Mahojiano na aliyenusurika katika shambulio lililoua askari wanne

Hivi hii kuonyesha video sura ya mtu aliyeshuhudia tukio au kupambana na majambazi haiwezi kuhatarisha usalama wa muhusika?Maana ninavyoamini ni kwamba wahalifu wengine tunaishi nao mitaani,sasa kwa hali hii si anaweza akafuatiliwa na "mtandao"wa uhalifu wakiamini kwamba wameonwa na taarifa zao zikapatikana?

Mimi siku nikipambana na majambazi nikafanikiwa kuwanyang'anya silaha na kuwakamata,sitaki mje na mikamera yenu kunimulika.Sipendi unaa!
 
Yani baadhi ya watu humu wamekosa utu kabisa.Inakuwaje mtu unafurahia tukio la mauaji Kama hili?? Vipi Kama aliyekufa angekuwa anahusiana na wewe kwa namna moja au nyingine? Hebu jivishe sura na mioyo ya hawa wafiwa japo kwa dakika moja halafu uone namna utakavyo feel.Hawa ndugu zetu wametangulia mbele za haki wameacha wake,watoto na ndugu waliokuwa wanawategemea tusikose utu kiasi cha kufurahia yaliyowatokea. Leo kwao kesho kwetu hatujui kesho yetu ni vema tukatenda mema.
Hizo silaha zilizoibiwa hatujui itakuwaje kesho inaweza ikatumika kwako au kwa jamaa zako.
Tujifunze kuwa na mioyo iliyojaa hofu ya Mungu.
Wapumzike kwa amani.
Sidhani kama kuna mtu amefurahishwa nahili tukio. Kinachoonekana watu wana maduku duku mioyoni mwao juu yautendaji wa jeshi la Polisi. Kwahiyo nimuda muafaka nadhani kwa jeshi letu kujitathmini upya utendaji wake dhidi ya raia, ili matukio yakusikitisha kama haya yanapotokea wapate sapoti ya raia wengi kama sio wote. Kwa comments ninazoziona humu nikwamba hali yamahusiano kati yajeshi letu la Polisi na raia sio nzuri. Ukitaka kupata ukweli huu angalia idadi ya comments zakusikitika moja kwamoja nichache mno ukilinganisha na zenye angalizo. Kwahiyo nadhani kuna kila sababu kwa jeshi letu kujitathimini upya.
 
Hivi huko walikovunja na kuiba silaha, hakukuwepo na ugumu wowote wa kuzifikia hizo silaha, maana naona story ambayo ime make headlines ni hiyo ya mauaji tu, wiki wa silaha hujaelezwa kwa kina... Na kwann inakua rahisi hivyo kuvunja kituo na kuiba silaha? Na kama ni rahisi kiasi hiki, majambazi watafanya wanavyotaka ktk nchi hii,.. Ni maamuzi yao leo waende wapi wakachukue wafanyie tukio... Kesho JESHI LA police linaita vyombo vya habari vikijinadi wamekamata jambazi likiwa na silaha,.. Silaha zitarudishwa kituon mda utakapofika wa jambazi kuiihitaji tena ataenda kuichukua kituoni! Hovyooo kabisa.
 
unajua mwigulu fanya kazi hasa hili ttzo laizma likabiliwe naskia mmefuta polisi jamii sasa hatari ndio hii mnaona mambo ya kuvaa uniform na kujijenga kisiasa magufuli haangalii
 
Hizo mbwembwe wanazoonyesha mitaani kututisha kumbe wao wenyewe hawana uwezo wa kujilinda!
Unafahamu wamekulinda na kujilinda mara ngapi kabla ya hili shambulio la kushtukiza?

Kwa kukusaidia zaidi, hakuna jeshi linalokwenda vitani na kurudi bila kupoteza wapiganaji wake.

Kumbuka polisi kila siku wako vitani.
 
Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo
huna akili..... mikutano ya vyama vya siasa inatangazwa lakin hujawah sikia majambaz wanatangaza enda vamia eneo husik..nchi inazid kuwa maskin kwa uwepo wa watu kama wewe
 
Police wetu ni dhaifu sana nakumbuka sitaki shari ukonga anyway pumzikeni kwa amani makamanda wa CCM
 
Well said mkuu. Linapokuja suala la maisha/uhai ni kitu kisichohitaji masihara wala kejeli! Na ni kweli pia hiyo silaha kesho yaweza kukudhuru wewe au kama sio wewe ni ndugu jamaa au mtanzania mwingine yeyote ambae ni nguvu kazi!
polisi wana udhi sana,wanabambikia kesi watu ovyo ovyo halafu walimuua mwangosi.hukumu ni hapa hapa duniani
 
Yani wananchi 56 wameuwawa Kagera mpaka sasa wako kimya afu polic 4 matamko kama mnashindana mnataka ushilikiano gani na wananchi naona la police limewauma sana kuliko wananchi
 
Nadhani mtazamo wa 'mazoezi' ya jeshi la Polisi sasa ubadilike, badala ya kufanya mazoezi ya kudhibiti raia wasio na silaha wakiandamana, wafocus kufanya mazoezi ya kukabili majambazi wenye silaha!
 
