mashishanga
JF-Expert Member
- Sep 16, 2016
- 611
- 429
Hicho kiko katika viapo vya kupendana ktk shida na raha, cha msingi aombe sana, hata hvo inaonekana aliolewa bado hajajitambua. Kwa maana nyingine alikurupuka. Tatzo kama hilo si la kuachana, ni la kutafuta ndugu au mtu wanayemwamini awe msuluhishi kati yao.Kupigwa sana kuhatarisha maisha yake.kuna kipindi alipigwa hadi kupoteza fahamu Siku tatu
NI KWA "HAI DIFINISHENI" MKUU!unasoma maandishi kwa 3D au HD
Math.. 5:32
Namaanisha fungu linaloelezea uasherati ni kulala/ kuoa/ kuolewa na ndg pasipo kujua.Math.. 5:32
Kuna kitu umekiongea na kimenigusa sana. Tunavunja agano la ndoa tangu tukiwa kwenye urafiki/uchumba na tunaendela tu hivyo hadi kwenye ndoa, bila toba wala kuziweka wakfu ndoa zetu (hatuweki misingi ya mahusiano yetu kwa Mungu), kinachokifuatia tunakijua wenyewe. "It's never a blessing if you started by sinning". Ila sisi kama kondoo tuliopotea tunarudishwa kundini na kila kitu juu ya maisha yetu kinafanyika kuwa kipya.Hicho kiko katika viapo vya kupendana ktk shida na raha, cha msingi aombe sana, hata hvo inaonekana aliolewa bado hajajitambua. Kwa maana nyingine alikurupuka. Tatzo kama hilo si la kuachana, ni la kutafuta ndugu au mtu wanayemwamini awe msuluhishi kati yao.
Tatizo la ndoa nyingi kuvunjika siku hizi ni kutomtanguliza Mungu. Ndoa ilivyoanzishwa, ni takatifu lakini ndoa za sasa tunaziendesha kibinadamu na kihisia. Tunaoa/Kuolewa kwa kusukumwa na hisia fulani, kitu ambacho badae ni tatizo kwa wanandoa.
Ndio maana ndoa nyingi za sasa hazina mibaraka kwa sababu tunavunja agano la ndoa tukiwa katika stage/hatua ya urafiki na uchumba. Na kama mtu unafahamu ulishazini kabla ya ndoa na haukutubu na kuungama kikamilifu na kumrudia Mungu, hata uweje, ndoa yako itakua ni matatizo tu.
Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
Haahah!!Ndoa haijaribiwi jaman kama mukuru asivyojaribiwa,viko vingi vya kujaribu lakin siyo ndoa mtapata laana
ipo talaka kwa wakristu kama sababu ni uzinzi,ukifanya uzinzi ukakamatwa au ukimkamata mwenzio na uzinzi na ushaidi uliokamilika talaka inakuhusu,hata kanisa ikigoma kuvunja ndoa talaka ipo,ukiishi na mtu mzinzi ni kufurahisha watu uambiwe ndoa bado ipo lakini ndoa ina muhusisha mungu,mungu anaona uzinzi hata ukaufanyie Kenya,na ukiachwa kwa uzinzi ukiolewa anayekuoa ana zini tu hata mkifunga ndoa kanis la uingereza ambapo hujulikani!Ndoa za wakristo mpaka kifo kiwatenganishe mkuu ila huyo dada mbona ataolewa sana naa kuachika hajafikisha 30 talaka tayari
From the very beginning, Mungu hakutaka kabisa talaka iwepo. Isipokuwa, kutokana na ugumu wa mioyo yetu, basi aliruhusu talaka under certain circumstances. Ingawa pia talaka sio kitu cha kuwa encouraged, isitokee tu kosa na mtu aka-opt talaka. Talaka inatakiwa kuwa last option baada ya series za vikao vya "kukiri, misamaha, kupatanishwa na kujirudi" kushindwa kabisa (unrepentant, serial cheater)ipo talaka kwa wakristu kama sababu ni uzinzi,ukifanya uzinzi ukakamatwa au ukimkamata mwenzio na uzinzi na ushaidi uliokamilika talaka inakuhusu,hata kanisa ikigoma kuvunja ndoa talaka ipo,ukiishi na mtu mzinzi ni kufurahisha watu uambiwe ndoa bado ipo lakini ndoa ina muhusisha mungu,mungu anaona uzinzi hata ukaufanyie Kenya,na ukiachwa kwa uzinzi ukiolewa anayekuoa ana zini tu hata mkifunga ndoa kanis la uingereza ambapo hujulikani!
