, naona kabisa naweza kupoteza Dira ya maisha.

Bado niko nae bibie licha mimi kuwa nje ila naona mahusiano yanaenda kufika kikomo licha yeye kuwa tayari kuelewa but nahisi baraka za wazazi hakuna na hilo tatizo licha tunaongea vizuri.

Mama mkwe alinielewa sana ila anaogopa kutengwa na ndugu zake endapo ataruhusu mimi kumuoa bibie.

Sijaja kuomba ushauri, hii ni story tu.
 
Bro mpeleke SERIKALI ZA mitaa with mashaidi. oa huyo mke. waambie family umeoa kwa njia ya SERIKALI. within 21 days, your done .

Dunia ya sasa amna wanawake wazuri na humble. tena nje ndo worse utaludi bongo unajuta. achana na dini. to hell with them. take your girl and leave.

Wazee wame bariki ni issue ya dini tu. they won't care. as long as its legal with certificate
 
🤣🤣🤣maza ake kakubal sababu ya visent vyako tu,wanawake wa kiislam hawana sauti kwa familia zao,eti ndugu zetu katika imaan "kafiri aka kafri" aweza oa mwanetu katika imaan?labda kama ingekuwa una hela kama gharibu 🤣ngoja ndugu katika imaan waje watupe mrejesho
 
Kama wameruhusu uzunguke mikoani na binti yao na wao hawaoni tatizo lolote basi hapo hakuna waislam, wewe beba huyo mke uondoke nae
 
Umefeli mkuu, imani sio maneno ni kuishi.

Ilifaa utamke hayo maneno,ubae kanzu na msikitini uingie,piga mimba halafu baada ya mtoto kuzaliwa unaingiza gia namba 5.

Kwakuwa maisha ni bara huku au nje kama utaamua ni rahisi sana mkeo kufata kile unachoishi yaani kuwa mkristo.
 
maza ake kakubal sababu ya visent vyako tu,wanawake wa kiislam hawana sauti kwa familia zao,eti ndugu zetu katika imaan "kafiri aka kafri" aweza oa mwanetu katika imaan?labda kama ingekuwa una hela kama gharibu ngoja ndugu katika imaan waje watupe mrejesho

Mama angekuwa na sauti basi angeamua, tatizi lipo kwa ndugu. ila mama hana shida, bibie hana shida.
 
Kama wameruhusu uzunguke mikoani na binti yao na wao hawaoni tatizo lolote basi hapo hakuna waislam, wewe beba huyo mke uondoke nae

Walijua mimi ni muislam, coz majina yangu nikikuambia lazima usemi mimi muislam.

Ila bibie hana shida na Dini, shida wazazi
 
Umefeli mkuu,imani sio maneno ni kuishi.

Ilifaa utamke hayo maneno,ubae kanzu na msikitini uingie,piga mimba halafu baada ya mtoto kuzaliwa unaingiza gia namba 5.

Kwakuwa maisha ni bara huku au nje kama utaamua ni rahisi sana mkeo kufata kile unachoishi yaani kuwa mkristo.

Ndio tulichopanga, twende kwao nikubali kusilimu kinafki, Lakini Moyo ulikataa kata kata kusilimu.

Baada ya maongezi niliomba wanipe muda
 
Miezi 2 miwili iliopita nilikuwa na binti wa kislam kwenye mahusano.

Before alijua mimi ni muislam kwasababu ya majina yangu yote mawili na hata majina ya ndugu zangu na marafiki niliowatambulisha kwake.

Nilienda zanzibar kwa lengo la kwenda kushangaa, nikajichanganya machimbo mengine nikakutana na huyu Binti anafanya biashara ndogo ndogo.

Kwa aina ya kazi yake ilivyokuwa na mavazi yake huwezi kujua kama bibie ni mzuri, mwenye mvuto.

Lakini niligundua hvyo na nikajichanganya kwake, nikajiongelesha tukaelewana nikamtoa Dinner na huko ndo upendo wetu ulipozaliwa.

Kutokana na alivyonipenda na jinsi upendo ulivyokuwa, unaweza kuzani tumekutana miaka 20 iliyopita.

