ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Wana JF,
Tunashukuru Mungu uchaguzi wetu umekuwa huru na haki. Sasa maisha baada ya uchaguzi yameanza rasmi.
Neno linalotamkwatamkwa sana katika kipindi hiki cha maisha baada ya uchaguzi ni "mawakala".
Napenda kuwakumbusha wanasiasa na vyama vya siasa kutambua yafuatayo kwa ajili ya chaguzi zijazo.
Unapomchagua wakala ni wajibu wako na chama chako kuhakikisha wakala huyo;
1. Anao uwezo wa kiafya kimwili na kiakili kufanya kazi hiyo.
2. Anao uaminifu na utayari wa kuifanya kazi hiyo.
3. Amepata mafunzo ya kumuwezesha kutambua wajibu na haki zake katika kazi hiyo.
4. Umeweka utaratibu wa kumpa support anapopata changamoto.
5 Umeweka utaratibu wa kumsimamia.
6. Umelinda maslahi yake binafsi.
7. Amefika kazini na kuifanya kazi.
Kwahiyo, wakala akishindwa kufanya kazi maana yake mgombea na chama chake hawana mfumo wa kuwapata, kuwaandaa na kuwasimamia mawakala. Ni aibu mgombea au chama kulalamika hadharani kuwa wameshindwa kusimamia watu wachache tu, hasahasa kwa chama kinachotafuta ridhaa ya kuongoza nchi.
Nawapongeza watanzania wote kwa uchaguzi mzuri.
Tuendelee kupokea matokeo rasmi kwa utulivu na amani.
Maisha baada ya uchaguzi yameanza, tujikite kwenye kuijenga nchi yetu.