Mahusiano, mapenzi, urafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano, mapenzi, urafiki

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Masanilo, Jan 2, 2011.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwanza nianze kwa kuwatakia Mwaka mpya 2011 uwe wa fanaka na mafanikio. Kwangu Mwaka uliyopita ulikuwa na changamoto nyingi sana ila nashukuru Mungu kwa yote.

  Leo nitapenda zungumzia silaha zitumikazo kwenye kuangamiza mahusiano katika ndoa. Urafiki wa kimapenzi hudumu zaidi na kuwa na faraja pale tendo zima takatifu la ndoa linapofanyika kwa maridhiano ya wote. Huleta matatizo iwapo mwanamke anatumia sex kama silaha, siku akichukia basi mnapeana migongo ama mzungu wa nne. Mara nyingi wadada wanaotumia njia hii husababisha wenzi wao kutafuta wagombea wenza. Tendo la ndoa ni muhimu katika kuboresha mahusiano tafiti nyingi zimeonyesha hilo, sitaki kurudia umuhimu wa sex kwenye maisha ya kila siku. Wanawake wanaotumia Ngono kama silaha mara nyingi hawadumu kwenye ndoa zao maana hujifananisha wao na kama chombo cha burudani ambayo anaweza mpatia mteja mwingine.

  Ulevi kupindukia, pamoja na kuwa na madhara kiafya pombe husababisha kuyumba kwenye suala zima la ndoa. Wanaume walevi wengi wao wamekuwa hawana uwezo wa kukidhi haja za kingono kwa wenzi wao. Wanawake waliolewa na wanaume walevi wanaongoza kwenye suala zima la cheating, tafiti zinaonyesha hivyo.

  Kudumisha ndoa cha muhimu ni kusikilizana na kupeana kile roho na matamanio ya mwili yanachohitaji. Sababu za kichwa kinauma, leo sijisikii ama baba anarudi amelewa kila siku na kuishia lala sebuleni ni hatari sana kwenye ndoa.

  The Most Rev Masanilo ni mtafiti huru aliyebobea katika masuala ya Mahusiano, mapenzi na urafiki
   
 2. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ahsante Baba Mchungaji.
  Wanaume nao wanatumia pesa zao kama silaha kwenye mapenzi...kwa njia 1 au nyingne.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Silaha ninazozungumzia hapa ni kumnyima mwenzio tunda kama kumkomoa hivi!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  "Nina mwezi wa 3 sasa sijamruhusu kunigusa"...!
  Ni jana tulikuwa na mkasa wa aina hii ukiwa umeletwa na mdada ambaye ni family friend wetu, kisa amepata habari kuwa bwanake ambaye anafanya kazi na kontrakta wa barabara ya Arusha-Namanga, ana mahusiano na mwanadada mwingine...

  Kwa ufupi ni wazi silaha hiyo ya kunyimana tendo takatifu la ndoa ni ya hatari sana...maana party inayolalamika lazima itatafuta namna fulani ya kumkomoa mwenzie kwa kuwa na mahusiano ya tofauti nje ya ndoa, halafu meli yote inakuwa inazama taratibu...
  Maongezi ni ufunguo...familia zipate wakati muafaka wa KUSEMEZANA...kwa mazuri na mabaya, hapo mndipo miarobaini ya shida zote itatolewa.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  "....Nina mwezi wa 3 sasa sijamruhusu kunigusa"...!

  Ni jana tulikuwa na mkasa wa aina hii ukiwa umeletwa na mdada ambaye ni family friend wetu, kisa amepata habari kuwa bwanake ambaye anafanya kazi na kontrakta wa barabara ya Arusha-Namanga, ana mahusiano na mwanadada mwingine...

  Kwa ufupi ni wazi silaha hiyo ya kunyimana tendo takatifu la ndoa ni ya hatari sana...maana party inayolalamika lazima itatafuta namna fulani ya kumkomoa mwenzie kwa kuwa na mahusiano ya tofauti nje ya ndoa, halafu meli yote inakuwa inazama taratibu...
  Maongezi ni ufunguo...familia zipate wakati muafaka wa KUSEMEZANA...kwa mazuri na mabaya, hapo mndipo miarobaini ya shida zote itatolewa.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ni tatizo kubwa sana hili! Mwezi wa tatu hawajagusana unategemea kweli hao hakuna anayegusa nje? Kuna wadada mkikosana ama akisikia chochoko zozote mtaani basi anahama chumba, na kukwambia hali yangu kiafya si nzuri kabisa nina breed Mwezi mzima lol?
   
