Kama unataka kwenda Comoro zingatia yafuatayo:
Kwanza uwe na passport ile kubwa (ya kitabu)
Visa unagonga hapa hapa siku hz (wana ubalozi wao hapa)
Chenji pesa zako kuwa Euro maana ndo wanazotumia kule
Usafiri upo wa aina mbili, ndege ATC go and return ni laki sita n sabini kama sikosei. Alafu kuna meli pale bandarini laki tatu na nusu.
Mji mkuu na wabiashara ni Moroni (ndio usafiri wote unaishia hapo, namaanisha ndege uwanja upo moroni na bandari yao ipo moroni pia.)
Kuhusu nyumba za kupanga kule zipo. Chumba kimoja utakuta Euro 60 kwa mwezi (ambayo ni kama laki na 30 hiv)
Ama unaweza kukutana na watz kule wakakusaidia pakulala (wapo wengi sana hasa wazanzibar)
Biashara unayoweza kupeleka kule;
Kama una mtaji wa kutosha peleka mchele (huu wa mbeya) unga wa sembe, ngano. Vitunguu, viazi mviringo. Au zile product za Azam (yale majuice au mo juice zile zinazouzwa mia tano huku)
Pia unaweza kupeleka magodoro, ng'ombe, korosho pia. Vyakula ndio vinaenda sana kule kuliko nguo.
Nadhani nimekujibu maswali yako mkuu