SoC01 Maisha kabla, wakati na baada ya chuo

Stories of Change - 2021 Competition

Karanga Lawfirm

Senior Member
Feb 10, 2021
161
165
John Karanga nikijana Wakitanzania aliyezaliwa mwaka 1993 mkoani Songwe wilaya ya Mbozi kata ya Vwawa. John alikulia Vwawa na baadae kuanza elimu ya msingi katika shule ya msingi Ichenjezya iliyopo mji mdogo wa Vwawa mwaka 2001.

Kama ilivyo ndoto kubwa ya wanafunzi wengi, nikufanikiwa katika maisha yao ya kielimu ili kuweza kufikia ngazi za juu za kielimu na hatimae kuweza kupata ujuzi ambao utawawezesha kupata ajira za kipato cha juu. Ndivyo hivyo hivyo pia ilivyokua kwa kijana John. John aliendelea kusoma kwa bidii ili kuweza kutimiza ndoto yake yakufikia elimu ya juu ili aweze kupata ajira nzuri. Mungu alijalia John alifanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2007 na baadae kufaulu na kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Isangu Mwaka 2008.

Mwanzo ulikuwa mzuri kwa John ambapo alisoma kidato cha kwanza na chapili katika shule ya sekondari Isangu, ambapo baadae alihama na kujiunga na shule binafsi ya sekondari Wiza iliyopo mji mdogo wa Vwawa. Safari ya John katika shule ya Wiza haikuwa nzuri kwani alishuka sana kitaaluma sababu ambayo ilichangiwa na makundi ya marafiki wasiofaa pamoja na uchanga wa shule hio katika ufundishaji. Kutokana na hilo John alifeli mtihani wakuingia kidato cha nne kwakushindwa kufikisha wastani uliotakiwa kwa wakati huo.

Safari ya John kielimu iliingia doa na ndoto za kufika katika ngazi ya juu kielimu ilipata misukosuko. Licha ya changamoto hio John hakukata taama, mwaka unaofwata John alijiunga na shule ya sekondari Ng'amba iliyopo mji mdogo wa Vwawa ambapo alirudia kidato cha tatu mwaka unaofwata. John alisoma na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2012 ambapo hakufanikiwa kufaulu. Baadae alirudia mtihani wa kidato cha nne nakupata alama zilizomuwezesha kujiunga na kidato cha tano.

John alijiunga na kidato cha tano katika moja ya shule kongwe jijini Mbeya. Akichukua masomo ya Historia Geografia na Kiingereza. Akiwa hapo John alipata bahati ya kutembelewa na rafiki zake waliomtangulia ambao walikuwa wakisoma vyuo tofauti tofauti nchi. Walimuelezea maisha wanayoishi vyuoni ambayo kwakweli yalimvutia sana John. Muonekano wao mzuri, simu pamoja na pesa za kujikimu walizopata kama mkopo zilimvutia sana John nakumpa shahuku kubwa yakutaka kufika walipo rafiki zake.

John akiwa kidato cha sita, alisoma kwa bidii ili aweze kufanikisha ndoto yake ya kujiunga na chuo kikuu. Alijiwekea malengo mazuri ya hapo baadae pindi atakapofanikiwa kujiunga na chuo kikuu. Ikiwa nipamoja na kutunza pesa atakayopata kwa mkopo ili aitumie kama mtaji wa biashara hapo baadae, kusoma kwa bidii ili apate ufaulu mzuri utakao muwezesha kupata kazi nzuri.

Mungu alimjalia John akajiunga na chuo kikuu mwaka 2017, pia akabahatika kupata mkopo kwa asilimia mia moja. Baada ya kufika chuo John alianza maisha ya chuo kwa kupanga na kujitegemea kwani alikuwa na pesa aliyopewa na bodi ya mikopo kwajili ya kujikimu. Mwaka wakwanza wa masomo John alisoma kwabidii kama alivyojiwekea malengo yake na kupata ufaulu mzuri. Baadae John aliingia mwaka wa pili ambapo alikutana na binti aitwae Neema mwenyeji wa Manyara ambapo John na Neema walianzisha mahusiano ya kimapenzi jambo lilopelekea John na Neema kuishi kama mke na mume. Maisha ya John yalianza kubadilika, pesa ikawa haitoshi tena, Neema akapata ujauzito na baadae kujifungua.

Jambo hilo lilipelekea John kujitwisha majukumu ya ubaba kwakuanza kujishughulisha na shughuli ndogo ndogo kwajili ya kujipatia kipato ili kukidhi mahitaji ya familia jambo lililo mpelekea John kushindwa kuhudhuria vipindi ipasavyo. Kutokana na uhafifu wamahudhurio John alifeli masomo yake nakushindwa kuendelea na chuo, jambo lililompelekea kurudi kwao Songwe huku akimuacha Neema na mwanae mjini Dar es Saalam ambapo Neema aliendelea na masomo yake.

Maisha ya John yalibadilika na kupoteza muelekeo, kwani John hakuwa na pesa wala cheti kutoka chuo alichosoma cha kumuwezesha kupata ajira ili aweze kujikimu angalau kwa kipato kidogo. John alibaki kuwa mzigo wa wazazi kwakuwa hakuwa na kazi yoyote ya kuingiza kipato. Ndoto za John kuhitimu chuo na kufaulu vizuri ili aweze kupata ajira nzuri ziliishia Songwe katika mji mdogo wa Vwawa.
 
Back
Top Bottom