Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,334
Ndugu zangu Watanzania wenzangu, leo naomba niweke sawa juu ya Padre Pio wa Pietrecina, Italia na matumizi ya Jina Pio katika maisha yangu (Deogratius Pio Kisandu). Baba yangu mimi sio Pio bali Pio ni jina nililopewa Utawani kwa ajili ya maisha ya kitawa, ambapo ilipaswa hapo baadae nitakuwa naitwa PADRE PIO WA AFRIKA. Baba yangu mimi anaitwa NALIMI na jina lake la ubatizo ni ALEXANDER.
Kuhusu Padre Pio.
Padre Pio alizaliwa May 25, 1887, Pietrelcina, Italy na alifariki September 23, 1968, San Giovanni Rotondo, Italy. Padre Pio alizaliwa na kuitwa Francesco na alibatizwa kwa jina hilo hilo la Francesco, na baadae alijiunga na utawa wa Wafransisko wa kapuchin na alipofikia hatua ya Unovisi January 22 1903 akiwa na umri wa miaka 15 alibadilisha jina na kupewa jina la maisha ya kitawa akawa Pio, kuanzia hapo akawa anajulikana kama Pio mpaka anapata daraja la Upadre kwa jina la Pio.
Kuhusu Deo Kisandu.
Deogratius Kisandu ameanza huduma za Kimungu akiwa na miaka 12 kama mwana VIRAFRA ( Vijana Rafiki wa Mt. Fransisko wa Asizi) jimbo katoliki la kahama na mwaka 1998 alijiunga na Utawa wa shirika la kifransisko la Ndugu wadogo wa Afrika lililopo Morogoro na kupangiwa Convent ya Kiroka, akiwa huko pamoja na watawa wenzake yeye aliamua kuishi maisha ya mfumo wa Padre Pio na kuomba apewe jina la kitawa kuwa Pio ili hapo baadae akipata daraja la Upadre basi atakuwa anaitwa Padre Pio wa Afrika, matengemeo yangu ni kuja kufanya mambo makubwa barani Afrika kama alivyofanya Padre Pio kwa wakati wake huko kwao Italia. Hata hivyo nilianza kutumia Deogratius Pio Kisandu, kwa maandalizi ya Pio wa Afrika. Lakini malengo yangu yalikwama kutokana na mazingira na kurudi mtaani, ambako jina hilo liliendelea mpaka elimu yangu ya Sekondari.
Kuhusu Kuapa.
Kutokana na mkanganyiko wa ndugu na jamaa wa kutokujua mfumo wa maisha ya kitawa niliamua kwenda kula KIAPO kwa Wakili ili kuondoa jina hilo la kitawa ambalo wengi hupotosha kuwa nililipachika bila kujua nilikuwa utawani. Nimeambatanisha hapa kiapo changu, Picha ya Padre Pio mwenyewe ambaye kwa sasa ni Mtakatifu ndani ya kanisa katoliki na picha yangu pia na birth certificate. Wengi wananiuliza kwanini natumia jina la NALIMI na nisitumie ALEXANDER, baba yangu Official Name yake ilikuwa ni NALIMI ISMAIL KISANDU hayo majina mengine yamekuja ukubwani, mzee wangu amebatizwa akiwa mtu mzima miaka ya 70s na hivyo hata nyaraka zake na ndoa aliyofunga na mama angu alifunga kwa jina lake lakuzaliwa na sio la ubatizo.
Nilipokuwa nasoma sekondari wengi hawakujua kama niliwahi kuwa mtawa na ndio maana nimepata misukosuko mingi sana.
Ndimi; Rev. DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.
KIJAKAZI CHA UKWELI