Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Dec 26, 2022
9,473
12,861
Kama mwandishi wa habari huru nilikua nachunguza viini vya migogoro katika maeneo ya ukanda huu wa maziwa makuu.

Nilibahatika kufanya mahojiano ya kina na washirika wa iliyokua serikali ya Rwanda kabla ya kupinduliwa mwaka 1994.

Watu wengi hawawezi kujua kua,karibia majenerali wote wa iliyokua serikali ya Rwanda mwaka 1994 walikimbilia nchi ya Zaire kabla ya baadhi yao kwenda ughaibuni kuishi.

Nilibahatika kufanya nao mahojiano kuhusu kupinduliwa kwao na wanajisikia vipi kupinduliwa na kuishi ukimbizini.

Niliwauliza je wanajihisi vipi na wao kufukuzwa kwa mtutu wa bunduki hadi ukimbizini na wale watu waliokua nao wamekimbizwa ukimbizini kwa mtutu wa bunduki.

Niliwauliza kuhusu mauaji ya kimbari na kikabila dhidi ya watusi wengi na wahutu wachache.

Niliwauliza kuhusu chuki waliyokua wanaipandikiza kama watawala kwa wananchi ili kuleta machafuko.
Niliwauliza kuhusu ukabila baina ya watusi na wahutu na wakati wote wanaongea lugha moja kinyaruanda.
Niliwauliza kuhusu mipango yao baada ya kupinduliwa ipoje.

Niliwauliza kuhusu wanajisikiaje wanapotuhumiwa kama wapangaji wa mauaji ya kimbari dhidi ya binadamu wenzao. Niliwauliza kuhusu vikosi vya wanamgambo makatili na wauaji wa intarehamwe.

Niliwauliza kuhusu mahusiano yao kisiasa na nchi jirani.

Nitakua nawaletea kwa vipengele hayo mahojiano yangu yote na vizazi vya wanajeshi wa iliyokua RAF (Rwanda Armed forces) kabla ya kupinduliwa na RPF forces mnamo mwaka 1994.

Mahojiano yanajumuisha mambo mengi ya kiuchumi na kisiasa na kitamaduni.

Na kuna ukweli ambao watu wengi hawaufahamu na hata kama unafahamika basi watu hawapendi kuuzungumza.

KABLA YA MFULULIZO WA MAHOJIANO YANGU NA WASHIRIKA WA FDLR NITAANZA NA HISTORIA FUPI YA MUHUSIKA MMOJA KAMA ALIVYONIADITHIA.

June 16 saa tatu usiku kwenye eneo la Gatuna au kwa kinyarwanda Katuna mpakani mwa Uganda na Rwanda 1987.

Kulikua na mkutano wa nje ya kambi kwenye upande ule wa mlimani kwenye mji ule wa mpakani.Na mkutano wenyewe ulikua wa makanali wa jeshi na wanajeshi wa vyeo vya chini waliokua wanaifuatilia hali ya wasiwasi mpakani katika mji wa Gatuna upande wa mpaka wa Uganda.

Taarifa za kijasusi za jeshi la Rwanda zilikua zinasema kua,wakimbizi wa kinyarwanda waliokua upande wa nchi ya Uganda walikua wanajiandaa kuivamia nchi ya Rwanda.Taarifa zilisema kua wanyarwnda ambao wamesajiliwa katika jeshi la NRM la Uganda walikua wanaondoka jeshini kwa kasi na kuenda kuunda vikosi vya kijeshi ili kuishambulia Rwanda.

ITAENDELEA!

- Sehemu ya Pili
- Sehemu ya Tatu
 
Nimesoma mpaka ulipoandika,

''Niliwauliza kuhusu mauaji ya kimbari na kikabila dhidi ya watusi wengi na wahutu wachache" nikapata wasiwasi kidogo.

Niliposoma kwenye moja ya komenti yako ukikili kagame ni mjomba wako nikafuta wazo la kuendelea na uzi wako.
 
INAENDELEA..........!!!!

Kanali ""F""anasimulia na kusema kua kwa mara ya kwanza katika maisha yake ndio huo mwaka 1987 ukikua wakati mgumu sana kwake,na kwa mara ya kwanza alipata hofu katika kutekeleza majukumu yake kama mwanajeshi.

Aliambiwa aende Kampala kutekeleza majukumu ya kijasusi ya kujua hivyo vikundi vya waasi vinavyojiandaa kuipindua serikali ya Rwanda ni vikundi vya akina nani.Maana kwa mujibu wa taarifa rasimi kutoka kwa majasusi ndani ya jeshi la Uganda (UPDF) ambalo lilikua chini ya NRM ni kwamba asilimia 46% ya askari wake ni wanyarwanda wenye asili ya kitusi,na mpaka wakuu wa intelejinsia na rasilimali watu ni wanyarwanda wanaoishi nchini Uganda.

Afande "F" anasema alikua na wasiwasi wa kufanya ujasusi Kampala sababu""In Kampala there,s no one to trust""" hata vyanzo vyake vya habari hakua anaviamini asilimia 100%.

Afande""F""aliyekua na cheo cha Kanali anasema kua pale mpakani kwenye mji wa Gatuna mpango kazi wa ulinzi wa mpakani aliokua anausimamia ulikua umekaa vizuri sana.

Anasema ikumbukwe mwaka huo 1987 serikali ya Rwanda kupitia yeye mwenyewe binafsi na washirika wake wa kijeshi waliopo nchi ya Zaire na Msumbiji na Mauritius alifanikiwa kufanya manunuzi ya silaha za kijeshi za logstic mbalimbali na iliigharimu serikali yake kiasi cha dola za kimarekani milioni 19 taslimu.

Pia serikali za Ufaransa na Afrika ya Kusini na Msiri zilikua zimewauzia silaha zilizoigharimu serikali ya Rwanda dola milioni 9 mwaka huo huo.

Kwahiyo mipaka yote ya nchi ya rwanda hasa upande wa Uganda ilikua imepewa kipaumbele cha kupangiwa wanajeshi wenye uzoefu na silaha bora kabisa za kivita mpakani,na kwa hilo hakua na wasiwasi bali wasiwasi wake ulikua ni ongezeko la vurugu za upinzani dhidi ya serikali aliyokua anaitumikia ndani ya rwanda na nje ya Rwanda.

Afande""F""anasema hakua na jinsi ilibidi avuke mpaka na kuingia nchini uganda na kujitambulisha kama raia wa Tanzania huku akitumia passport feki ya Tanzania na jina bandia la Ezekiel Magulio mkazi wa Mwanza na kabila msukuma na ni mfanyabiashara wa samaki katika ukanda wa ziwa Victoria.
Anasema aliamua kutumia passport feki ya kitanzania sababu kwa hali halisi ilivyokua,ilikua rahisi kufanya kazi zake nchini Uganda akiwa kama raia wa Tanzania kuliko akiwa raia wa nchi nyingine.
Anasema kabla ya kuondoka mpakani mjini Gatuna upande wa Rwanda ilibidi afanye mkutano na wanajeshi waliopo chini yake na kuwaachia maelekezo ya namna ya kuendesha ulinzi wa mpakani na kuhakikisha hakuna mtafaruku utakaotokea na kuzua hali ya sintofahamu pale mpakani,wakati yeye atakapokua mjini Kampala.

KOLOLO KAMPALA 1987:
Mshirika wa afande "F""alikua anakaa kwenye nyumba ya kukodisha mitaa ya kololo na alikua ndie mtoa habari ambae kwa kiasi kikubwa angeweza kuaminika kwa afande""F"".

Kulikua na habari zifuatazo kutoka kwake.

MOSI: Ndani ya jeshi la Uganda kulikua na movement iliyoitwa Rwanda patriotic front ambayo iliwashirikisha wanajeshi wa Uganda wenye asili ya kinyarwanda,na lengo kubwa la hii movement ni kwa hawa wanajeshi wa jeshi la uganda wenye asili ya kinyarwanda kuiangusha serikali iliyokua madarakani nchini rwanda kipindi hicho.

Na hizi zilikua taarifa za kuaminika sababu mtoa taarifa kama nilivyosema alikua anaaminika kwa kiasi kikubwa na afande""F"" na alikua ni kapteni usu karika jeshi la Uganda (UPDF) lililokua chini ya serikali ya NRM.

Hizi habari zilimfanya afande""F" aanze kufuatilia kwa umakini hawa wanaharakati viongozi wa movement ya Rwanda patriotic front ni akina nani na wafadhili wao ni watu wa namna gani,na uwezo wao wa kuhatarisha usalama wa mpakani upoje na njia za kuwamaliza nguvu ni zipi?

Akiwa mjini Kampala kama mfanyabiashara wa kitanzania na makazi yake yakiwa maeneo ya kololo na akiwa anavaa mawigi ya ndevu bandia,basi afande""F""anasema alianza upelelelzi wake mara moja wa kuwabaini hawa watu na kutoa ripoti kwenye makao makuu ya kikosi chake cha kazi mjini Chigali (Kigali) baada ya kupewa taarifa hizi na chanzo chake cha habari mjini kampala.

