Maisha haya, nyie acheni tu!

Maisha haya, nyie acheni tu!

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,569
Reaction score
2,584
Habarini za humu wenye jamvi, naomba nikunjue jamvi kwa mkasa wa dada mmoja mkazi wa sinza ambaye ni jirani yangu kwa jina anaitwa Angela.

Mnamo siku ya Jumatatu natoka zangu kwenye mishe mishe zangu nafika home napigiwa simu angela anaumwa yupo sinza palestina amelazwa kaishiwa damu na hali yake ni mbaya sana. Basi baada ya kupigiwa simu ikabidi nioge halafu nianze njia ya kwenda hospitali kumcheki huyo Angela, nafika pale hospitali nakutana na rafiki yake ambaye alimpeleka hospitali nikamuuliza vipi akaanza kunisimulia.

Asubuh alikuwa vizuri tu ila mchana akaanza kusema anajisikia vibaya kwa hiyo nikampigia ndugu yangu ni daktari Tanga, akasema nimpe dawa ya kutuliza na maumivu na dawa nyingine".According to huyo rafiki yake ni kwamba baada ya hapo akaanza kutapika na kubleed kabisa tena damu nyingi sana. Akaamua waende kituo cha afya kwa matibabu kufika pale akawekewa drip na kumpa huduma ya kwanza, wamekaa pale baada ya nusu saa akaambiwa atamfia pale so ndo akapelekwa huko Sinza Palestina.

Sasa baada ya yale maelezo mimi nikamuuliza kinachohitajika ni nini ili tujue tunafanyaje, basi akasena kuna gharama za vipimo na vitu vingine so ikabidi tuchange pale aendelee kupata huduma. Moja ya vipimo alivyopigwa ni ultrasound, sasa katika kuchukua majibu nikaona kitu cha kushangaza kwenye ile picha ikabidi kigoogle nikaona kitu kama abortion hivi sasa nikajiuliza inawezekana alijaribu kutoa mimba.

My assumptions were right pale alipokuwa admitted wodi ya wajawazito nikajua kumbe ni tatizo la mimba hili sio bure. Na ni kweli alifanya jaribio la kutoa mimba madaktari wakamsafisha.

Niancho jiuliza kwanini ndugu zangu wanawake mdange? Hadi mpate ujauzito na kuja kusumbua watu wengine? Cha ajabu hata akiba ndani hana na kudanga kote kule. Tafadhali jamii iianaglie hawa wadada.
 
Weye ndugu, mbona simulizi yako ilipaswa kuwa fupi isiyozidi mistari minne? (Nakaa Sinza. Kuna dada anaitwa Anjela ametoa mimba. Enyi wanawake,msitoe mimba ni hatari sana. Mnaweza mkakufilia ma-mbali mbali huko) Basi, ungekuwa umemaliza kutuhadithia.
 
Weye ndugu,mbona simulizi yako ilipaswa kuwa fupi isiyozidi mistari minne?(Nakaa Sinza.Kuna dada anaitwa Anjela ametoa mimba.Enyi wanawake,msitoe mimba ni hatari sana.Mnaweza mkakufilia ma-mbali mbali huko)Basi,ungekuwa umemaliza kutuhadithia.
Ndugu walipigiwa simu hawana chochote
 
NDUGU Yangu sio Kila mdangaji ni Malaya, wanapitia changamoto sana sana! Tuwaombee tu
Dah....Kuna kitu flani Hivi unakimisi....kwa kifupi mwanamke ni haki yake kupewa "Asante" dunia nzima.....hiyo udangaji, umalaya, uchangudoa no... ni maneno tu 🤣🤣🤣🤣
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom