Maisha katika nyumba za kupanga

Maisha katika nyumba za kupanga

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,349
Habari za leo wandugu,

Dunia hii kuna wengine hawajawahi kabisa kuishi katika nyumba za kupanga, wengine maisha ya uswazi hawayajui kabisa, basi leo nimeona tuangalie maisha katika nyumba za kupanga. Ukweli ni kuwa maisha katika nyumba za kupanga si mabaya, ni wewe mwenyewe utakavyoiweka akili yako.

Unaweza kujifunza mapishi katika nyumba za kupanga, kwani kupika wote mnapika pamoja, kama ulitoka kwenu hujui kipika chapatti, utakutana na wapangaji wenzako ambao tena wanapika chapatti za biashara, na utajifunza kukanda unga hapo. Si chapatti tu, ni mapishi mengi.

Ukitaka kuishi vizuri kwenye nyumba za kupanga usiwe mbea na mfuatiliaji wa mambo ya watu pia usipende kuanika ya kwako. Ukikuta unaongelewa wewe dharau tu, kama hujaanika sana yako watakayo kuwa wanaongea watakuwa wanahisi.

Rafiki zangu wa kiume kama watatu hivi waliniambia bikra zao zilitolewa na wapangaji wengine wakati wakiwa wadogo kwenye nyumba za kupanga, mimama isiyokuwa na haya anamsubiri mama wa kijana ametoka, ndipo kijana anapoitwa chumbani, huko anakuta ameandaliwa chai na vitafunwa na akapewa mchezo. Kama vile wale wa ushuani wanaposema bikra zimetolewa kwa ma housegirl huku kwetu kwa Mtogole kuna mengi pia yanaendelea.

Dhumuni la waraka huu ni kufahamishana dunia inavyoendelea katika nyumba hizi, kuna mengi yanayoendelea ambayo wazazi hawayafahamu. Fikiria kama hili li mama linalomuitia kijana wako chai lina magonjwa, mpaka uje uhfahamu mtoto ameathirika kabla hajafikisha miaka 20.

Siku njema.
 
Uswahilini usipokuwa mbeya watakusengen ya wewe kuanzia wageni wako, unachokula, mpaka unavyovaa
Kuna brother mmoja alipata chumba uswaz, sasa asubuhi alikaanga mayai mawili kwa breakfast, khe it was a talk of the house, anakunywa chai na mayai. Basi mkaka kuwakomesha akawa anapita kwa wauza chips anaomba maganda, asubuhi akishakaanga mayai yake mawili anatupa maganda kama ya mayai sita hivi, wee wa mama wanakaa kabisa kuhesabu maganda.
 
duh!!
 
Umenikumbusha shosti,nilienda kumuona shogangu tuliachana zamani sanaa baada ya kukutana nae akanikaribisha kwake
na alikua best yangu sanaaaa nikasema wavha weekend moja niende sasa kuelekezwa mpaka kufika ilikua shughuli,haya kufika wako wapangaji wenzie nikawa nimemchukulia zawadi,mara akatoa jiko kuanza kupika duu mara huyu anatoka anapiga msuwaki ,mwengine kavaa kanga moja anakwenda chooni sehemu ndogo,mwengine kawasha redio sauti kubwa,mama mwenye nyumba nae anaongea msijua kula vizuri tuu nakua na wageni wenye magari mjue nakulipa kodi nakufagia zamu ikifika,muache na kuchukua waume za watu manake hamna miko wengine hata anaewafadhili mnamchukulia bwana wake,mie nilibakia nimetoa macho na mijicho yangu ilivyokua mikubwa,nikamwambia shosti huku hamaa ntakusaidi kodi duu sijawahi kuona mama mtu mzima akiongea pumba kama yule....
 
Umenukumbusha shosti,nilienda kumuona shogangu tuliachana zamani sanaa baada ya kukutana nae akanikaribisha kwake

Hahaha, mama mwenyenyumba alaimwaga radhi.
 
Kuna kaka mmoja alikuja kusoma UDSM, alipangisha chumba Tandale. Alikuwa na girl friend wake wa long time, mtoto wa kisure basi mtoto akawa anakwenda weekend kwa jamaa, maji mnachota mtaa wa pili ndiyo kuna kisima, basi asubuhi mkaka akawa anakwenda kumchukulia babe wake maji ya kuoga, mwe wewe wa mama wasiache kumchamba, huyu ndiyo utamuoa huyu, mwanamke amelala wewe unakwenda kuchota maji.
 
Umenukumbusha shosti,nilienda kumuona shogangu tuliachana zamani sanaa baada ya kukutana nae akanikaribisha kwake
na alikua best yangu sanaaaa nikasema wavha weekend moja niende sasa kuelekezwa mpaka kufika ilikua shughuli,haya kufika wako wapangaji wenzie nikawa nimemchukulia zawadi,mara akatoa jiko kuanza kupika duu mara huyu anatoka anapiga msuwaki ,mwengine kavaa kanga moja anakwenda chooni sehemu ndogo,mwengine kawasha redio sauti kubwa,mama mwenye nyumba nae anaongea msijua kula vizuri tuu nakua na wageni wenye magari mjue nakulipa kodi nakufagia zamu ikifika,muache na kuchukua waume za watu manake hamna miko wengine hata anaewafadhili mnamchukulia bwana wake,mie nilibakia nimetoa macho na mijicho yangu ilivyokua mikubwa,nikamwambia shosti huku hamaa ntakusaidi kodi duu sijawahi kuona mama mtu mzima akiongea pumba kama yule....
Nyumba zingine kuna vitimbi. Unaweza kuhama kwa siku moja Kama hujazoea haya mambo
..........wenye nyumba wengine wazungu japo mnaishi nyumba moja mnaweza msionane hata miezi.mnaishi Kama familia no makelele....
 
Jamaa yangu alikuja kunitembelea, huyu jamaa yangu ana gari, sasa alipopaki mwenye nyumba akatoka akaanza kummind kwa nini anapaki bila kuuliza, eti ile ni sehemu yake ya kupaki kwa hiyo atoe gari pale, cha ajabu gari lenyewe halikuwepo siku hiyo nzima.
 
kuna babu mmoja nilikuwa nimepanga kwenye nyumba yake yaani yeye akifulia tuu anakuja kudai hela tena kwa jazba kama anakudai vile, Mungu si athuman nikapata nyumba yaan mwenye nayo hata hakumbuki kudai hela yake hadi astuliwe tuu kwamba asee njo uchukue hela yako.
 
Utakuta nyumba ndogo inadai pesa jazba zote anamazilia kwako kisa wewe mpangaji.
 
Jamaa yangu alikuja kunitembelea, huyu jamaa yangu ana gari, sasa alipopaki mwenye nyumba akatoka akaanza kummind kwa nini anapaki bila kuuliza, eti ile ni sehemu yake ya kupaki kwa hiyo atoe gari pale, cha ajabu gari lenyewe halikuwepo siku hiyo nzima.
Sasa mgeni wako atajuaje kama na yeye ana gari?
 
Back
Top Bottom