Uko sawia kabisa.....
Kuna club moja nilienda bukoba, hadi saa saba usiku anapiga nyimbo ambazo hata hazieleweki..... nikachukia nikatoka kwenda zangu kulala japo nilikuwa na mzuka wa kubambiwa ile mbaya.
Ila kuna club nilienda mwanza ile iko underground juu kuna hotel, nilicheza mziki mwanzo mwisho, niliingia pale saa 4 usiku hakuna hata watu nikaondoka club saa 10 alfajir na hapo niliacha watu bado wanayarudi hehehehehee.
Napenda sana kucheza mziki, unachokisema nakuelewa vizuri, nafikiri baadhi ya wamiliki wanamwambia DJ afanye hivo ili wauze vinywaji, kumbe hawajui mtu ukicheka sana unasikia kiu utanunua tuu vinywaji vingi kuliko ukikaa bila kucheza.