Maisha na mapenzi

gstar

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
759
1,250
Katika mchakato wa Maisha kuna mengi tunapitia, kuna kupanda na kushuka pia kuteleza na kuanguka. Kila kitu tunacho pitia ni Mungu ndiye amepanga kutupitisha huko hivyo hata kama ni magumu kiasi gani unayo ya pitia usimkufuru Mungu.

Kila mtu unaye kutana naye ama kuishi naye ni wa thamani kwako kwa maana huwezi jua ni kwa vipi atakuja kukusaidia, waswahili wanasema “usitukane mamba kabla hujavuka mto.” Ukikwazana na mtu na kutofautiana ni vyema mkapatana naye lakini kama ikibidi kukaa mbali naye iwe ni kwa amani pia.

Kuna usemi maarufu wa kipolisi usemao kuwa ukikamatwa na askari kwa kosa lolote ni vyema ukakaa kimya kwa sababu chochote utakacho kisema kitakuja kutumika dhidi yako mahakamani. Hivyo basi kukaa kimya ni bora kuliko kuongea mambo yatakayo kuja kukuhukumu.

Tufanyeje tunapokuwa na hasira sana, kwa mawazo yangu mimi ni bora kukaa mbali na tukio ama kujitenga na mtu ambaye hatokupa furaha maishani. Kujitenga na mtu ambaye hatokupa furaha maishani haimaanishi kumchukia yule mtu bali inafungua ukurasa mpya wa maridhiano ambayo mwisho wake waweza kuwa, kukubaliana ama kutokubaliana.

Upendo umegawanyika katika makundi matatu, upendo wa kimungu, upendo wa kindugu na upendo wa mke na mume. Upendo wa kindugu waweza kuwa wa kirafiki ama wa damu kwa kuzaliwa, upendo wa kimungu hauna sababu unampenda mtu kwa sababu tu yeye ni binaadamu kama ulivyo wewe. Haina haja ya kumchukia mtu, kama hukubaliani na huyo mtu kwa namna moja ama nyingine bora ukae naye mbali kata mawasiliano naye basi inatosha ukimchukia haito kusaidia chochote.

Upendo wa mke na mume sababu yake ni tendo la ndoa hivyo kama hakuna tendo la ndoa upendo huo haupo. Mapenzi yanahusisha jinsia mbili tofauti mwanamke na mwanaume, katika mapenzi haya kunavyo vipengele vyake cha kwanza ni uaminifu, cha pili furaha na cha tatu amani. Vipengele hivi vyote ni muhimu, kimoja wapo kikipungua katika mapenzi kinahatarisha uhai wa mapenzi hayo.

Mapenzi ni kiumbe hai, kinazaliwa kinakuwa kinakomaa pia chaweza kufa. Kiumbe hai kikikosa chakula kitakufa lakini kikipata chakula kita nawiri na kukua hata kunenepa. Vivyo hivyo kwa mapenzi yakikosa chakula chake basi yatakonda na mwisho kabisa yatakufa. Kwanini tunalia wakati mapenzi yakifa ilihali tunayauwa wenyewe kwa kuyanyima chakula?

Subira, uvumilivu, ustahimilivu na kusameheana huyafanya mapenzi yasonge mbele lakini hapo ni lazima mizani ibalance kwa pande zote mbili, nani hustahimili na kusamehe zaidi ya mwengine? Jitahidi usiwe chanzo cha hayo yote
.
 
Amen ujumbe maridadi
Uufuate sasa hahaaa

Ila ubinadamu ni kazi sana. Ukiwa mkimya watu wanakuchulia punguwani au mjinga so muda mwingine ni vyema kuwarudisha watu kwenye line pale unapochoka.
 
Uufuate sasa hahaaa

Ila ubinadamu ni kazi sana. Ukiwa mkimya watu wanakuchulia punguwani au mjinga so muda mwingine ni vyema kuwarudisha watu kwenye line pale unapochoka.
Tena wanakuona boya boya wanakuweza
 
Mi huwa naheshimu sana ma x wangu wakitaka msaada nawasaidia tupo !! Poa kabisa japo watu huwa wanaamini kuwa nina wala ila huwa sijali maana ni maisha

sent from toyota Allex
 
Back
Top Bottom