PILI: Kulikua na habari pia kuhusu mpango wa serikali ya uganda kutaka kuwarudisha kwa nguvu mamia ya maelfu ya wanyarwanda waliokua uhamishoni nchini uganda na hasa wale waliokua jeshini na wale waliokua na mafunzo ya kijeshi maana walionekana kama tishio ndani ya serikali ya Uganda.Na afande""F"" alikua lazima azifuatilie na kuthibitisha habari hizi pia baada ya kupewa na chanzo chake cha habari

PAULO JACOB KAGAME NA TWEGEZE MOVEMENT 1987 KAMPALA UGANDA:
Huyu ndio mtu pekee aliyekua anafahamu ujio wa afande""F""ndani ya kampala na alifanikiwa mara tatu kuonana nae na kuzungumza kuhusu ujio wake na ujasusi wake dhidi ya wanaharakati wa rwanda patriotic front waliokua kwa kipindi hicho wanajikusanya kuanzisha movement yao ya kijeshi ili kupambana na serikali ya Rwanda.Japo ilikua siri mno mwaka huo na ni watu wachache sana waliokua wanaifahamu hii movement katika mwaka huo 1987.

Paulo Jacob Kagame alikua nani na alihusika vipi na muingiliano wa shughuli za afande""F"" mjini kampala?

Huyu Paulo Jacob Kagame yeye alijulikana kama code namba 17 na alikua double agent wa serikali zote tatu za Uganda na Rwanda na Zaire katika ukanda ule wa maziwa makuu.Na alikua mtaalamu wa saikolojia kama taaluma ila pia alikua muasisi wa movement inayoitwa TWEGEZE mwaka huo wa 1987 iliyoasisiwa mjini Nairobi Kenya na wanyarwanda waliokua wanaishi uhamishoni mjini Nairobi.

Pia alikua mshirika wa ubalozi mdogo wa Israel mjini nairobi,na alikua mfanyabiashara wa madini tajiri ila asiyekua na jina kwa sababu za kiusalama.Tutamzungumzia huyu Paulo Jacob Kagame huko mbele,kwa sasa tuachane nae kwa mda.

AFANDE ""F"" MJINI KAMPALA 1987
Kwanini afande""F"" alikua ameonana mara tatu na code 17?
Ni kwa sababu ili mpango wake wa kupata taarifa ufanikiwe lazima awe na double agent wa kufanya nae kazi kwa makubaliano ya kila upande kufaidika kwa pasu kwa pasu.Hizo mara zote tatu wakizokutana ndizo zilizompa afande""F""habari za uhakika kua ipo siku huko mbeleni kutakua na machafuko nchini rwanda na ikumbukwe hiyo ilikua ni mwaka 1987 mwezi July.

Code 17 alimuhakikishia kua hii movement ipo na tayari imeshasogeza vikosi ambavyo vimevaa kama wanajeshi wa uganda, mpakani mwa uganda na rwanda na kusubiria siku ya kuanza mapambano ya kuivamia Rwanda na ni bora arudi Kigali na kutoa taarifa kwa komandi kuu ili wajiandae na vita itakayokuja siku za mbeleni na hilo halikwepeki.Lakini afande""F""anasema kua mshirika wake huyo CODE 17 alimficha kuhusu mpango na harakati za TWEGEZE na hilo alikuja kujua baadae sana wakati yupo ukimbizini mjini Bukavu nchini Zaire.

Afande""F"" anadai kua baada ya kukaa mjini kampala kwa mda wa miezi mitatu basi ilimlazimu kurudi mjini Kigali (Chigali) na kuwasilisha ripoti yake mbele ya kamandi kuu ya kijeshi na kuwaeleza hali halisi ya mambo yalivyokua huo mwaka 1987 na hali ya hatari inayoweza kujitokeza huko mbeleni katika usalama wa nchi ya Rwanda.

Afande"""F""anakili kua moja ya udhaifu wa jeshi la rwanda la wakati huo ni kuruhusu siasa za kikabila kuingia mpaka jeshini na kutengeneza matabaka kwa wanajeshi na raia. Na anakili kua toka nchi ya Rwanda inapata uhuru ni kwamba siasa za kikabila ziliharibu mfumo mzima wa utawala.

Ndio maana anasema hata maoendekezo yake aliyoyawakikisha katika komandi kuu ya kijeshi anasikitika hayakufanyiwa kazi kwa sababu ya ukabila na siasa za chuki na uroho wa madaraka baina ya majenerali na wakuu wa vikosi ndani ya jeshi la Rwanda.

Vilevile anasema wanasiasa wa vyama vya upinzani na chama tawala walikua na mitazamo kinzani kuhusu namna bora ya kumaliza ugonjwa sugu wa "UKABILA" ndani ya nchi ya Rwanda.

Na hiyo ilichangia pia kwa kiasi kikubwa machafuko yaliyofuatia miaka ya mbele.

ITAENDELEA!
 
Back
Top Bottom