Maisha mapya katika nchi za watu

Maisha mapya katika nchi za watu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,350
Hii story inamhusu Henry, kijana wa miaka 32 aliyekuwa mhudumu wa bank kwa miaka 10. Ana mke na watoto wawili wa kiume. Siku mojja waliitwa kazini na kuambiwa bank wanapunguza wafanyakazi, alilipwa kiinua mgongo milioni 15.

Alifikiria jinsi atakavyo endesha maisha na ile pesa. Aliamua kulipa kodi ya miaka miwili, alimpa mke wake milioni 4, nyingine alilipia shule Ulaya na kupata visa.

Alipofika Ulaya mwenyeji wake alikua anaosha magari. Ilibidi ajiunge nae. Katika maongezi alimueleza mwenyeji wake kuwa amekwenda kutafuta maisha. Mwenyeji wake alimshauri aoe ili awe na resident permit.

Katika ile car wash mwenyeji wake alijuana na wateja wengi sana. Kuna mama wa 42 ana watoto wawili, nyumba career ya kueleweka lakini hana mume. Alimuona huyu ni right candidate.
 
Hatari faya ili kumpumbaza mwanamke wake awe anamtumia mishiko tu ya kufa mtu na asiruhusu kumuita aje kumtembelea huko mbele ila yeye ndio arudi bongo kila baada ya mwaka.,,,Akishajijenga ndio arudi Bongo mazima.
 
Henry alipeleka mahari nyumbani kwa yule mama, walifanya harusi ya serikali. Yule mama alikua mpambe mashuhuri, alitaka mume wa kuvaa nae sare akienda kwenye ma party. Henry alipanda juu, handsome fulani. Akitokea kwenye party na mama, mama anajiona amepata mume.

Kasheshe ilianza sasa wakati maisha halisi yanaendelea. Mwanamke ana gubu, Akilala kwenye kochi mchana anaambiwa utaniharibia makochi yangu, akifungua fridge anatajiwa bei yake.

Henry alikaza moyo, alitafuta leseni ya magari akapata kazi kama dereva wa basi. Udereva wa basi Ulaya kuupata ni process ndefu na ni moja ya unskilled labour inayolipa vizuri. Henry alipiga mzigo na faraja kubwa aliipata kiwa kazini. Nyumbani kulikua kwa moto sana.
 
Bila picha hainogi habari kuishia njiani..wazee tupo kikaoni tunasubiria umalizie
 
Wakati huu Henry alipata mshahara wa kueleweka lakini alijibanza kwa mama kaisubiri makaratasi. Kila Jumamosi na Jumapili inabidi aende kwenye party na mama wakati kazini ndiyo shift zinalipa.

Kumziba mama mdomo Henry alibadilisha sakafu ya nyumba, alitoa fitted carpet aliweka tiles, alibadili makochi aliweka leather na jikoni alibadili fridge, jiko kila kitu.

Hajakaa sawa mama amepata mimba ya menopause khe, Henry alikuna kichwa.
 
Hii story inamhusu Henry, kijana wa miaka 32 aliyekuwa mhudumu wa bank kwa miaka 10. Ana mke na watoto wawili wa kiume. Siku mojja waliitwa kazini na kuambiwa bank wanapunguza wafanyakazi, alilipwa kiinua mgongo milioni 15.

Alifikiria jinsi atakavyo endesha maisha na ile pesa. Aliamua kulipa kodi ya miaka miwili, alimpa mke wake milioni 4, nyingine alilipia shule Ulaya na kupata visa.

Alipofika Ulaya mwenyeji wake alikua anaosha magari. Ilibidi ajiunge nae. Katika maongezi alimueleza mwenyeji wake kuwa amekwenda kutafuta maisha. Mwenyeji wake alimshauri aoe ili awe na resident permit.

Katika ile car wash mwenyeji wake alijuana na wateja wengi sana. Kuna mama wa 42 ana watoto wawili, nyumba career ya kueleweka lakini hana mume. Alimuona huyu ni right candidate.
Inamwendelezo
 
Baby shower ilifanyika kubwa, mama alikua ndiyo mwenyekiti wa umoja wa wanawake kwenye community, alichangia sana harusi za watoto wa mashost. Leo baby shower ya mwenyekiti wote walileta zawadi na kupiga selfie za kutosha.

Huku nyumbani Henry alishamfahamisha wife mchongo mzima kuwa hapa ni temporary makatasi yakiitika babe unapanda pipa na vijana.

Picha za baby shower zilijaa Facebook na Instagram, mama na baba kijacho wakipokea zawadi. Wapenbezit nuksi waka mtag mke wa Henry. Hali ya hewa ilichafuka sana.
 
Back
Top Bottom