Mahojiano na Kafulila yafutwa Clouds TV

Mahojiano na Kafulila yafutwa Clouds TV

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
1,885
Reaction score
4,013
Anaandika Davidi Kafulila

Kipindi clouds360 nilichoalikwa leo kuanzia saa mbili unusu asubuhi kwajili ya kujadili masuala yanayoendelea nchini kama nilivokuwa nimewajulisha jana ambacho kilikuwa kikitangazwa tangu jana kimefutwa nikiwa studio tayari kwa maelekezo toka juu!


Poleni mliokuwa mkisubiri kunifuatilia!

David Kafulila.

YALIYOMKUTA David Kafulila, katika Studio za Kituo cha Utangazaji cha Televisheni ya Clouds, hatokisafau maishani mwake.

Ni kwa kuwa, alialikwa kuzungumzia masuala ya uchumi na baada ya kufika, aliandaliwa kama wageni wangine wanavyoandaliwa lakini ghafla wakamtosa.

Kafulila aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (2010-2015) amesema “sintoisahau siku hii.” Amesema alialikwa na chombo hicho cha habari kuzungumzia mwenendo wa uchumi nchini.

Ni kutokana na historia yake alipokuwa mbunge kwamba, alikuwa kinara kwenye Bunge la 10 baada ya kuibua ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh. Bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Hata hivyo Kafulila akiwa tayari ametayarishwa kwa kuvalishwa kipazasauti ili kuanza mjadala katika kipindi cha 360, ghafla aliombwa radhi kwamba “kuna maelekezo kutoka kwa mkurugenzi kuwa, kipindi kisirushwe.”

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo baada ya kuondolewa katika studio za kituo hicho amesema “binafsi sikutarajia siku moja kukutwa na hali hii.

“Sikujua kama siku moja Tanzania itafika hatua hii. Nilijisikia vibaya kuvuliwa mice nikiwa tayari kwa mjadala lakini nilijua tatizo ni zaidi ya watangazaji.

“Nilitaka kuzungumzia kwa mapana anguko la sekta ya fedha na sekta binafsi na mazingira ya biashara na uwekezaji kwa ujumla na namna athari yake inavojitokeza kwenye kupunguza uwezo wa serikali kutoa huduma kama elimu, afya kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.”

Aidha, Kafulila amesema anadhani kulikuwa na maelekezo ya ziada nje ya mfumo wa kituo hicho kwa sababu, haamini kama tangazo ambalo lilirushwa jana kutwa nzima pia leo asubuhi bila mkurugenzi kufahamu.

Na kwamba, hata kama angejua bado vipindi ni suala la wataalamu wa utangazaji.
“Sijui mmiliki alihofu nini kwangu. Hali ya uhuru wa vyombo hivi ni tete na kwa sheria ya habari inayokwenda kupitishwa bunge lijalo, vyombo vyote vitakuwa chini ya ulinzi wa dola na ndio mwisho wa uhuru wa vyombo hivi,” amesisitiza Kafulila.
 
Yaani upo studio kipindi kinafutwa, woga wote wa nini Na unatoka wapi.!
 
Haya ni maelezo yake mwenyewe
Kipindi clouds360 nilichoalikwa leo kuanzia sambili unusu asbh kwajili ya kujadili masuala yanayoendelea nchini kama nilivokuwa nimewajulisha jana ambacho kilikuwa kikitangazwa tangu jana kimefutwa nikiwa studio tayar kwa maelekezo toka juu! Poleni mliokuwa mkisubiri kunifuatilia!. *David Kafulila*
 
Haya ni maelezo yake mwenyewe
Kipindi clouds360 nilichoalikwa leo kuanzia sambili unusu asbh kwajili ya kujadili masuala yanayoendelea nchini kama nilivokuwa nimewajulisha jana ambacho kilikuwa kikitangazwa tangu jana kimefutwa nikiwa studio tayar kwa maelekezo toka juu! Poleni mliokuwa mkisubiri kunifuatilia!. *David Kafulila*

Kwani Kafulila ana wadhifa gani kisiasa?
 
kuna kipindi clouds radio pia walianza mahojiano.na wanasiasa kama mtatiro,hashim rungwe ambaye.kupitia mahojiano hayo alifungua sana akili za watu.

lakini ghafla nayo yakafutwa,hasa baada ya misumari ya moto ya hashim rungwe
 
kama upinzani ulianza kabla na enzi za redio tanzania,gazeti la mzalendo na uhuru ambayo hakika hayakuwapa fursa kuelezea fikra zao,but still,wali hold on mpaka wakatambulika rasmi.

ni wazi kwamba ukizuia vyombo vya habari visiwape nafasi wapinzani ndio kama unakoleza moto wa upinzani

kipindi cha redio tanzania,wasapu,fesibuku,twita hazikuwepo
 
Hii serikali inaogopa hata kivuli chake.Atukuchagua Tembo atuongoze tulichagua raisi by Butiku
tembo akiingiliwa na siafu au sisimizi kwenye.mkonga wake, ataupigapiga kwenye miti mno,ataupiga mno,na anaweza kusababisha hata kifo chake.
bandari,wafanyabiashara,warumishi,TRA......

mpaka sasa uchumi umejifia
 
Back
Top Bottom