Maisha magumu yaitoa chimbo familia ya Q Chilla

Dionize N

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,848
3,293
Familia ya msanii wa bongo fleva Q Chilla wameamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo yakifamilia.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, baba mdogo wa Q Chila amesema kwamba hofu juu ya mkataba ni kwamba haukuwa na ushahidi wowote kwa upande wa Q Chilla hali inayombana na kushindwa kuendelea kimaisha na kushindwa kuwa na nyumba yake.

Amesema familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chillah ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.

Ombi: wasanii jitahidini kuwa na wanasheria ili wawashauri kabla hamjasaini mikataba vinginevyo mtaishia kulalamikia watu huku makosa ni yenu. Acheni ubahili.

Source: EATV
 
Sasa ina maana Q hakuona vipengele vya mkataba kabla ya kusign? Hana washauri? hii ni aibu..
 
Q.Chillah na rafiki yake TID naweza kusema ndo best losers wa bongo flava
 
KWELI KABISA JAPO NI VIPAJI ILA NI MALOSER WAKUBWA
Ukiuliza watakuambia mziki kipindi chao ulikuwa haulipi wakati wenzao akina Prof.Jay, Nature, Jide, Jaymo, FA, AY, na wengine wengi tu wana maisha mazuri tu kupitia huu muziki lakini wao hawakuwekeza popote hata viwanja hawana sijui walitegemea nini
 
Huo siyo ubahili bali ni elimu ndogo, wasaniiwengi hajasoma yani elimu yao wengi ni darasa la saba sasa wanashindwa kujikuendeleza kielim mwisho wasiku wakikutana na wajanja wanaingizwa chakike.
 
Sasa ina maana Q hakuona vipengele vya mkataba kabla ya kusign? Hana washauri? hii ni aibu..
Inaweza kuwa aliona lakini kwa kuwa siyo fani yake,alihitaji mwanasheria ili amfafanulie baadhi ya vipengele ambavyo ndivyo vimemuweka pabaya.
 
Familia ya msanii wa bongo fleva Q Chilla wameamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo yakifamilia.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, baba mdogo wa Q Chila amesema kwamba hofu juu ya mkataba ni kwamba haukuwa na ushahidi wowote kwa upande wa Q Chilla hali inayombana na kushindwa kuendelea kimaisha na kushindwa kuwa na nyumba yake.

Amesema familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chillah ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.

Ombi: wasanii jitahidini kuwa na wanasheria ili wawashauri kabla hamjasaini mikataba vinginevyo mtaishia kulalamikia watu huku makosa ni yenu. Acheni ubahili.

Source: EATV
Jamaa mjanja, kaona akisema yeye itakuwa msala kwa meneja...... Bora atume ndugu
 
Zamani nilimuona anajitapa kuwa amelamba bingo, anamkataba wa maisha yeye na watoto wake hawatakuwa na shida.
Nilishangaa sana nikajiuliza unamlipaje huo mkataba, Leo na wazee wake namuona analialia tena.
 
Zamani nilimuona anajitapa kula amelamba bingo, anamkataba wa maisha yeye na watoto wake hawtakuwa na shida.
Nilishangaa sana nikajiuliza unamlipaje huo mkataba, Leo na wazee wake namuona analialia tena.
Mkataba wa maisha bila Gari...Nyumba na blingbling nyingine??
 
Back
Top Bottom