Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
MAJIBU YA NAPE KWA HOJA HII:

INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU (wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!

Huwa inauma na mafunzo kusema vibaya na wazalendo na wanyonge wenzangu, na imekuwa ni mafundisho mazuri kwangu. Lakini nikisemwa na mafisadi, wezi, watumiaji vibaya wa rasilimali za nchi, tena kwa kuumia tu kisa mirija yao imekatwa, kwangu ni faraja kubwa kwani inaonyesha vita dhidi ya matumizi ya rasilimali za nchi yetu inaenda vizuri na imekamata pazuri!

SITAKATA TAMAA, NITASONGA MBELE MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU. NCHI KWANZA VYAMA BAADAE!
Habari yenyewe:

na Ahmed Makongo, Kahama | Tanzania Daima


KATIBU wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye ametajwa kuwa gamba namba moja linalotakiwa kuvuliwa, kwa kile kilichodaiwa kutoa matamshi mengi ambayo yamekivunjia heshima na kukidhohofisha chama hicho.

Nape pia ameshutumiwa kwa kushindwa kwake kubuni mbinu za kuingiza wanachama na zaidi kupambana na wimbi la kuhama kwa viongozi, makada na wanachama wa CCM.

Shutuma hizo nzito zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige (CCM) jana wakati akizindua matawi mawili ya wakereketwa wa chama hicho ambao ni wajasiriamali, katika Kijiji cha Isaka wilayani hapa.

Maige alisema kuwa Nape amekuwa akitoa kauli ambazo si za msingi, zisizojenga bila kujua kuwa zinakidhohofisha chama hicho tawala.

Mbunge huyo ambaye amepata kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa la wana CCM wanaohamia vyama vya upinzani, ambalo ilitegemewa kuwepo kwa juhudi za makusudi za kuzuia chini ya usimamizi wa katibu huyo wa itikadi na uendezi.

"Kitendo cha CCM kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza anasema hajali na eti hao ni makapi," alisema kwa kushangaa.

Nape akihutubia vijana mjini Bukoba siku chache zilizopita, alidai kuwa hata kama wanachama wote watahama, yeye (Nape) atabaki peke yake na CCM haitakufa.

Alidai kuwa kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haiwezi kupuuzwa na kiongozi makini, na kuongeza kuwa zinahitajika busara na bidii za kuwapa moyo waliopo ili nao wasiondoke na si kuwasimanga.

"Jamani Nape anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama.

"Ninalolisema hapa lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilionao kwa chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama, tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema kabla mambo hayajaharibika?"

Maige alimwomba Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja kutumia nafasi yake kuwashauri wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya Nape.

Wakati Maige akitoa maneno hayo mazito, Mgeja alikuwa ameinamisha kichwa chake chini, lakini mamia ya wana CCM pamoja na wananchi wengine walishangilia kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Maige aliwalaumu viongozi wa CCM katika ngazi ya wilaya na kata, ambao wamekuwa na tabia ya kutowatembelea wananchi na kusikiliza kero zao, wakisubiri mpaka viongozi wa kitaifa.

Alisema tabia hiyo ni moja ya vyanzo vya wananchi kuichukia CCM.

"Jamani inakuwaje kiongozi mwenezi wa CCM kata ama wilaya anakaa kimya kabisa, hakuna kazi yoyote ya uenezi anayoifanya, hata kama katika kata ama wilaya yake itakuwa imetembelewa na wapinzani na wakamwaga sumu, wao hawajibu, wanasubiri mbunge ama diwani aitishe mkutano na wao hujitokeza," alisema.

Alisema ili kukabiliana na wimbi la mabadiliko, ni vizuri wana CCM wakakaa chini na kujipanga vizuri kwa kuwa kitu kimoja badala ya kugawanyika kutokana na maslahi binafsi.
 
Yule waziri aliyefukuzwa Uwaziri wa utalii na maliasili ameanza tambo mara hii kamvaa katibu mwenezi wa CCM( vuvuzela) na kudai anakibomoa Chama. Katumia pesa nyingi kuhakikisha stori hii imatoka kesho magazeti yote ya kila siku......vinema imaendelea...
 
Hakika sasa naweza kuamini CCM imevunjika vipande vipande. Hii ni hatari kwa chama kinachotawala.
 
Hapo chacha! Nape sogea hapa mara moja! Bahati nzuri huwa unafuatilia sana humu jamvini!
 
Hana lolote maige,faru wa jk toka south africa wameuliwa mikononi mwake alichukua hatua gani?nape watume tra wamchunguze na vilori 2 eti usd 20000 Kwa mwezi
 
Nape nimekushauri mara nyingi kuwa UNAPOONGEA USIMALIZE UBAKISHE MENGINE na USITUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO. muda Si MREFU utafukuzwa ccm kama Jambazi sugu, Hio ndo ccm ambayo kila mtu kafunzwa kuchafua wengine ili apate madaraka, kama ulivyopata Madaraka kwa kuwachafua watu na wewe utatoka kwa kuchafuliwa 2
 
Jambo moja lipo wazi....naona hivi sasa Maige amekuwa mkali mithili ya mbogo majeruhi wa kule kule alikokuwa kabla!!! Mbona kauli kama hizi tulikuwa hatuzisikii toka kwake kabla?! am very sorry with this guy....!!

Nadhani Maige aliamini he's doing a very great job pale maliasili! Inaelekea hakutarajia kabisa kukutwa na yale yaliyomkuta! Nina uhakika hata JK akiingia kwenye anga zake ni lazima amchane!!!

Saikolojia ya kawaida inanituma kwamba, baada ya Mama Mwangunga kupigwa chini ubunge (na hatimae uwaziri) na Maige kuchukua mikoba ya uwaziri wa maliasili basi alikamia aoneshe distinguished performance with excellent track records.....unfortuantely, kabla hajafika kokote kiasi cha kuweza kujipambanua kwamba alistahili uwaziri kamili tangu zamani; maige akakumbwa na yaliyomkumba na kuachwa mithili ya faru majeruhi!!
 
..................................watu wenyewe anaowahutubia ndio hawa wenye njaa hivi hata huyo Nape hawamjui ..wao akili yako ipo kwenye pesa waachiwe kitu kidogo basi
542941_4094164917922_245787864_n.jpg
 
Hii habari ningeikubali kama chanzo cha habari kisengekuwa cha NPR...
 
Ndo maana huwa nakataa vijana kama Maige kuonjeshwa Madaraka.
 
Mods unganisheni hii thread na ile ya Nape Gamba namba moja
 
Back
Top Bottom