Mahusiano ya padre Pio wa Italia na Deo Kisandu wa Tanzania

Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
Ndugu zangu Watanzania wenzangu, leo naomba niweke sawa juu ya Padre Pio wa Pietrecina, Italia na matumizi ya Jina Pio katika maisha yangu (Deogratius Pio Kisandu). Baba yangu mimi sio Pio bali Pio ni jina nililopewa Utawani kwa ajili ya maisha ya kitawa, ambapo ilipaswa hapo baadae nitakuwa naitwa PADRE PIO WA AFRIKA. Baba yangu mimi anaitwa NALIMI na jina lake la ubatizo ni ALEXANDER.

Kuhusu Padre Pio.

Padre Pio
alizaliwa May 25, 1887, Pietrelcina, Italy na alifariki September 23, 1968, San Giovanni Rotondo, Italy. Padre Pio alizaliwa na kuitwa Francesco na alibatizwa kwa jina hilo hilo la Francesco, na baadae alijiunga na utawa wa Wafransisko wa kapuchin na alipofikia hatua ya Unovisi January 22 1903 akiwa na umri wa miaka 15 alibadilisha jina na kupewa jina la maisha ya kitawa akawa Pio, kuanzia hapo akawa anajulikana kama Pio mpaka anapata daraja la Upadre kwa jina la Pio.

Kuhusu Deo Kisandu.

Deogratius Kisandu ameanza huduma za Kimungu akiwa na miaka 12 kama mwana VIRAFRA ( Vijana Rafiki wa Mt. Fransisko wa Asizi) jimbo katoliki la kahama na mwaka 1998 alijiunga na Utawa wa shirika la kifransisko la Ndugu wadogo wa Afrika lililopo Morogoro na kupangiwa Convent ya Kiroka, akiwa huko pamoja na watawa wenzake yeye aliamua kuishi maisha ya mfumo wa Padre Pio na kuomba apewe jina la kitawa kuwa Pio ili hapo baadae akipata daraja la Upadre basi atakuwa anaitwa Padre Pio wa Afrika, matengemeo yangu ni kuja kufanya mambo makubwa barani Afrika kama alivyofanya Padre Pio kwa wakati wake huko kwao Italia. Hata hivyo nilianza kutumia Deogratius Pio Kisandu, kwa maandalizi ya Pio wa Afrika. Lakini malengo yangu yalikwama kutokana na mazingira na kurudi mtaani, ambako jina hilo liliendelea mpaka elimu yangu ya Sekondari.

Kuhusu Kuapa.

Kutokana na mkanganyiko wa ndugu na jamaa wa kutokujua mfumo wa maisha ya kitawa niliamua kwenda kula KIAPO kwa Wakili ili kuondoa jina hilo la kitawa ambalo wengi hupotosha kuwa nililipachika bila kujua nilikuwa utawani. Nimeambatanisha hapa kiapo changu, Picha ya Padre Pio mwenyewe ambaye kwa sasa ni Mtakatifu ndani ya kanisa katoliki na picha yangu pia na birth certificate. Wengi wananiuliza kwanini natumia jina la NALIMI na nisitumie ALEXANDER, baba yangu Official Name yake ilikuwa ni NALIMI ISMAIL KISANDU hayo majina mengine yamekuja ukubwani, mzee wangu amebatizwa akiwa mtu mzima miaka ya 70s na hivyo hata nyaraka zake na ndoa aliyofunga na mama angu alifunga kwa jina lake lakuzaliwa na sio la ubatizo.

Nilipokuwa nasoma sekondari wengi hawakujua kama niliwahi kuwa mtawa na ndio maana nimepata misukosuko mingi sana.

Ndimi; Rev. DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.

KIJAKAZI CHA UKWELI
 
Attachments

Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,288
2,000
Hapa Tanzania wewe ni nani hasa?

Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,837
2,000
Alianza kuuukana Ukatoliki
Akaja na kuushambulia ulokole,
Akahamia waraka kwa Askofu Pengo,
Akaja na nia ya kuandika Biblia mpya,
Akarudi tena na Mtakatifu Pio!

Huyu MTU ni MGONJWA wa AFYA ya AKILI!...asaidiwe.

Kama mtadharau tahadhari hii ninayoitoa hapa, wazazi wa watoto anaowafundisha Kule Mkolani/Buhongwa sekondari Mwanza kunasiku mtawashuhudia katika vyombo vya habari wakitapika POVU!
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
image.jpeg
image.jpeg
Deogratius Kisandu habari za siku....Ninakusalimu kwa jina la Mtakatifu Fransisco wa Assis

Huyu Deo toka alipotoka ndani ya Shirika la Ndugu wadogo la Padre Ricardo(Pekupeku) pale Morogoro amekuwa kama chizi.

Hii ni kwa sbb ya kuvamia imani na kuzama ndani ya imani wakati akili ikiwa haijakomaa.Padre Pekupeku na aina ya maisha yake ukikaa naye lazima uote uchizi tu.

Maana ni mwendo wa kuvaa ndala,kula viporo,kulala chini kwenye ngozi na kushinda shambani kulima na kufanya kazi.Usafiri ni mwendo wa miguu au baiskeli(kwao pikipiki na gari ni kama anasa)

Ukiishi maisha haya hata kwa miaka miwili,kama una imani ya kuungaunga,lazima uwe "chizi" kama Deogratius Kisandu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom