Feb 7, 2017
Familia ya Q Chillah walia na mkataba wa maisha
Familia ya msanii Q Chillah imejitokeza na kuhoji mkataba wa Q Chillah na QS Mhonda J. Entertainment ambao unamfunga huyo msanii ''kisheria'' maisha yake yote.
Familia inajiuliza mtoto wao Q Chillah aliposaini mkataba wa maisha wa kazi zake za muziki alikuwa amelewa au vipi kwani hawajawahi kuona mkataba wa kazi za kisaini popote pale ulimwenguni wenye kipengele cha kumfunga msanii ndani ya mkataba maisha yake yote.
Familia ya Q Chillar imetoa ombi kwa QS Mhonda J Entertainment wakae pamoja kupitia mkataba huo upya badala ya kupelekana mbele ya vyombo vya kisheria kupata ufafanuzi wa uhalali wa mkataba wa ''maisha'' baina ya msanii huyo na kampuni ya QS.
Hali hii imewakumba wasanii wengi kutokuwa makini wakati wa kusaini mikataba na hatimaye kutofaidika na jasho la kazi yao. Tusikilize kilio cha wanafamilia ktk video clip hapa chini:
Source: EastAfrica Television