Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Kesho siku ya Jumapili kuanzia majira ya saa saba za mchana (EST) sawa na saa tatu za usiku (Saa za Afrika ya Mashariki) tunatarajia kuwa na mahojiano na Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kampuni ya Richmond. Ni matokeo ya Kamati hiyo ndiyo yaliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa kujiuzulu na hatimaye Baraza la Mawaziri kuvunjika.
Tutazungumza na Dr. Mwakyembe karibu mwaka mmoja kamili tangu matukio yale ya Februari 2008, matukio ambayo yalikuwa ni ya kihistoria. Tutazungumza naye pia mambo mengine ya kitaifa saa na wakati huu ambapo Taifa letu linapitia katika mabadiliko makubwa ya kifikra ambayo tumeyaasisi na kuyaongoza kwa umahiri mkubwa.
Utaweza kusikiliza mahojiano yetu kupitia KLHN kwenye MWANAKIJIJI.COM "live".
Wakati unasubiri, BONYEZA HAPA KUSIKILIZA MUZIKI
Last edited by a moderator: