Mahojiano na Dr. Harrison Mwakyembe

Majibu aliyoyatoa Mh. Dr. Mwakyembe, mbunge wa Kyela katika mahojiano yake na Mwanakijiji yamenifanya niamini 100% kuwa usanii ndani ya CCM na serikali umekomaa na unaambukiza. Kwamba kuna wapiganaji ndani ya CCM wanaoweza kuleta mabadiliko itabakia ndoto kama alivyodhihirisha Dr.

1. Huyu ndiye Dr. anayemtetea Mkapa na kumsifu kwa utendaji mzuri na kuwaomba watanzania waache kumhusisha na ufisadi.

2. Huyu ndiye kama mwenyekiti wa tume ya Richmond, kwa makusudi aliificha bunge sehemu ya ripoti kwa kuhofia kuiumbua serikali.

3. Huyu anatamka hadharani kuwa ukitaka maisha mazuri na wananchi wazidi kukusikiliza ubaki CCM - hata kama inanuka ufisadi.

4. Huyu huyu anamtetea Waziri Mkuu kwa matamshi ya hatari kwa kisingizio kuwa Pinda kama mwanasheria hawezi kutamka maneno kama hayo - labda waandishi wanafunzi ndio walichemka.

Haya ni baadhi tu ya mengi yanayonifanya nichukue kwa tahadhari kubwa yale yote yanayotamkwa na wale wanaoitwa eti wapiganaji ndani ya CCM. Asante MKJJ kwa kunifungua macho - huwezi kujifunika hilo hilo shuka lililo na wachafu halafu useme u msafi.

Mag3,
napata taabu sana kuwaamini Watanzania kama hata kwenye kitu dhahiri kama hiki tunaweka chumvi! Nimeisikiliza mara tatu interview ya Dk. Mwakyembe na Mwanakijiji, sijaona akimtetea Mkapa na kusema ati "Watanzania waache kumhusisha na ufisadi"; sijamsikia Mwakyembe akisema kubaki CCM ni neema ila kasema "watu wenye kuweza kutoa kauli hiyo ni wale walioingia kwenye siasa kuganga njaa. Amesema yeye anajivunia kisomo chake". Hoja ya kwamba alilificha Bunge sehemu ya taarifa ya Richmond haina maana kwa kuwa Mwakyembe alikuwa mwenyekiti wa kamati, hakuwa yeye kamati. Afterall alijieleza kuwa hayo waliyoyaweka pembeni wangeyatoa kama Lowassa ange"resist" kujiuzulu. Mbona aliposema watengue kanuni ili wamwage upupu bungeni, kila mtu alishika adabu? Halafu Mag3 unamlaumu!

Mwakyembe kajieleza kisheria kwa nini anamtetea Pinda. Na wewe Mag3, jenga hoja usilaumu tu! Sasa naamini wengine mnatumia mwanya huu kumaliza hasira zenu kwa niaba ya Lowassa na Rostam. Dk.Mwakyembe usikatishwe tamaa, songa mbele nna mapambano ndani ya CCM. Kutoka CCM ni uoga, ni kuwakimbia akina Makamba na mafisadi wengine. Kajieleza vizuri sana kuwa yeye ni mjumbe wa NEC, ni kiongozi wa juu wa CCM, hawezi kukihama chama chake, atapambana ndani kwa ndani. Mimi namwambia Dk. Mwakyembe aendeleze mshikamano wao ndani ya Bunge (Kilango, Sendeka, Kimaro, Zambi, Selelii, Manyanya) mpaka kieleweke!
 
Mkuu Fataki,
pamoja na kwamba jina lako lina kasheshe, naheshimu hoja zako nzito. Tuna tatizo Watz kutoa hukumu za papo kwa papo bila uchambuzi kama wako. Umenifanya na mimi niingie kwenye mtandao kutafuta interview hiyo. Namfahamu Dk. Mwakyembe miaka mingi, kafanya mengi (kama kujiuzulu udirector wa NBC on a question of principle), mambo ambayo wengi wetu hatuwezi hata kudiriki. Watu tuliopitia NBC tunamjua Mwakyembe kuwa jasiri, mpenda haki na ukweli. Kijikomba si dini yake. Nitajimwaga baadaye, baada ya kuisikia interview hiyo!
 
Back
Top Bottom