Mahusiano Mabaya baina wanafamilia na wadada wa kazi ni moja ya sababu za ukatili kwa watoto wetu majumbani

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,551
12,416
Ukatili unaofanywa na wadada wa kazi dhidi ya watoto majumbani unaongezeka siku hadi siku, lkn huenda bila kujua sisi kama wanafamiia tunaweza kuwa chanzo kizuri cha ukatili huu.

Hata hivyo baadhi ya wadadisi wanabainisha kwamba mojawapo ya sababu za ukatili huo ni kama ifuatavyo;

1. Wakuu wa kaya hasa akina mama kukosa upendo kwa wadada wa kazi
Unakuta mama kila anapokuwa nyumbani basi hataki kbs kushuhudia dada akitoa hata tabasamu hata na watoto anaowalea kutwa nzima, kutwa kugombeza, jambo dogo la kumwelekeza basi atagomba na kumtukana matusi tena mbele ya watoto , jambo hili huleta simanzi kwa wadada na hatimaye hugeuka wakatili bila kujua ukatili ule waufanyie kwa nani ndipo baadae hupata mahala pa kurejeshea machungu yao ambako ni kwa watoto wadogo.

2. Mahusiano Mabaya ya wazi baina ya wakuu wakaya-Majibishano na Ugomvi baina ya wakuu wa kaya.
Majibishano ya maneno na ugomvi wa waziwazi baina ya wakuu wa kaya humfanya dada wa kazi kuamini hayo ndiyo aina ya maisha wanayopaswa kuishi wanafamilia hao na hapa waathirika wakubwa huwa ni watoto.

3. Ucheleweshaji wa stahiki au stahiki duni kwa dada wa kazi
Wakuu wengi wa kaya wamekuwa wakiwalipa mishahara midogo wadada wa kazi lkn pia kwa kuchelewa hata zaidi ya miezi 3 au kutokuwalipa kabisa. Hali hii huleta hasira kwa dada wa kazi na hali hiyo humfanya kufanya mambo ambayo yapo nje kbs na utaratibu.

4. Uhusiano wa kimapenzi baina ya Baba na dada wa kazi
Ikifika hatua hii dada wa kazi hunogewa na kutamani kuleta ukorofi ili ifike siku abaki yeye na baba ndani ya nyumba, hali hii ujenga tabia ya kutaka kukorofishana na mama lkn kwa sababu ya uimara wa mama ugomvi huamishiwa kwa watoto ambao hawana namna yyt ya kukabiliana na dada.

Hayo ni kwa uchache mdau unaweza changia tujue tatizo ili hatimaye tupate suruhu ya matatizo haya ili basi tupunguze ukatili kwa watoto wetu dhidi ya dada wa kazi....

Karibuni kwenye mjadala
 
Wasichana wengine wana roho mbaya tu. Anaweza asiteswe wala nini akawa na uchawi wake mfukoni.
 
Kina mama ambao ndiyo mabosi wao ndiyo wanasababisha haya,wana lugha mbaya sana juu yao,baba ukiingilia unaambiwa una jambo lako,sasa unakaa kimya ukipata chansi unaongea nae kwa upande ki utu na kuhakikisha nyie na watoto mpo salama.Hachelewi kuwapiga sumu wote.Baba akiwa karibu na beki 3 jua dada atadumu na watoto watakuwa salama.Naomba kuwasilisha
 
ugumu unakuja pale ambapo utaanza kuwa karibu na dada wa kazi, Wamama huwa wawazi mengine zaidi ya kwamba unamnyandua!!
 
Ukatili unaofanywa na wadada wa kazi dhidi ya watoto majumbani unaongezeka siku hadi siku, lkn huenda bila kujua sisi kama wanafamiia tunaweza kuwa chanzo kizuri cha ukatili huu.

Hata hivyo baadhi ya wadadisi wanabainisha kwamba mojawapo ya sababu za ukatili huo ni kama ifuatavyo;

1. Wakuu wa kaya hasa akina mama kukosa upendo kwa wadada wa kazi
Unakuta mama kila anapokuwa nyumbani basi hataki kbs kushuhudia dada akitoa hata tabasamu hata na watoto anaowalea kutwa nzima, kutwa kugombeza, jambo dogo la kumwelekeza basi atagomba na kumtukana matusi tena mbele ya watoto , jambo hili huleta simanzi kwa wadada na hatimaye hugeuka wakatili bila kujua ukatili ule waufanyie kwa nani ndipo baadae hupata mahala pa kurejeshea machungu yao ambako ni kwa watoto wadogo.

2. Mahusiano Mabaya ya wazi baina ya wakuu wakaya-Majibishano na Ugomvi baina ya wakuu wa kaya.
Majibishano ya maneno na ugomvi wa waziwazi baina ya wakuu wa kaya humfanya dada wa kazi kuamini hayo ndiyo aina ya maisha wanayopaswa kuishi wanafamilia hao na hapa waathirika wakubwa huwa ni watoto.

3. Ucheleweshaji wa stahiki au stahiki duni kwa dada wa kazi
Wakuu wengi wa kaya wamekuwa wakiwalipa mishahara midogo wadada wa kazi lkn pia kwa kuchelewa hata zaidi ya miezi 3 au kutokuwalipa kabisa. Hali hii huleta hasira kwa dada wa kazi na hali hiyo humfanya kufanya mambo ambayo yapo nje kbs na utaratibu.

4. Uhusiano wa kimapenzi baina ya Baba na dada wa kazi
Ikifika hatua hii dada wa kazi hunogewa na kutamani kuleta ukorofi ili ifike siku abaki yeye na baba ndani ya nyumba, hali hii ujenga tabia ya kutaka kukorofishana na mama lkn kwa sababu ya uimara wa mama ugomvi huamishiwa kwa watoto ambao hawana namna yyt ya kukabiliana na dada.

Hayo ni kwa uchache mdau unaweza changia tujue tatizo ili hatimaye tupate suruhu ya matatizo haya ili basi tupunguze ukatili kwa watoto wetu dhidi ya dada wa kazi....

Karibuni kwenye mjadala
Hiyo namba 4 huwa ni silaha ya msaada kwa baba kaya. Ndiyo maana akaitwa beki 3 kupandisha na kukaba mashambulizi.
 
Back
Top Bottom