Maisha BORA: Songea mfuko wa cement sh 20, 000 per bag!

mkuu usiwalaumu, imnawezekana kabisa walimchagua Dr Slaa, ila NEC walimchagua JK

mkuu hapo kwenye red. NEC walimteua jk, maana sikusikia wakisema rais mchaguliwa ila walisema rais mteule
 
Lakini kuna mikoa mengine ilikuwa inatia kichefuchefu mfano Pwani na Tanga watu maskini kufa mtu ukimuuliza mtu kwani ulimchagua JK anakuambia eti ni muislamu. Ukimtazama yeye nguo amevaa imetoboka halafu anakuomba buku aende akale yeye na familia yake. Sasa kweli unaweza kusema hawa wasilaumiwe. Wacha tu wapigike mkate ufikie Tshs 10,000,000, nauli 1,000,000 ndio akili za watanzania zitakaa sawa....

hawa watu ni tatizo mno
 
naungana mkono nanyie, atleast sisi wengine tunajimudu huu ndio ukweli tulikuwa tunalilia zaidi hao masikini zaidi, but wao wanadanganyika sana wakairudisha the dudu klinalowala, acha waumie hadi wajitambue, sionei mtu huruma wakalilie pale ikulu, mijutu masikini ukiiambia tuchange regime haitaki so tuwasaidieje? sitompa mtu msaada huku tanga kwani wameniangusha sana wagosi hawa na ni maikini mno! watajiju sasa
 
kuna mtu pembeni yangu hapa ni mtu wa makamo kavaa kofia ccm, tshirt ccm ananiomba nauli aende nje ya mji kidogo hapa tanga, nkamwuliza wewe ulkuja kufanya nini town? kasema alijiandikisha huku na alikuja mpigia JK kura yake, na sababu yake ati ni kuwa waliambiwa waiokoe nchi na makafiri so akapewa 10,000, now zimeisha anapita pita kuomba nauli, well nimehojiana nae ssana, sijampa hata sh moja, nikamuambia aende ofice za ccm kasema ameenda kaambiwa hawana hela za hivyo kutoa kwa kila mtu, imagine na amevaa full green!! watajiju hao masikini wanaotupeleka shimoni miaka nenda rudi, wenzao hela ya kuchange mboga aah tunayo! shida kwaoo!
 
source: TBC1 sijui wanalalamika nini hao hao ndio juzi wamepiga kura kuendeleza ujinga huo!sitaonea mtu huruma kwa lolote lifanyalwo na serikali ya ccm!

Ubongolala hivi hata wewe uliamini Slaa angeshika madaraka cement ingeuzwa shs 5000? hiyo bei ya kununulia ay ya kiwandani? na je kama cement ingekuwa shs 5000 mfuta ya disel na petrol ya kuusafirishia huo mfuko yangekuwa shs 150/= kwa lita? na mchele kilo moja ingekuwa shs 200? au hii ni sawa na ahadi ya kujenga barabara kandokando ya bahari? Umepewa akili fikiria kaka.
 
unaongea hujui nkodi wanazokata ktk hizi bidhaa, imekuwaje net ya sh 6000 inauzwa sh 500? mbona imewezekana acha kufikiria ndani ya box wewe, waza nje ya box pia na mawazo mgando acha, yeyusha akili hiyo
 
Msidanganyane na kufanywa wajinga kuna vitu vingine haviwezekani labda mfute kodi zote kwenye cement na kwenye mafuta na mpunguze gharama za umeme na serikali itoe rawmaterials kwenye viwanda wao kazi yao iwe ku process tu...........
 
2,000 USD Zimeshatengwa ili Chenge awe Spika wa Bunge

Wanataka Chenge awe spika kwa kila hali, Watahonga vibaya mno

HAkuna Rangi tutaacha kuona cc watanzania kipindi hiki cha 5yrs.

Petrol tayari imesha gonga 1,780 per lita ...............na bado ibaendelea kupanda
 
source: TBC1 sijui wanalalamika nini hao hao ndio juzi wamepiga kura kuendeleza ujinga huo!sitaonea mtu huruma kwa lolote lifanyalwo na serikali ya ccm!
Hivi haya maneno uliyosema umejiuliza juu ya uchakachuaji..........??? Au unawatupia lawama wao as if mchakato wa kura upo safi.........??? Mtu kushinda inaweza ikawa hata kwa kuchakachua..........
 
2,000 USD Zimeshatengwa ili Chenge awe Spika wa Bunge

Wanataka Chenge awe spika kwa kila hali, Watahonga vibaya mno

HAkuna Rangi tutaacha kuona cc watanzania kipindi hiki cha 5yrs.

Petrol tayari imesha gonga 1,780 per lita ...............na bado ibaendelea kupanda
Itaendelea kupanda........ kwa SONGEA tuuuu AU TZ nZIMA........??? au HATA ALIKO BONGOLALA.........??? BY THE WAY....................hivi huoni kuwa hiyo USD 2,000 uliyoiandika ni VIJSENTI TUUUUUUUU........???
 
Ubongolala hivi hata wewe uliamini Slaa angeshika madaraka cement ingeuzwa shs 5000? hiyo bei ya kununulia ay ya kiwandani? na je kama cement ingekuwa shs 5000 mfuta ya disel na petrol ya kuusafirishia huo mfuko yangekuwa shs 150/= kwa lita? na mchele kilo moja ingekuwa shs 200? au hii ni sawa na ahadi ya kujenga barabara kandokando ya bahari? Umepewa akili fikiria kaka.

