Mahojiano na aliyenusurika katika shambulio lililoua askari wanne

Ninavyodhani ilitakiwa tusikitike sana kwa hili tukio na kulaani kwa nguvu zote ikiwa wenye siraha nzito wanauawa. je wasio na siraha nzito na mafunzo inakuaje? na pia hao waliokufa ni ndugu zetu kazi tuu ndio zimetutofautisha ila si vyema kuwakejeli tunazungumzia uhai wa watu wanne hapo...
 
Yani baadhi ya watu humu wamekosa utu kabisa.Inakuwaje mtu unafurahia tukio la mauaji Kama hili?? Vipi Kama aliyekufa angekuwa anahusiana na wewe kwa namna moja au nyingine? Hebu jivishe sura na mioyo ya hawa wafiwa japo kwa dakika moja halafu uone namna utakavyo feel.Hawa ndugu zetu wametangulia mbele za haki wameacha wake,watoto na ndugu waliokuwa wanawategemea tusikose utu kiasi cha kufurahia yaliyowatokea. Leo kwao kesho kwetu hatujui kesho yetu ni vema tukatenda mema.
Hizo silaha zilizoibiwa hatujui itakuwaje kesho inaweza ikatumika kwako au kwa jamaa zako.
Tujifunze kuwa na mioyo iliyojaa hofu ya Mungu.
Wapumzike kwa amani.
 
wapumzike mahala pema lakini inabidi jeshi letu sanaa lizidishe ushirikiano na raia
 
Yani baadhi ya watu humu wamekosa utu kabisa.Inakuwaje mtu unafurahia tukio la mauaji Kama hili?? Vipi Kama aliyekufa angekuwa anahusiana na wewe kwa namna moja au nyingine? Hebu jivishe sura na mioyo ya hawa wafiwa japo kwa dakika moja halafu uone namna utakavyo feel.Hawa ndugu zetu wametangulia mbele za haki wameacha wake,watoto na ndugu waliokuwa wanawategemea tusikose utu kiasi cha kufurahia yaliyowatokea. Leo kwao kesho kwetu hatujui kesho yetu ni vema tukatenda mema.
Hizo silaha zilizoibiwa hatujui itakuwaje kesho inaweza ikatumika kwako au kwa jamaa zako.
Tujifunze kuwa na mioyo iliyojaa hofu ya Mungu.
Wapumzike kwa amani.
Usishangae!!.......watu wamepoteza ubinadamu kabisa mkuu.
 
Tukio linasikitisha kweli, Mungu azilaze roho za waliofariki mahali pema!
Lakini nao polisi wafanye kazi zao kwa weledi, wakati wa maandamano imekuwa ni desturi polisi kuwapiga raia wasio kuwa na hatia na wasio na silaha, hii hali imechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kujenga chuki dhidi yao!
Polisi waache kutumika kisiasa, tabia ya kuwakamata, kuwapiga na hata kuuwa watu wanaofanya yao kwa mujibu wa katiba ni fedheha na kukosekana kwa weledi!
Wamekuckia mkuu!..washajifunza tayari.
 
Wapumzike kwa amani vijana wetu. Wameacha ndugu jamaa na familia zinazowapenda na kuwategemea sana
Kuna ongezeko kubwa la uhalifu siku za karibuni, lakini askari wetu wako kwenye mazoezi mazito tena yanayoonekana live mitaani (kitu ambacho nadhani sio sahihi)kuonyesha utayari na umahiri wao (wa kupambana na upinzani? Nisihukumu)
Jeshi la polisi linapaswa kujitambua na kujitafakari, askari wengi vijana ndio wameanza kazi jeshi la polisi, bado hawajawa na uzoefu kazini...mbaya zaidi wamekutana na adha ya mazoezi yenye kutesa na kuchosha mno...kwa ajili ya show off za ubabe usio na maana yoyote
Wanachoka mno ila hawana pa kusemea... wana changamoto za maisha ni binadamu wanahitaji kupumzika lakini wakubwa hawajui hilo
Wengi siku hizi utawakuta kwenye vituo vya polisi kwenye mageti ukiwaangalia unasoma kabisa sura za uchovu na kukata tamaa
Wana kazi zenye kukera kuhoji wanaoingia kituoni, kuwapigia salute wakubwa wote kila dakika wanapopita hapo, kutumwatumwa kila wakati kama wasichana wa kazi
Wahurumieni hawa vijana sisi tunaoongea nao tunajua wanachoka mno . wanafanya kazi kwa shift muda wa kuwa off Wapumzike wanatakiwa kwenye gwaride
Kwa jinsi hii hata wakivamiwa ni ngumu kujibu mashambulizi

Umenena vyema kaka, jeshi la polisi linajivunia karibu vijana wapya 90,000 walioingia jeshini ndani ya miaka miwili iliyopita. Bado kuna malalmiko ingizo jipya walioingia kazini june mwaka huu bado hawajapata mishahara yao ya miezi miwili achilia mbali posho za kujikimu. sasa unafikiri watakua na uzalendo? je mazoezi watayokua wanafanya yataingia? vipi kuhusu utimamu wao kimwili na kiakili na utayari wao dhidi ya kupambana na matukio ya kihalifu?

MBAGALA inabidi patangazwe kama kanda maalum kipolisi ni eneo lilokua kwa kasi miaka 10 ilopita, idadi ya watu inasma dhahiri shahiri kua panahitaji si tu vituo vy apolisi vya nyongeza basi iwe kanda maalum inayojiratibu yenyewe. mfululizo wa matukio ya kihalifu pia unaonesha hili.
 
