Maisha marefu huambatana na mabalaa(story)

Maisha marefu huambatana na mabalaa(story)

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,351
Reaction score
1,100
mesimuliwa kuwa wakati fulani Jibril (as) alimuendea Nabii Suleimani (as) akimletea bakuli lenye maji ya uhai na akamwambia: Mola wako amekupa chaguo ambalo ukilichagua, unaweza kunywa maji haya na kubaki hai hadi siku ya hukumu.
Suleimani (as) aliliweka suala hii mbele ya kundi la watu, majini na wanyama, akawataka ushauri na wote wakamshauri kuwa anywe yale maji na aweze kuwa wa milele.
Suleimani baada ya kutafakari, alibaini kuwa alikuwa hajapata maoni ya nungunungu na hivyo akamtuma farasi akamwite, lakini nungunungu hakuja. Kisha alimtuma mbwa na hapo akaja mara moja!
Suleiman (as) akamwambia, “Kabla sijataka ushauri wako juu ya shauri langu, ningetaka kujua kwa nini nilipomtuma farasi mnyama anaye hes- himiwa zaidi hukuja, lakini nilipomtuma mbwa, mnyama mbaya kuliko wote, uliwasili mara moja?” Nungunungu alijibu, “Farasi licha ya kuwa mnyama anayeheshimika, hana utii, ambapo mbwa licha ya kuwa mnyama mbaya kuliko wote, ana utii; akipokea mkate kutoka kwa mtu, hubakia kuwa mtiifu kwake katika maisha yake yote.”
Kisha Suleiman (as) akasema, “Bakuli lenye maji ya uhai limeletwa kwangu na nimepewa chaguo, ama niyakubali au niyakatae. Wengine wote wamenishauri niyanywe ili niwe wa milele.”
Nungunungu akasema, “Je maji haya ya uhai ni ya kwako tu au watoto wako, familia na marafiki wanaruhusiwa kuyanywa pia?” Akasema, “Hapana! Ni kwa ajili yangu tu.”
Kisha nungunungu akashauri, “Ni busara ukayakataa, kwani utakapopata maisha marefu, watoto wako wote, ndugu na marafiki wataondoka kabla yako, kila siku inayopita itakuwa ikikuletea msiba na huzuni na hivyo kufanya maisha yako kuwa machungu.” Suleiman (as) aliukubali ushauri huu na akauzingatia, (kwa) kuyarejesha maji ya uhai​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom