CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 687
Ndugu zangu wana JF
Leo nina kitu nataka tujadiliane
Maofisini au makazini tunafahamiana na watu wa aina mbalimbali, kuanzia makabila, dini, matabaka, mpaka tabia. Na hata mashuleni na mavyuoni. Kwa mchanganyiko huu tunajikuta tunajenga urafiki na watu mbalimbali. Ngoja nitoe kilichonituma nipost hii topic.
Kule bandarini (TPA) kuna mzee mmoja anaitwa Kirondo Manyanya (his official name) ana umri upatao miaka 48 sasa. Ana watoto wakubwa wa3. Siku moja alimuaga mke wake anaenda kazin siku ya Jmosi ambayo anawahi kurudi. Mke akaingiwa na wasiwasi baada ya kuona mume wake kachelewa kurudi, akawaomba watoto wake wawili waende kazini kwa baba yao maana huenda akawa kapata matatizo huku wao hawajui. Watoto kufika mapokezi, baada ya salamu wakauliza:
"Tumekuja kumuona Mzee Manyanya, yupo?"
Wakajibiwa: "Mzee Manyanya?? Mbona hakuna mtu wa jina hilo hapa? Kwani mnamjuaje"
Wakasema: "Ni baba yetu, anafanya kazi hapa muda mrefu sana"
Basi yule mtu wa mapokezi akaamua amuite mfanyakazi mmoja amuulizie kama anamfahamu Mzee Manyanya.
Yule mfanyakazi akajibu: "Eeh ndio namfahamu"
Yule mtu wa mapokezi akashangaa! "Hee! Mbona simjui??"
Akajibiwa: "Si ndo yule Mzee wa Kujambisha, kwanza nani anamtaka maana hapa hajulikani kwa jina hilo bali ni Mzee wa Kujambisha"
Yule mapokezi akamwambia ni watoto wake. Basi wakaruhusiwa waingie ndani.
Basi yule mfanyakazi akawa hajui alipo, akaamua kuchukua viganja vya mikono yake akabana na mdomo ili ajambishe: "Brruuuuuuuuuuuu"
Mara akasikia jibu: "Wee K*mamakooo"
Kwa kufuata jibu na sauti lilipotokea akawaambia wale watoto: "Baba enu yupo upande huu"
Kufika eneo hilo kukawa na makontena mengi, hawajui alipo. Akajambisha tena: "Brruuuuuuuu"
Wakasikia tena jibu: "Wee K*maaa, unafi*wa"
Basi akajua, huyo mzee yupo kontena lipi akawapeleka tena wale watoto.
Kufika kwenye kontena karibu kabisa na alipo Mzee Manyanya, yule mfanyakazi akajambisha tena: "Bruuuuuu"
Yule Mzee akafura kwa hasira, akagonga lile kontena kwa nguvu na kumfuata aliyejambisha huku akitukana matusi ya nguoni mfululizo.
Ile anatoka tu akakutana uso kwa uso na watoto wake!!!!! Akaamua apoe! Akawauliza: "Mmekuja kufanya nini?"
Wakamjibu mama yao kawatuma waje kumuangalia.
Basi akawaambia yuko salama waende nyumbani. Mzee akaanza kuwasindikiza watoto wake nje, ghalfa tena yule mfanyakazi akajambisha tena: "Bruuuuuu". Yule Mzee kama kawaida, akamwaga matusi mbele ya watoto wake.
Sasa huo ni mfano tu wa baadhi ya majina ambayo watu huitana makazini, maofisin au hata mashuleni na mavyuoni kutokana na mazoea fulani waliyojenga kwako au tabia fulani uliyonayo. Wengine huitwa DOGO, KICHWA, EM BII OO, FISADI n.k.
Je haya majina tunayadhibiti vipi hususani mipaka yake? Kama ni jina la kukudhalilisha tunachukua hatua gani?
Anakuja mgeni chuoni kwako, kazin kwako anasikia unaitwa "Wee kindimu cha jukwaa, leo una wageni ??" Unajisokiaje kudhalilika hivi??
Maoni yetu tafadhali.