Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Kweli nchi iko kwenye auto-pilot

Hapana. Kwenye Historia kuna mambo mengi sana.

Unaweza kuweka History kwalililo jema au baya. Unaweza kuamua chama (CCM) kinyang'anywe madaraka baada ya utawala wako. Hii itabakia kwenye historia ya nchi milele, na baada ya hapo unaweza kusema nilihamasisha demokrasia.

Marejesho, tulia tafakari utaelelewa kinachoendelea.

Rubani yupo amekaa kwenye kiti chake anaangalia lidege la CCM inavyoenda kuingia baharini. Yeye ana Parachuti ataifyatua ikikaribia kuzama.

Alamsik

FP
 
Mbona maneno matamu kama hayo hayakusikika kabla ya kitumbua kuingia mchanga ? Hawa wote ni wamoja, hakuna zaidi ya mwingine.
 
Japo hata nape siyo mtu wangu,
lakini maige anapagawa kukosa hela ya wizi
siku akiswekwa lupango ndo ataimba hayo
mashairi vizuri.
 
Asubiri Bunge lijalo la Bajeti,atoe hasira zake kwa kutoa hoja kali dhidi ya Serikali iliyo mtema tuone kama kweli yeye ni MAIGE.
 
Kiswahili bana
I am so sad about this silent plan to disquit Nape from his confort zone of pursuing his duties. There's circumtancial evidences prevailing showing a well structured sinister plan to portlay Nape as an arrogant and failure. Doesn't make any sense to throw the burden of recruiting party's memebers or stopping old old ones to move to Nape.

Nape has weakness like we other human being. But the act of putting his name behind every party's blunder is absolutely not acceptable.

If we start pointing fingers none will remain safe. Ezekiel Maige himself turmished the Party's image by his underpeformance as a Minister. He later circulated ambigious statements which he failed to defend. Now he is throwing another song! Shame upon you.
 
Maige anajitahidi kusecure nafasi yake kwenye mioyo ya wapiga kura wake esp kwa vile ameshachafuka anajaribu kujisafisha kwa kumtumia Nape na kujidai anaipenda CCm mo than all the party members, on the other hand anachosema si maneno matupu ka vile kuna kaukweli
 
sukuma culture...?

St. Ivuga tutake radhi kabla sijachafua hewa hapa jamvini. Ntakupiga BAN ya masaa sasa hivi! Nashangaa Msukuma gani anayelialia ovyo ovyo huyu! Huko sasa ni kujidhalilisha kwa nini asikae kimya? Utafikri kanyang'anywa urithi! Nyamb..ff zake!
 
Maige na Nape ni sawa na mchawi na msukule. Warudi kwenye shrine (baba mwanaasha) waelewane. Wanachafua kijiwe wakati wote wanakula hapo hapo
 
Hana lolote maige,faru wa jk toka south africa wameuliwa mikononi mwake alichukua hatua gani?nape watume tra wamchunguze na vilori 2 eti usd 20000 Kwa mwezi
Ni lazima nikiri kwamba katika historia ya nchi hii hajapata kutokea mtu m.p.u.m.b.a.v.u kama huyu Maige aliyedhani cheo ni urithi wa mali ya baba yake. Mawaziri wote wametulia yeye peke yake analia mpaka unajiuliza ana akili timamu? Alipokuwa waziri amekuwa akimponda Rais waziwazi akidhani atakuwa waziri milele. Kichekesho ni kwamba alikuwa anaota kugombea urais!!Nape endelea kuwatia adabu. Chama hiki ni taasisi na ungeogopa kama wanaotishia kujitoa ni waadilifu. Hivi kukimbiwa na mke muasherati kunauma nini? Maiga asidhani kwamba regional balancing iliyomuibua yeye ina maana ya kuwa na sifa kwa cheo hicho. Na sasa nawaomba radhi wale wote nilikuwa nadhani wanamuonea kwa kumuonea wivu kwa cheo chake. Dawa ya watu hawa ni kuwafikisha mahakamani na kuwafukuza kutoka kwenye chama!!
 
Hivi kupanda ndege ni ufisadi??

Kutumia helikopta kwenye kampeni je?
mkuu umeenda mbali, shida sio kupanda ndege bali uhalisia wa anayeongelewa. Wanaotetea wanyonge unawajua hata kabla ya kutamka neno moja.
 
Kutokana na mnyukano wa Maige na Nape, nimejifunza kuwa hata sisi wananchi tumeyumba, kuchanganyikiwa na kupofuka. Sasa hivi hatufanyi tena critical analysis vizuri ili kufuatilia mambo.

Mimi kwa mtizamo wangu naona mambo mawili kwa Maige...
(1) Maige alipokuwa waziri alisimamia serikali anayoongoza. Hilo lilipaswa kuwa hivyo hata kama ungekuwa wewe ...
(2) Baada ya kutolewa uwaziri, sasa amebaki na ubunge wa CCM. Sasa anaongea kama mwana siasa na mbunge wa CCM.

Tafsiri tuanazotowa kuwa "alikwina" kuyasema hayo yote kabla, hiyo ni kupuuza ukweli wa tofauti za majukumu, lugha na uwajibikaji wa Waziri na Mbunge.