Cement ya Pakistan inauzwa Dar kwa bei ya chini kuliko Twiga Cement na hii ni baada ya kusafirisha toka Pakistan mpaka Dar, kulipia kodi za serikali na kuweka faida juu. Kwa lugha nyingine kwa bei hii ya Twiga Cement hapa Dar ama tunalipia "inefficiencies" zao au wanapata "supernormal Profits". Hivyo mimi naamini kabisa tunaweza kupata Cement ya bei ndogo zaidi ya hii tunayolipa sasa hata kufikia Tshs 5000 waliyoahidi hawa waheshimiwa wa CHADEMA.
 
Ubongolala hivi hata wewe uliamini Slaa angeshika madaraka cement ingeuzwa shs 5000? hiyo bei ya kununulia ay ya kiwandani? na je kama cement ingekuwa shs 5000 mfuta ya disel na petrol ya kuusafirishia huo mfuko yangekuwa shs 150/= kwa lita? na mchele kilo moja ingekuwa shs 200? au hii ni sawa na ahadi ya kujenga barabara kandokando ya bahari? Umepewa akili fikiria kaka.

Kwa nini ishindikane Migodi ya madini inapewa Exemption ya mafuta na mambo mengi tu na baada ya hapo wanakuachia asilimia tatu na endapoa wakipata faida, kwanini ushindwe kukipa viwanda vya kutengeneza Cement nchini kwa manufaa ya maendeleo ya inch???

Kila kitu kinawezekana iwapo mipango ikiwekwa.
 
Unajuwa kuna watu kwa jinsi tunavyoibiwa wanaona huduma bure haiwezekani......................Hebu fikiri...........
Kagoda,
Mabango ya JK yamelipiwa na serikali,
Kiwira,
Bulyanhulu,
Buhemba,
Tanzanite,
Liganga.
Maliasili zooteeeeeeee ikiwemo Loriondo iliyouzwa,
Buzwagi,
Kabanga nikel,
Resolute,
Chenge,
Mafisadi,
Tulawaka,
Nyamongo,

etc..........etc.............

Hivi mnajuwa pale uwanja mdogo wa ndege wa Bulyanhulu dhahabu kiasi gani inaondoka kila wiki.........??? na CONCENTRATE kiasi gani inaondoka na malori pale mgodini.............????? BAKINI KUSHABIKIA SIASA NA KUONA KILA KITU HAKIWEZEKANI WAKATI WENZETU WANAKULA. HIVI NYERERE ALIWEZAJE.........??? Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi daftari likiisha unamwonyesha mwalimu na anakupa jipya............... HAYO YALIWEZEKANA BILA MATUMIZI YA MADINI, BILA UWEPO WA MAFISADI..................

KUNA MUUNGWANA KASEMA HAPO JUU......... NET YA TSHS. 6,000/=....INAWEZEKANA VIPI IUZWE TSHS. 500/= ................ nami naongeza.............inawezekana vipi watoto wadogo watibiwe bure....... na ishindikane kwa wengine...........???

ETI MWIZI (FISADI) ANARUDISHA ALICHOIBA NA ALIYEIBIWA (SERIKALI) ANAFANYA SIRI.....................halafu kuna mjinga yupo pembeni anashangilia........
 
Miaka mitano ikiisha watashika adabu.
Na hili ndo tatizo kubwa kabisa linalotukabili...................yaani tunadhani bei ya cement kule Songea si tatizo letu sote, bali la wanaoishi Songea........... wenzetu hapo Kenya........bei ya mkate sehemu moja linakuwa ni tatizo la wote hata kama wewe unanunua kwa bei rahisi.............AMA KWELI WAMETUDIVAIDI NA SASA WANATURULU.....................

Tunasahau kwamba kule tatizo ni bei ya cement........na uliko wewe UNASHIKISHWA ADABU NA BEI YA MAHINDI wakati wa kule Songea anayapata kwa bei rahisi......................TATIZO MANAWEKA SANA USHABI WA SIASA HADI MNASAHAHAU HAKI ZENU..................

KWA TAARIFA YAKO BAADA YA MIKA MITANO KILA MTU ATAKUWA KASHIKISWA ADABU..................... WEWE KWA HILI MWENZIO KWA LILE....................usijione upo salama
 
Mtakoma, na bado. Hadi ifike 2015 mfuko wa cement utakuwa umefika Sh 50,000 huko ungonini. Dr Slaa aliwaambia mkamuona hafai bali mkwere ndo bomba. Sasa mnalalamikia nini? Hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania tena na kwa kasi zaidi, ari zaidi na guvu zaidi.
 
Mjadala wote huu ni maisha magumu kwa watanzania wote. Na haya yote yanasababishwa na uongozi mbovu wa serikali. Dawa yake ni kuitoa madarakani na kuweka uongozi mbadala. Mwaka huu haikuwezekana ingawa wengi walikuwa na nia hiyo. Miaka mitano si mingi sana wala si michache sana. Tuanze kujiandaa sasa kuwatoa. Ahadi walizotua kwenye kampeni zao hawawezi kuzitimiza kwani zilikuwa kwa ajili ya kuwaadaa wapiga kura. Na wananchi wataona hivyo ifikapo 2015. Nasubiri kuona kiwanja cha ndege cha kimataifa kigoma na tatizo la maji kuwa historia dar.

Pia kwa kuwa wametumia kazi ya ziada kupata ushindi mwaka huu, 2015 tutakuwa makini zaidi kuwadhibiti ili kazi zao za ziada za kupata ushindi sizifanikiwe.
 
Hakuna lisilowezekana hapa duniani wewe sokomoko. Kama viongozi waliopo kwenye madaraka wanaona hawezi basi waondoke wapishe wengine wanaoweza. Sio kung'ang'ania tu madaraka wakati hawana uwezo wa kuleta mabadiliko kwenye maisha ya wananchi.
 
Back
Top Bottom