Mambo vipi wanajamvi wenzangu, hope mnaendelea vizuri kabisa pia kwa wale wakazi wenzangu wa jiji la DSM nafahamu kwamba tupo katika maandalizi ya kumpokea rais wa dunia Barack Obama na ujio wake kutoka Marekani, nisingependa niwachoshe sana kwani wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi, leo nimekuja na uzi wangu wenye kichwa cha habari kinachosema mahusiano ya wabunge hawa.?Mhh, nieleweke kwamba nimeleta huu UZI sio kwa lengo la Kisiasa au kwa kumkandia mtu ila nimeleta hili jambo ili tuweze kushare na kutoa tathimini kuhusiana na jambo hili ambalo nimepata taarifa zake ambazo nimeshindwa kuzihimili kuzificha katika kifua changu .
Kwa ufupi wiki kama mbili zilizopita nilipata nafasi ya kuzunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ziara ya kikazi, katika mikoa niliyotembelea moja ya mkoa ambao ulinifanya nilete huu Uzi hapa leo ni mkoani DODOMA ambapo niliweka kambi pale kwa muda usiopungua takribani siku tano, kwa ufupi pale Dodoma kuna binamu yangu ambaye yeye ni muajiriwa wa serikali ambaye anafanya kazi katika Bunge tukufu la Tanzania, kama mnavyojua karibu mgeni wenyeji wapone ndio ilichukua awamu yake, nilipata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali mkoani pale ikiwemo kutembelea chuo cha UDOM na maeneo mengine mengi kwani sikuwahi kufika katika mkoa huo, lakini katika hali ya kushangaza kuna rafiki wa huyu binamu yangu ambaye ni sista m1 hivi wa makamo, yeye anafanya kazi katika hoteli moja marufu sana pale Dodoma alikuja kumtembelea binamu yangu ikawa kama bahati akanikuta, mimi nikawa npo busy na Laptop yngu kitu cha Apple nafanya yangu, alipoondoka ndipo huyu binamu wangu akaamua kuning'ata sikio, ishu kamili ilikuwa hivi:
Binafsi nisingependa niwataje hawa wamama kulingana na heshima kubwa wanayopewa katika jamii lakini kwa mtu mzima mwenye uelewa anaweza kufahamu ninaowazungumzia, Kuna wamama wawili ambao wao ni wabunge pale Dodoma sema wapo vyama viwili tofauti na huwa ni marafiki wa karibu sana hata katika safari zao huwa hawaachani kama mkia, sasa yule mama wa makamo kaja kumpa umbea huyu binamu yangu kwamba kwa uchafu wanaoufanya sasa imekuwa too much, kwa ufupi hawa wabunge wawili wanamahusiano ya jinsia moja hata aina ya magari wanayotumia yamefanana ukiongezea na nguo mpaka cheni na vidani wanavyovaa , huo mchezo wanaoufanya watu wa kwenye mahoteli wanapofikia wameshawashtukia na hakuna siri tena, pia kuna kipindi m1 kati ya waheshimiwa hao aliwahi kumuweka kinyumba msanii m1 mkubwa wa filamu nchini kwa muda wa miezi takribani mitatu wakifaidi penzi hilo haramu katika hoteli moja jijini Dar es salaam.
Kusema kweli baada ya kumegewa huo umbea na kutajiwa majina ya hao waheshimiwa nilichoka kabisa na hata sikuweza kuamini kwamba wangeweza kufanya uchafu kama huu, nimeamini msemo ule unaosema dont judge a book by its cover, yaani hao waheshimiwa ukawaona kwa nje ni wasafi sana wanakubalika katika jamii lakini behind the scene madudu wanayofanya hata Mungu hapendi.
Namalizia kwa kusema kwamba hawa waheshimiwa wanaofanya haya madudu ni vyema wakabadili muelekeo wao wa maisha na kujirudi katika mstari unaofaa kwani endapo jamii ikaja kudhibitisha hili itawacost katika Maaisha yao na hata kupoteza heshima kubwa ambayo walikuwa wanapewa na wananchi wa Tanzania.