Tukirudi nyuma kidogo tunaweza kuona ukweli mwingine, kwa wana CCM, huu ni ukweli mkubwa! Nape ni mshirika mkubwa katika kukiuwa chama. Matamshi ya kushikisha watu ukutani, na kuita watu gamba wakati haijathibitishwa kisheria ni kuwaonea watu. Ni kuwaonea watu kwa sababu CCM ni chama tawala, ndiyo kimeshika serikali, na serikali ina uwezo wa kushitaki watu wote wenye makosa ya jinai ili sheria ichukuwe mkondo wake. Chama cha siasa hakiwezi kuhukumu watu na kuwatangaza wahalifu bila mchakato wa sheria kufanyika.

Maneno ya Nape yameleta migawanyiko katika safu ya uongozi, fedheha kwa wanachama na kuonekana kama kuna namna ya kuoneana na kulinda baadhi ya kundi chafu lakini lenye nguvu zaidi ndani ya chama.

Maige, yaewezekana ana makosa ya utendaji, lakini ni vyema akishitakiwa na ushahidi utolewe mahakamani badala ya kumwita fisadi tu kwasababu amekutuhumu kuathiri chama katika kipindi hiki kigumu. Mimi kwa hapo nachelea kumtetea Nape. Lakini Maige, pamoja na frustrations zake, ni Mbunge wa CCM na lazima azungumze na watu wake na kuwaeleza upepo wa kisiasa unavumaje na kuelekea upande gani. Hna kosa. Majibu na tabia za Nape zitaendelea kukiumiza chama cha mapinduzi. Zamani tulimsikia Mh Lowasa akilalamika, tukamsikia Mh Aziz akilalamikia gutter politics na sasa Mangie...ugonjwa unazidi kuongezeka na mwisho utauwa chama hivihivi kama mchezo wa kitoto
 
Hello to JF Members, MAJIBU YA NAPE KWA HOJA HII

Nimefanya uchambuzi wa maelezo yaliyotolewa na Mhe. Maige sambamba na majibu ya Mhe. Nape na kubaini kuwa ni sawa na ngoma za jadi ambazo kila mtu hutaka kushinda.

Inajulikana tangu awali kuwa Nape amepewa nafasi ya Ukatibu Mwenezi, kazi ambayo imemwelemea kutokana na kutokuwa na uwezo wa kubuni mbinu mbalimbali za kuiimarisha CCM. Kutokana na uwezo wake, anadhani kuwa anafanya vyema, kumbe ni kukidhoofisha. Nasema hivyo kwa sababu nimefuatilia "arguments" zake kutokana na hoja mbalimbali ambazo amekuwa akizijibu, majibu yake ni mepesi na yasiyokuwa na mashiko. Mfano ni huu ambao ametolea majibu kuhusu shutuma zake kutoka kwa Maige.

Kwa upande mwingine, Maige amekuwa anaongea sana siku za hivi karibuni na mambo mengi ni kuhusu mambo ambayo CCM inayafanya kwa kushindwa kutekeleza wajibu kwa mujibu wa ILANI yao. Yote haya tunayasikia baada ya kupokwa nafasi ya uwaziri aliyokuwa nayo, na tunajiuliza alikuwa wapi siku za mwanzo hata kama alikuwa waziri? Kwa nini asiyaseme haya aliyoyaona akiwa kiongozi wa kitaifa, ayaseme leo? Au alikuwa amewekwa ndani ya chupa kama msemo wa Mbunge Mama Beatrice Shelukindo alivyonena?

Hata hivyo, rai yangu kwa wana CCM, wasipuuze asemayo Maige kwani wajue kuwa alikuwa jikoni na siri nyingi za jikoni anazijua ikiwa ni pamoja na michezo mingi michafu anaijua na sasa wasipokuwa makini ataanika yote ayajuayo na kuwaacha wenye dhamana kutotazamana.

Naanza na maneno haya kwa leo, as long as ndo mara yangu ya kwanza ku-post phrase ndani ya hili jungu kuu.

Mayame wa Mayame



.
[/QUOTE]

Join Date : 31st May 2012
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received0
Likes Given0
Karibu sana Jamvini, Naona umeanzisha ID mpya ili umjibu Nape tu. Hongera!
 
ninachopendea ccm ni kwamba wanagombana wao kwa wao...cdm inajipamba kupambana na ccm lakini wao ccm wanadundana wao kwa wao yani hapa i can imagine dr slaa amekaa kwenye kochi lake na a glass of wine anatabasamu tu maana kazi yake kasharahisishiwa na ccm wenyewe
 
I am so sad about this silent plan to disquit Nape from his confort zone of pursuing his duties. There's circumtancial evidences prevailing showing a well structured sinister plan to portlay Nape as an arrogant and failure. Doesn't make any sense to throw the burden of recruiting party's memebers or stopping old old ones to move to Nape.

Nape has weakness like we other human being. But the act of putting his name behind every party's blunder is absolutely not acceptable.

If we start pointing fingers none will remain safe. Ezekiel Maige himself turmished the Party's image by his underpeformance as a Minister. He later circulated ambigious statements which he failed to defend. Now he is throwing another song! Shame upon you.

Mbona English yenyewe unaielewa vizuri tu, au unajifunza english gani?
 
Back
Top Bottom