Yani baadhi ya watu humu wamekosa utu kabisa.Inakuwaje mtu unafurahia tukio la mauaji Kama hili?? Vipi Kama aliyekufa angekuwa anahusiana na wewe kwa namna moja au nyingine? Hebu jivishe sura na mioyo ya hawa wafiwa japo kwa dakika moja halafu uone namna utakavyo feel.Hawa ndugu zetu wametangulia mbele za haki wameacha wake,watoto na ndugu waliokuwa wanawategemea tusikose utu kiasi cha kufurahia yaliyowatokea. Leo kwao kesho kwetu hatujui kesho yetu ni vema tukatenda mema.
Hizo silaha zilizoibiwa hatujui itakuwaje kesho inaweza ikatumika kwako au kwa jamaa zako.
Tujifunze kuwa na mioyo iliyojaa hofu ya Mungu.
Wapumzike kwa amani.
Mkuu!..police wenyew ndio wanafanya chuki iwepo.cku hizi police na raia na maadui.wajirekebishe
 
Police nao waache kutumika vibaya na wanasiasa...Haiwezekani inteligensia za Police ziwe zinaona mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu lakini ujambazi haiuoni ...Iwe fundisho kwao wafanye kazi za kupambana na ujambazi sio kupambana na raia wasiokuwa hata na fimbo
Kwani hao waliokuja kupora bunduki ni wanasiasa?! Hebu tumia akili yako hata kidogo basi sio kila jambo unaleta mihemko ya kisiasa tu, bunduki hizo huenda zikakufuata hata wewe.
 
sijaiba sijaua so sijamkosea Mungu na nakifahamu pia maaskari hawa wanaotumika na wanasiasa kila siku kupiga na kutia huku wengine wanashangilia kuona watz kapigwa

Leo kwa kua ni askari eeehhh!!basi mka mkijua huku mitaani tumechoka na udhalimu wanaofanya maaskari wenu wa kila aina,kuanzia rushwa na kusingiziwa kesi kibao!
Tena hakuna kituo chenye rushwa na udhalimu kama kizuiani mbagala almaarufu'maturubai'

Wananchi wamechoka wamechoka wamechokaaaaa!!!
Mkuu umenena vema, hoja yako ni ya msingi pia issue yangu ni kwamba hata hao wanaoshangilia Askari wakinyanyasa raia ni wapuuzi sana tena wakukemea isiwe ivo. Heshima na utu wetu waafrika ni kuwa kitu kimoja inapotekea msiba bila kujali itikadi wala kuweka siasa. Tuwape pole ndugu na wafiwa na kuombea mengine yarikebishwe kwa weledi. Nadhani ndo jambo sahihi kwa wakati utokeapo msiba.
 
Siku zote tunajifunza kutokana na makosa.
Ni wakati wa jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa weledi bila kuonekana kutumika na upande fulani dhidi ya upande mwingine.
Mazoezi ya hadharani ya siku mbili zilizopita yameonesha dhahiri jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kupambana na upinzani. Hali hii inaleta uhasama kati ya polisi na upinzani ambao sio wachache kwa mujibu wa uchaguzi uliopita.

Kwa sasa ni vigumu mno kwa raia mwema kuweza kusaidia jeshi la polisi kwa sababu ni kama wameshatengeneza uhasama wa kudumu kutokana na kauli tata za viongozi zinazowasisitiza wananchi kuwaogopa polisi.
RIP polisi wetu. Mmetutangulia hata kabla ya 1 sept.
Sawa, wasisaidie, lakini impact ya bunduki zilizoibiwa mwisho wa siku itarudi kwa raia pia.
 
Ni tukio mbaya kutokea lakini kwann wanatumia nguvu nyingi kujiandaa na oparetion ukuta wakati hao wanaenda kuwazuia hawana hata marungu. Askari wetu jiandaeni kwa kukabiliana na matukio kama hayo, siyo kupita mitaani kutisha wanainchi
 
kwani nimetukana hapo,kila mtu ana haki ya kuandika kile anachoona yeye,,polisi wanajiona wao wako smart sana,na kujiandaa kupiga watu sep 1,bila sababu ya msingi,wanaacha kulinda nchi dhidi ya majambazi,haujiulizi majambazi gani wanakwenda kuiba benki usiku?hao ni wauwaji wanawajaribu polisi,ni kama kule sitaki shari,ilivyotokea,
 
Mkuu!..police wenyew ndio wanafanya chuki iwepo.cku hizi police na raia na maadui.wajirekebishe
Mkuu hata Kama kwa tukio Kama hili anayeweza kulifurahia lazima atakuwa na mapungufu.Watu wanaingiza siasa kwenye matukio yasiyo hitaji siasa Kama hili. Kifo siyo kitu cha kufurahia hata kidogo.
Mkuu vipi hizo silaha walizopora hao majambazi umeshajiuliza kuwa zinaweza kuleta madhara kwa nani?? May be kesho au kesho kutwa zikakudhuru hata wewe.
Hili si jambo la kufurahia hata kidogo.
 
Kabisa. Wanaweka siasa hadi kwenye roho za watu.
Kuna kitu hakijakaa sawa kichwani mwa Watanzania na sijui nani atakiweka sawa. Kushangilia au kufurahia kifo cha binadamu mwenzako!!!! hata kama amekutendea ubaya kwa namna gani lakini katika kuondoka duniani inatakiwa tusikitike yawezekana angeweza kukomba mshamaha na mkamalizana. Lakini pia bila kujali ni askari, mwandishi wa habari, mwanachama wa chama cha upinzani au tawala wote ni binadam mauaji kwa namna yoyote ile yakemewe na kulaaniwa na mpenda haki yeyote. Eee MUNGU tuepushie uchuro huu.
 
Back
Top Bottom