Dah poleni sana familia ya askari wetu waliopoteza maisha na polen sana jeshi la polisi mungu awape nguvu msikatishwe tamaa na matukio km aya hii ni bahati mbaya sana kwenu,ila cc wananchi tunawaamini na tupo pamoja ktk kufichua wale wote wasiotakia mema taifa letu
 
Kwanza niwape pole sana Polisi na familia za askari waliouawa. Pili polisi lazima wafahamu kuwa kuna tatizo sana la askari kulinda usalama wa raia, walijisahau sana ikafika mahali mpaka majambazi yakaona uwezekano wa kupambana na polisi. Naweza kusema wamewalea sana wezi na majambazi. Sikuwa nafahamu kama jeshi la polisi lina vyombo imara na madhubuti vya kulinda usalama wa raia, hizi siku mbili wametuonesha wanazo nguvu, sasa nachoshindwa kuelewa inakuwaje majambazi yatende haya yote na hata kujiaminisha kwenda kwenye makao ya polisi (ref staki shari incident) na kufanya ualifu? Mh Mwiguli naamini Uwezo unao wa kubadili hii dhana ya majambazi kwenye ardhi ya Tanzania. Kuweni makini na achene masihara na wezi na majambazi, ifike mahali kila mtu anayeona alternative ya maisha ni kuiba aogope. Nchi zingine mbona zimeweza? wakikukamata tu ndio mwisho wako. Lkn sisi tumezoea kuona majambazi yanapelekwa polisi na kurudi, kufanya masihala na waalifu sio jambo jema.

hata ukiwa na utaalama vip mtu akikuvizia lazima akudhuru kwa kuwa atakuwa amejiandaa vya KUTOSHA,bila wew kujua na watu wanambinu nyingi na hata marekeni sep 11, ilivyamiwa kwa kuwa watu walikuwa wamaejianda bila wao kujua , na weo pia walikuwa wazemabe
 
Kila mtaa na mjumbe wa nyumba kumi kura zakutaja majambazi na waharifu zianze zoezi lisimamiwe na police wakiongozwa na waziri wa mambo ya ndani. Pangenoga Mrema angepewa uwaziri wa mambo ya ndani
 
Unafahamu wamekulinda na kujilinda mara ngapi kabla ya hili shambulio la kushtukiza?

Kwa kukusaidia zaidi, hakuna jeshi linalokwenda vitani na kurudi bila kupoteza wapiganaji wake.

Kumbuka polisi kila siku wako vitani.
Vita ipi zaidi ya kushiriki ujalnazi na rushwa
 
Nisiongelee tukio lenyewe, bali zoezi la usajili wa silaha.
Hivi unaamini kwamba wahalifu au wale wanaomiliki silaha kinyume na taratibu walisalimisha silaha zao kweli? Yaani jambazi asalimishe silaha yake asiyomiliki kihalali halafu kesho yake akavamie lindo au kituo cha polisi ili apore silaha nyingine? Waliosajili ni wale wenye nia njema tu.

Kifupi bado polisi, kama yalivyo maeneo mengine ya utendaji nchini wanahitaji kujipanga upya.

Kuhusu kejeli zinazotokeza, nadhani polisi, serikali na wapenzi wa CCM wamezitaka wenyewe. Hii ni kwa sababu jeshi la polisi limejipambanua kama lipo maalum kukandamiza wapinzani badala ya kuwa neutral. Haiwezekani raia wanapanga kuandamana bila hata fimbo wala jiwe lakini karibia mwezi sasa tunaona polisi wanafanya mazoezi ya vitisho mitaani na kutishia kuvunja miguu na hata kuua watu. Huu uhasama wameutaka wenyewe. Na linatakiwa liwe fundisho kwa kila mtu. Usitegemee huruma pale yanapokukuta wakati wewe huna huruma unapokuwa na maamuzi na nguvu. Yaani ubinadamu kwao ni vitisho vya bunduki nzito na mabomu mitaani? Polisi wanakabilije waandamanaji kwa nguvu namna hiyo badala ya kuwalinda ili wafike salama huko waendako ikiwa ni pamoja na kuzuia wale kenge kwenye msafara wa mamba, ambao watataka kutumia mwanya huo kusumbua raia na mali zao?

Polisi wajichunguze
CCM wajichunguze
Serikali ijichunguze
Watanzania wajichunguze
Mimi pia sitaingia kwenye mambo ya siasa maana yako kikatiba zaidi yaani polisi wanalundikwa lawama kutokana na makosa yaliyoko kwenye katiba.Jeshi la polisi linawajibika na linamtii Amiri Jeshi wake ambaye 1. Ndio Rais 2. Ndio mwenyekiti wa chama kimojawapo cha siasa 3. Ndio mteuzi wa watu wote muhimu.
Kwa hiyo utaona hakuna uwezekano wa polisi kukiuka maelekezo kutoka kwenye chombo kilichoiunda.

Kuhusu uhakiki wa silaha. Kwani hujui kuwa baadhi ya majambazi walikuwa wakitumia silaha zinazomilikiwa kihalali kufanyia matukio? Wamiliki wa silaha walikuwa wanazikodi kwa majambazi kwa dau zuri tu wakijua kuwa rekodi kuhusu silaha zao ama hazipo au si sahihi. So zoezi la uhakiki limepunguza kwa kiasi fulani hayo mambo ya kukodishana hivyo kuna njaa ya silaha mtaani.
 
Back
Top Bottom