Nilimwambia mimi nataka nimuoe na alikubali tena kwa furaha sana, lakini cos mimi naishi nje nilimwambie anipe muda niende nifungashe vya kwanvu alafu nirudi niamishie makazi Tz.

Tulikubaliana hilo, lakini aliomba akanitambulishe kwa wazazi wake kwanza kabla ya kuondoka, ili nikirudi mambo mengine yafanyike.

Hapo ndipo nikafikiria swala la DINI, niliamua kumwambia mwenzangu ukweli mimi ni mfuasi wa Yesu Kristo, alifikiri namtania, Nikamuonyesha picha nikiwa kanisani. ikawa hakuna namna.

Binti akashauri niwe muislam, nikamwambia haiwezekani, akaniambie basi niwaambie wazazi wake nitakuwa muislam ili tufanyikishe malengo ya kuwa pamoja na kama nitaendelea kufuata Yesu yeye hana shida na hilo.

Nilikubali cos mimi nae huyu bibie mzuri sana alafu hana mambo mengi, ni mpole sana mnyenyekevu, anasikiliza alafu ananipenda sana.

Bibie alikuwa amewaambia siku nyingi kuhusu mimi, bibie alichangia kubadili mazingira ya nyumbani kwao kupitia mfuko wangu.
kwaiyo hata nyumbani kwako nilikuwa na heshima yangu maana nilikuwa namtoa Zanzibar tunaenda mwanza, Arusha hata wiki mbili lakini ananiambia nisiwe na shaka kuhusu nyumbani kwako cos wanajua yuko wapi na nani,lakini bibie hakuwah kuniambia hilo.

Ukweni.
Taarifa ya mimi kuwa kuwa mfuasi wa Yesu ilifika ukweni, lakini wazazi walimshauri bibie anishawishi niwe Muislam.

Nafika ukweni nakuta kundi la watu wamenisubur kunisilimisha.

Wakaniambia kuwa na mwanetu lazima uwe muislam na sheikh anaenda kukusilimisha leo.

Sheikh alinimbia niwe nafuatia maneno atakayoongea.

Alipoanza kuongea nikahisu ganzi. alafu ni kawaida nipohisi kitu mara nyingi nasema Jesus Christ kama kukemia kile kitu. ndo nikatamka Neno jesus Christ baada ya sheikh kutamka maneno ambayo mimi nilipaswa nifuate kuyaongea.

Kuanzia hapo nikaleta kizaa zaa.

Siku hiyo ilishindikana mimi kusilimu. kuna maneno mengine si lazima yote niweke hapo.

Licha ya yote, Bibie anasema hawezi kuniacha, wazazi wanataka tu nisilimu tu wanipe mwanao.

Kila ninapofikiri kukiri kuwa muislam ndo naishi kabisa kuchanganyikiwa, naona kabisa naweza kupoteza Dira ya maisha.

Bado niko nae bibie licha mimi kuwa nje ila naona mahusiano yanaenda kufika kikomo licha yeye kuwa tayari kuelewa but nahisi baraka za wazazi hakuna na hilo tatizo licha tunaongea vizuri.

Mama mkwe alinielewa sana ila anaogopa kutengwa na ndugu zake endapo ataruhusu mimi kumuoa bibie.

Sijaja kuomba ushauri, hii ni story tu.
Mpe mimba mkuu biashara inaishia hapo. Unaletewa mkeo asubuhi mapemaa.
 
Hata ww ni mdini maana dini isingekuwa na uzito kwako basi usingeona kazi kuiacha dini yako ili uoe, lakini kitendo cha ww kuwa tiyari kumuacha binti badala ya kubadili dini ni jibu tosha kuwa dini yako ndo kitu unacho kipa thamani kuliko kitu chochote.

Kwa hiyo ww kama unajiona una haki ya kusimamia dini yako basi tambua na haki ya hao wazazi wa binti kusimamia dini yao ,nenda kaoe wa dini yako ili kuepusha migogoro isiyo kuwa na ulazima kwenye maisha yako.
 
unaanzaje mahusiano na mtu asiye wa imani yako? utapata tabu bure. njoo nikupe ndugu zangu wa kike wazuri kwelikweli uoe
 
Huyo mdada ana chura? Tuanzie hapo kwanza. Maana zenji kule tako zao ni ubapa umelazwa.
 
Back
Top Bottom