Maige afichua siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige afichua siri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Jun 29, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

  Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

  Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.


  "Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."

  Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

  "Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

  Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

  Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

  Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

  Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

  Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

  Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

  Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.

  Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.

  Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

  Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga

  majira
   
 2. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ntarudi.....
   
 3. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Huyu mie naona baada ya kufukuzwa kazi, alienda kwa aliokuwa anawasikiliza wamkatie share yake wakamtolea nje. Alitulia hakula vua kutosha hivyooooo, sasa roho inamuuma. Akirudishwa kwenye uwaziri kesho basi ni ataiba vizuri from day one.

  Pole ulikuwa mtumwa wa hao vigogo ila ndo ukome kusaidia wezi na kutotumikia. Wananchi vizuri.
   
 4. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Maige anaposema hivyo inamaanisha Rais Kikwete hafai basi
   
 5. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kama vipi aame huko! Aamie CHADEMA apate haki za msingi na hata akiwa waziri atapata nafasi ya kupgania haki.
   
 6. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  "Roho inamuuma kutolewa katika uwaziri ndiyo maana anasema ovyo...." Mheshimiwa naomba kuondoa kauli hiyo ahsante
   
 7. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tatizo naona sasa lipo kwa Maige Mwenyewe,kukubali kutumika na kutumiwa na hao vigogo badala ya kuwatumikia wananchi.Madudu ambayo ungebaini na kuwaambia wananchi na jinsi ya kukabiliana nao ungeshinda vita maana wewe katika vita yako ungekuwa na wananchi waliowengi na Mungu wao ,kama ambavyo Magufuli anavyotenda kazi zake ,system haimpendi lakini ananguvu ya wananchi.Maige rudi kwa wananchi utubu vizuri na kukiri kutumika kama Condom.
   
 8. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  Muheshimiwa Maige anataka wananchi wamwonee huruma, wakamwombee kwa Mh Raisi Kikwete walau arejeshewe nafasi yake ya uwaziri, maana kila anapofikiria mikopo aliyochukua kwa bond ya mshahara wa uwaziri, kubakiza mshahara wa ubunge pekee hautoshi kulipa madeni maana ndululu zilizosalia ni chache. Pole Maige, ni ajali ya kisiasa tu
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mheshimiwa tundu lisu kauli hiyo si nzuri,na ujue nakuheshimu sana.
  chezea madaraka weye?
   
 10. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hapo simuelewi vizuri Maige anaposema aligusa maslahi ya vigogo ndio yakamfika yaliyomkuta anamaanisha kuwa Rais anawasikiliza hao vigogo kuliko waziri wake?
  Kama hivyo ndiyo inakuwaje ile kauri maarufu ya Mnyika. Naona kama anazidi kuithibitisha!! UDHAIFU KILA PEMBE
   
 11. b

  bdo JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  bahati hairudi mara mbili, imetoka, ila Maige anasaidia kujua uozo wa CCM
   
 12. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili swala linainekana linamsumbua sana rafiki yangu. lakini mi namshauri akae kimya kwani kwa kuendelea kulizungumza swala hilo anaweza akapotoka siku moja na hali ikawa mbaya zaidi.
   
 13. paty

  paty JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  chuki sina ila roho inauma - maige
   
 14. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ngoja nifikiri zaidi...
   
 15. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  angekuwa ni shujaa wa kweli kama anavyosema sasa basi angejiuzulu na hapo angejipatia sifa kubwa sana, lakini kusubiri hadi kupigwa chini ndo kila kukicha anatuchosha na viji-maneno vya kipumbavu, maige una nafasi nzuri ya kuwatumikia wapiga kura wako kwa maana ndio kazi ya msingi waliokupa
   
 16. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mfamaji............................
   
 17. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mbona haelezi ameweza vipi kununua nyumba ya bilioni 1.3 au zaidi na kulipia Cash wakati ni muda mfupi tu kateuliwa kuwa waziri na mshahara wake unafahamika?
   
 18. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  NI EZEKIEL MAIGE, ADAI ALIINUNUA KWA DOLA 410,000, LEMBELI APINGA, ASEMA ALIINUNUA KWA DOLA 700,000 TASLIMU
  Fidelis Butahe na Daniel Mjema
  SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

  Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).

  Awali, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate.

  Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hili kwamba Waziri Maige amenunua nyumba moja kati ya nne zilizoko sokoni.

  Hata hivyo, dalali huyo hakutaka kueleza alinunua nyumba hiyo lini na kwa gharama gani baada ya kueleza kuwa yeye si msemaji wa kampuni hiyo.

  “Nyumba zipo nne na mbili zimeshauzwa. Maige kanunua nyumba moja. Nyumba nyingine mbili bado hazijauzwa na kwa sasa tunamalizia kuziwekea milango na bustani,” alisema Athuman.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri Maige alisema hakununua nyumba hiyo kwa Dola 700,000 kama inavyodaiwa, bali alinunua kwa Dola za Marekani 410,000.
   

  Attached Files:

 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Huyu Maige anafanya Watanzania ni wajinga. Tokea ang'olewe anapiga kelele tu na wala hajishtukizii kwa nini hamna anaemsikiliza. Kama anajipenda ni bora akae kimya tu maana atazidi kujiharibia.
   
 20. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wacha kupiga kelele ngoja watu waone wenyewe,ili nikuelewe jiuzuru uanachama leo alafu uingie chama chocho ambacho unaamini kinapigania maslah ya watanzania ugombe ubunge ili upiganie haki ya watanzania vizur
   
Loading...