Asante Heaven Sent,From the very beginning, Mungu hakutaka kabisa talaka iwepo. Isipokuwa, kutokana na ugumu wa mioyo yetu, basi aliruhusu talaka under certain circumstances. Ingawa pia talaka sio kitu cha kuwa encouraged, isitokee tu kosa na mtu aka-opt talaka. Talaka inatakiwa kuwa last option baada ya series za vikao vya "kukiri, misamaha, kupatanishwa na kujirudi" kushindwa kabisa (unrepentant, serial cheater)
Malaki 2:16
Maana mimi nachukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israel......
Kwa hiyo Mungu hataki kabisa wanandoa kuachana. Ila akaruhusu tu kuachana kwenye situation hizi
1. UASHERATI
Mathayo 19:3-9
6: Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7: Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8: Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9: Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
#(Mathayo 5:32)
Kwa hiyo kumbe kuna talaka kuja inayoruhusu kuoa/kuolewa tena (Re-marry), na kuna talaka isiyoruhusu kuoa/kuolewa tena
2. KUTELEKEZWA NA MKE/MUME ASIYEAMINI
1 Wakorintho 7:12-15
13: Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14: Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15: Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
Kwa situation ya huyo dada aloletewa thread, japo Mungu hajaruhusu talaka, nafikiri hata Mungu hapendi wala hafurahishwi na vipigo. "Mke ni mwili wako", sasa mtu anayempiga mkewe hadi kuzimia siku 3 ni anamconsider kweli mkewe kuwa ni mwili wake? Nani anayeweza kuupiga hivyo mwili wake?
Nafikiri mke after series za kuonyana, misamaha na kupatanishwa kushindikana, anaweza akaondoka na wanae kukimbia hizo abuses (kutengana kwa muda), but sio kuomba talaka. Anaondoka ili ampe huyo mume muda wa kujitafakari, kuomba msamaha na kujirudi, aachane na hizo habari za kupigana kabisa. Akisema abaki tu, hatuna uhakika na usalama wa maisha yake+ vile vipigo vinatraumatize sana watoto. Under this situation sidhani hata kama wakiachana wataruhusiwa kuoa/kuolewa tena
N:B baada ya kuachana make sure umetubu kwa kushindwa kutimiza Agano mliloliweka mbele za Mungu (mpaka kifo kiwatenganishe), coz honestly hatutakiwi kuweka Agano then tukashindwa kulitimiza. Mungu wetu ni mwaminifu anatimiza ahadi zake zote juu yetu, inakuwaje wewe umdanganye na kutotimiza ahadi yake kwako? So ikitokea basi make sure unavunja nguvu ya Agano lile, otherwise Agano litakutesa maisha yako yote
Kumbukumbu 23:23
Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.
Mathayo 12:36-37
36: Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.
Kuna waja ukiwaambia leo kuwa waikuwepo magaidi wa Kikristo watabisha niaje...Ni kweli kabisa mkuu, King Henry alipata mabinti kwenye ndoa yake ya kwanza, alitaka mrithi kwahiyo aliomba kibali cha Pope na kukataliwa, kutoka hapo Uingerezeza iliwatesa sana wakatoliki wote ambao hawakuwa tayari kubadili na kwenda Anglican. Hii ndiyo sababu kubwa ya uhasama wa Ireland na England.
Nijuavyo mimi ndoa ya kikristo haina talaka, ISIPOKUWA inaweza kubatilishwa kwa baadhi ya sababu zifuatazo;Habari,
Naomba kwa wenye uelewa mpana hasa kwa wakristo kuhusu MTU aliyepeana talaka na mumewe Je, anawezekana kuolewa tena kwa ndoa ya kanisani kama ilivyokuwa awali?
Ukizingatia MTU hiyo umri bado MDOGO huko Kwenye 20s tumsaidiaje MTU huyu ili asiangukie kwenye uzinzi?
Wakristo nisaidieni Tafadhali.
IKuna waja ukiwaambia leo kuwa waikuwepo magaidi wa Kikristo watabisha niaje...
Naukubali sana msimamo wa Irish Republic na kile chama chao cha kususa susa.
Vita haijaisha ujue. Mambo ya Brexit yamefufua upya madai ya Uskochi na automatikale Ireland... Tusichakachue mada ya watu aisee! Talaka inawazingua...I
Jerry Adams amekuwa mzee sikuhizi, jamaa aliwapelekesha sana Waingereza.
Wataomba poh tu subiri time will tell.Vita haijaisha ujue. Mambo ya Brexit yamefufua upya madai ya Uskochi na automatikale Ireland... Tusichakachue mada ya watu aisee! Talaka inawazingua...