 7. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Zote ni silaha....kukomoana!
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  thanx jumar,
   
 9. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Swali, kama mwanaume ameoana na mwanamke Rasmi yaani kwa Ndoa au harusi. Kwa bahati wakazaa watoto angalau 2. je Wakija kuachana tatizo linakuwa ni kukosa uvumilivu, au shetani ameingilia ndoa.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu inategemea na sababu! Kama ni uzinzi basi ndoa hiyo is beyond repairable hakuna kusingizia shetani
   
 11. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ndoa nyingi huingia matatizoni kwa kunyimana Tunda!
  Masanilo uliyoyasema ni ya kweli
  Nakutakia Maisha mema kwa Mwaka 2011 uwe wenyewe utafiti wa hali ya Juu!
   
 12. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Mchungaji asante lakini mimi naona wadada ufanya hivyo kwasababu yawezekana umemkwaza hivyo sidhani kama ummkwaza bado utake show upewe utapewa mgongo tu!!sasa kama umemkosea bado ukanyimwa show ukaona suruhisho latatizo lenu nukwenda kumtafuta mgombea mwenza utakuwa umepotoka!! nimtizamo wangu.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Heri ya Mwaka mpya Rev Masa,

  Hili suala ni gumu sana mkuu. Ingawa sex inatakiwa kuwa immotional deal, mara nyingi watu wamelifanya kuwa physical zaidi na kupoteza maana yake ya msingi.

  Kuna dada mmoja nilisikia habari zake kuwa yeye anaamini sex ni sawa na kumgusa mtu mkono na alikuwa tayari kutoa kwa mtu yeyote... A very complex business ingawa hatuwezi kukwepa kununua shea katika hizo kampuni!
   
 14. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kutumia sex kama silaha ni makosa sana,,hata kama kuna makwazo ni muhimu kuongea na kutatua tatizo,,,lkn mchungaji kuna wanandoa wanatengana chumba kabisa kutokana na chronic cheating,,hii unaizungumziaje?
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Duuuh hii iko complicated sana! Sasa huyo dada akikutana na vijana wa sasa mikono si itaota sugu kwa kusalimiana mara kwa mara? Kazi kweli kweli
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kutengana vyumba nadhani si suluhisho! Ningependa wakae chini wamalize tatizo. Kuna Dr mmoja mkoa wa Shinyanga alikufa akiwa chumbani kwake bila mkewe kujua kwa siku mbili, sababu za kutengana.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mbona bado anakata mitaa? Ukipenda naweza kukutumia contacts zake labda unaweza kumpatia ushauri nasaha!
   
 18. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  "Ingawa sex inatakiwa kuwa immotional deal, mara nyingi watu wamelifanya kuwa physical zaidi na kupoteza maana yake ya msingi." upendo katika ndoa ni muhimu zaidi, mapenzi ni zaidi ya tendo la ndoa. mapenzi ni kauli nzuri, na maneno kama samahani, asante na mawasiliano. Mawasiliano ni kwa kumwambia mwenzio kile unachojisikia kama hupendi hiki, au unaudhika kwa jambo fulani au unapenda kitu fulani. Pia uvumilivu na kuacha anasa vinadumisha ndoa hasa akina dada zetu, msishindane kwa mavazi, hereni, au mapishi au kwenda out. ishi kulingana na kipato cha Mume wako. ukiepuka anasa, vishawishi utavipata wapi????
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahahah huyo hawezi nielewa labda nami nisalimiane naye kwa kugusana mikono! Hahahahahahahahhh
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii kitu ni biashara ya hovyo sana. Yaani mtu anaweza kuwekeza mtaji wake hata kama anajua fika toka rohoni kwamba kampuni yenyewe iko mahututi.

  Tatizo langu ni watu kujidai kuwa wanaweza kuisha na matatizo ya kimahusiano bila kuchukua jitahada za kuyatatua kwa kudhani kuwa yatajimaliza yenyewe. Kwangu mimi natumia mtindo wa zege halilali. Kila kitu kinaisha siku hiyo ili panapowezekana siku mpya ianze na mambo mapya. But...ni kazi ngumu sana, tena kwetu sisi wanaume wa kibongo kwani wakati mwingine inatutaka kujishusha na kuwapigia wenzetu magoti! Na ukizingatia mila zetu zimetuaminisha kuwa wao ndio lazima wapige magoti na kulilia wanaume siku zote..

  Afadhali safali yangu ilianza 1947, sijui hawa dot.com wanakwenda kwendaje!
   
Loading...