Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Mavuvuzela wanapimana nguvu,wakati sie pembeni tunaokota points tu,kazaneni tu na najua kuna mwingine tena atajitokeza humohuo CCM kuunga kauli alizozitoa Maige
 
Nape wasikukatishe tamaa, kamua kamua kijana, kama sio wewe wananchi wangeijuaje NYINYIEM???
wasikutishe hao wahuni, piga kazi tutakupa nafasi 2015 NYINYIEM wakishakaa benchi, nawashangaa CDM wanakukashfu wakati unawasaidia.
 
Hakika sasa naweza kuamini CCM imevunjika vipande vipande. Hii ni hatari kwa chama kinachotawala.

Ukiona kwenye familia kila mtu ni mkubwa na anatoa matamko ya kumshutumu mwenziye ujue hiyo familia siyo tu imesambaratika bali haipo.
CHADEMA mkisikia haya mjue mnafagiliwa njia ya kuchukua nchi 2015 ninyi nyamazeni kimya stick to the goal songa mbele kwa mbele
 
Unajua Maige anaweza akawa na hoja ya msingi kabisa au kunakitu anakijua lakini kwakua hakusema enzi ni waziri kwa maslah ya kulinda meza sasa hiv watu hawamuelewi,mi nazani akisikilizwa na akachimbuliwa anamengi,mi najua mbali na ubadhilifu kwa kutumi report ya CAG lakin inaonekana kabisa kunakitu anakijua ambacho huwenda alikitaa na anaamini ndicho chanzo cha kumtoa kwenyd uwazi.Mtakuja kuniambia

WANAOTETEA meza wote ni watetezi wa maslahi yao binafsi na wale waliowateua na sio watetezi wa maslahi ya Watanzania. Katu kwangu hawezi kuwa mtu wa kupigiwa mfano kwavile tu aliacha kusema yale yenye maslahi ya taifa kwa lengo la kulinda meza....watu wa namna hii ni hatari kuliko huyo Nape. Kama kuna mambo aliyotakiwa kuujuza umma na kulinda maslahi ya Watanzania lakini alipata vikwazo kutokana na nafasi (meza) yake basi alitakiwa kwanza kuachia ngazi mwenyewe na kuanza kutujuza hayo maovu.....kinyume chake, kwa sasa ni ngumu kutushawishi tusiamini kwamba zake ni kelele za mfa maji ambae kutapatapa ni ada! Angalau basi, angevuta subra kisha ndo akaanza kubweka lakini kashindwa kutumia japo busara ambayo isingeweza kukosekana japo kwa mziwanda aliye ndani ya Serengeti Boys!
 
Maige hapaswi kumsema vibaya Nape eti anazoofisha chama, kwani ufisadi alioufanya Maige pale Maliasili unajenga chama au taifa kwa ujumla? Pia wananchi msalala mmelogwa na nanani? Mnamshangilia mwizi wa twiga wakati mwizi wa kuku mnamchoma moto. Kweli hii ni bongo lala.
 
hana usafi wowote ila ktk hili maige anaonyesha mfaano mbovu ndani ya chama kwa kuanza kumshambulia nape baada ya yeye kuondoshwa ktk uwaziri ilhali anatambua nape ni gamba siku zote.
Tuwe wakweli. Nape ni mmoja wa wanasiasa makini waliobaki CCM. Kinachomtatiza ni kuwa amezungukwa na uozo kila kona. Binafsi nikisikia Nape amehamia CDM, nitashanilia. Lakini nikisikia CDM imempokea Maige nitahuzunika sana.
 
Hivi nani yuko karibu na huyu Maige amshauri aanze ratiba za kwenda gym na kufanya mazoezi. Hii itamsaidia sana afya yake ambayo inaonekana kuwa na mgogoro (obesity) na pia itamuondolea msongo uliochochewa na kupoteza uwaziri.
 
tehe tehe tehe tehe tehe, kama ni mzalendo wa kweli aseme ni nani alisafirisha twiga wetu, story za Nape hazijengi, anataka kujiimarisha kwenye siasa, kama Nape anatumika inawezekana hata yeye anatumika.
 
INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU( wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!

Huwa inauma na mafunzo kusema vibaya na wazalendo na wanyonge wenzangu, na imekuwa ni mafundisho mazuri kwangu. Lakini nikisemwa na mafisadi, wezi, watumiaji vibaya wa rasilimali za nchi, tena kwa kuumia tu kisa mirija yao imekatwa, kwangu ni faraja kubwa kwani inaonyesha vita dhidi ya matumizi ya rasilimali za nchi yetu inaenda vizuri na imekamata pazuri!

SITAKATA TAMAA, NITASONGA MBELE MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU. NCHI KWANZA VYAMA BAADAE!
hapa kwenye red naona ni yale yale ya ujenzi wa mnara wa Babel, wote ni wamoja tu bali ndio hivyo hawasikilizani tena kwa lugha, 'mungu' wao UFISADI keshawachanganya.
Yanayotokea sasa yangelitokea miaka 20 au 30 iliyopita ingekuwa heri lakini yanatokea wakati 'kansa' ilishakula sehemu kubwa ya mwili ambapo itawapa kazi ya ziada watakaoingia baada ya CCM.
1Nape na ujumbe wake wakiwasili Uwanja wa ndege wa Bukoba.jpg 22.jpg

 
Nape ni kituko kweli hivi unadhani unaongea na vichaa au? Ni wanyonge gani unaowatetea wewe mbona hatuwaoni na wala hatujakuona hata siku moja ukifanya hivyo? Hiyo CCM tu si ya wanyonge any more unawezaje wewe kuwatetea wanyonge wakati chama chako kimejaa wezi na wabinafsi wa hali ya juu wasiojali maisha ya wanyonge wa Tanzania? Give us a break Nape ongea mengine please lakini si hili la kutetea wanyonge ogopa moto ndugu.
 
Maige hapaswi kumsema vibaya Nape eti anazoofisha chama, kwani ufisadi alioufanya Maige pale Maliasili unajenga chama au taifa kwa ujumla? Pia wananchi msalala mmelogwa na nanani? Mnamshangilia mwizi wa twiga wakati mwizi wa kuku mnamchoma moto. Kweli hii ni bongo lala.

Hata mimi nimebaki nimeduwaa..yaan eti Maige ni mzuri na mbomoa chama ni Nape?
Kosa la Nape liko wapi hapo, kama waziri ameshindwa kusimamia Maliasili za nchi ambacho ndio kilio cha wengi. Hawa mawaziri wanadhani ni kazi rahisi kuingiza wanachama?. Unawezaje kuingiza wananchama wapya kama serikali ambayo mnaiongoza imezingirwa na kugubikwa na ufisadi wa kutisha ukiwemo kutorosha maliasili za nchi?? Utawaambia nini wananchi ili wakuamini??..Maige aache porojo bwana!

'Chama legelege huzaa Serikali legelege and vice versa'.
 
Maige bana.....si atulie.....

We unaweza kutulia chumbani wakati unaona kabisa moto unawaka sebuleni kwako?, au hujui kama file la twiga na yooote aliyosema CAG bado yanatakiwa mahakamani?, Hapo kila mbinu lazima itumike hata ikibidi kuvunja nyumba na kugawana kokoto.


Nundu aliporudi jimboni akataka kusherekea wakamzuia, Mkulo nae anachunguzwa ila hataki Hosea aseme (mbaya zaidi na nyumba/kiwanja alichouza, wapangaji wanagoma hata kumfungulia mlango mnunuaji achilia mbali kuhama!),

Hii ni vita kamili, subiri kidogo
 
nape anafanya kazi ya CCJ ata kama maige naye ni mwizi lakini anasema kweli kuhusu nape,haiwezekani kiongozi unafurahi wanachama wako kuhama,ila furaha yake iwe fumbo kwa CCM kuwa dogo bado anapiga kazi za CCJ wala akili yake haipo kabisa CCM
 
Back
Top Bottom