johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 91,133
- 158,446
Hii nimeona ni kali zaidi yaani Ruto amebanwa hadi amefuta Bajeti ya Ofisi ya Mke wa Rais
Kwa sasa Gen Z ndio wanatengeneza Sera za Nchi yao, Wazee wamepumzishwa.
---
Rais wa Kenya, William Ruto ameondoa bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ofisi ya Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Kiongozi na amefuta Mashirika 47 ya Serikali na kusitisha safari zisizo za lazima kwa Wafanyakazi wa Serikali pamoja na kuzuia ununuzi wa magari mapya ya Serikali.
Akihutubia Taifa la Kenya leo July 05,2024 Ruto ametangaza kupunguza idadi ya Washauri wake kwa 50% ambapo ameanzisha hatua nyingine kadhaa za kubana matumizi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inaingia na pia amekata bajeti za ukarabati wa majengo ya Serikali kwa 50%.
Ruto pia amesema hakuna Afisa wa Serikali atakayeruhusiwa kushiriki katika shughuli za kuchangisha pesa zinazoendelea na amewaagiza Maafisa wa Serikali kuacha shughuli za hisani, hasa walioonekana wakionyesha pesa nyingi wakati wa hafla za kutoa misaada ambayo imezua taharuki kutoka kwa Wakenya.
Ruto amesema kufuatia mashauriano mapana na wenzake wameafikiana kupunguza gharama mbalimbali zikiwemo kufuta angalau Mashirika 47 ya Serikali yenye vipengele vinavyoingiliana lengo likiwa ni kuboresha huduma za Serikali kwa Wananchi na kuwafanya Wakenya wapate huduma sahihi kutoka Serikalini.
PIA SOMA
- Rais Ruto kushiriki mjadala na Wakenya kwenye X Space, Julai 5 kwa saa tatu