Mahojiano kati ya Mungu na Mwasapila

Mahojiano kati ya Mungu na Mwasapila

Hii ishu ya Babu imekua kama Big G iliyoisha utamu tumeichoka jamani. tuongeleeni mengine

asante manyanza kwa kuliona hilo, kwani hata kwenye tv habari ya kwanza tumeizoea kuwa ni ya loliondo
 
Mwasapila amefanya kipi zaid hadi awe na mawasiliano na mungu kiasi hiko?
Maana amesisitza kua anakeep intouch na mungu zaidi ya tujuavyo,

Hii kitu imeleta maswali mengi sana kuliko majibu yake,iko kazi kubwa hapa.
 
Jana nimeckiliza clouds walivyotoa ushuhuda hakuna aliyepona ukimwi babu mwizi
 
Mpaka hapo Mungu ni bussiness man, ana kazi na hizo fedha.
 
''Mungu alisema na mimi kuhusu gharama za dawa na akasema kila atakayekunywa dawa ni Sh500 tu ya tanzania na nilipomuuliza kuhusu wageni alisema dola moja''.Anaeleza mchungaj Mwasapila.
Lakini anasema yeye hakuamini kuhusu kiwango hicho na alipomuuliza Mungu alimletea katika ndoto noti ya sh 500 na kumwonyesha pande zote mbili za noti hiyo akimthibitishia maono hayo.
Alipomhoj Mungu kuhusu mtunza fedha,mwasapile anasema ''Nilimuuliza mungu ni nani atakuwa mtunzaji wa fedha hizo na akanionyesha mtu atakayezitunza''.Mtu huyo ni ni muumini wa KKKT USHARIKA WA SONJO,ILA HAKUTAJA JINA LAKE.
Mwasapila anasema fedha zote zinatunzwa na kwamba Mungu alisema ana kazi nazo,anabainisha kuwa Mungu bado hajatoa tangazo kuhusu ni kazi gani fedha hizo zitafanya.


''Nasubir tangazo la mungu kwamba fedha hizo zitafanya kazi gani,ila yeye alisema zitunzwe ana kazi nazo''.Anabainisha Mwasapila

Ila alienda mbali na kusema'Pengine anataka fedha hizo zitumike kujenga sehemu mpya ambayo tutahamishia huduma,lakini sijui maana alisema atanambia matumizi yake kwa sasa siwezi kujua''

KUHUSUU MAWASILIANO NA MUNGU
Huku akitabasamu mwasapila anasema
''Aaah......yaaani Mungu anasema na mimi mara nyingi na tena ananitia moyo sana katika huduma hii ninayoifanya,hata ninapokuwa na maswali kuhusu jambo fulani katika utendaji wangu yeye ananiambia mambo mengi sana''.
Huyu ndo mwasapila
source Mwananchi la jumamos april 9,2011.
Nawasilisha


Mpaka nimsikie Mwasapila mwenyewe akisema ndo naweza kuamini haya. Kama hii ni kweli, nani aliyekuwa anatuambia kuwa kuna mgao wa 200 na 300 kati ya hizi 500. je ni huyu mzee au watu walizusha tu?
 
Huu ni uongo. Mwasapila hajaongea na Mungu bali yeye anamapepo yaliyomfanya awe mganga wa tiba za jadi. Mungu gani anaonesha dawa halafu lazima itolewe na mwasapila pekee badala ya kuruhusiwa watu wengi wamsaidie na hivyo kuondoa msongamano na kuepusha vifo vya wagonjwa. hii janja iliyoandaliwa kwa umakini mkubwa na kupigiwa debe na vyombo vya habari.
 
YOH;20:17- Yesu akamwambia usinishike ;kwa maana sijapaa kwenda kwa BABA ,lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie , ninapaa kwenda kwa BABA yangu naye ni BABA yenu, kwa MUNGU wangu naye ni MUNGU wenu , KWA HIYO UNATAKA TUAMINI KUWA WANA WA ISLAEL NAO NI MIUNGU.....?
Mkuu kwa nini umekariri hako kakifungu kamoja toka kwenye Bible halafu umekimbia kuja kuuliza swali ambalo ni jibu?! Nenda kasome Bible hiyohiyo uone. Siyo tu hao bali wote wamwaminio Yesu wanakuwa miungu... Na kwa wanaodhani kuitwa mwana/mtoto wa fulani lazima awe amejamiiana na mwanamke: Twambieni kwenye wimbo wa Taifa mnapotaja watoto wa Africa, ni lini Africa aliwaoa mama zenu?!
 
huwezi kujua uache lipi uchukue lipi utata mtupu tambua kwenda kwa babu sio lazima ila ni muhimu.
 
kweli vituko na mauzauza havitaisha!

inasemekana kuwa katika hizo 500/-:

200/- za kanisa

200/- za wachumngaji wanaomsaidia

100/- zake mwenyewe

sasa kumbe zote zake? sasa ile breakdown ya awali watu waliitoa wapi?

eti na mungu alimteulia mweka hazina!

jamani, huyu nabii wa kikombe huyu!!!

Hapo sasaaaa!!!! Mpaka mtunza hazina Mungu kamfunilia atakuwa ni yupi, Inaonyesha Mungu anajua mahesabu maana amempangia kabisa, kuwa wageni ni dollar 1,
 
Kuna jirani yangu kapigwa na mtu kisa kasema babu muongo. Amemwambia huyo kaka kuwa kapoteza hela yake kwenda samunge, we kapata kichapo cha hatari. Nadhani watu wengi wameshakuwa brainwashed kabisa.
 
kila umwitae baba ni BABA YAKO,
YESU HAKUWAI KUMWITA MUNGU BABA,MSIMZUSHIE MTUME WA MUNGU HUYU,

JOHN 11

41 So they took away the stone. Then Jesus looked up and said, “Father, I thank you that you have heard me. 42 I knew that you always hear me, but I said this for the benefit of the people standing here, that they may believe that you sent me.”
 
Hivi anapowasiliana nae {Huyo Mungu} humjia vipi? Anaona umbo au anasikia sauti? Waandishi wetu wa habari sijasoma anywhere kama wamehoji hili. Anapata uhakika gani kama 'anaoteshwa' yawezekana 'anaota'.
 
Mkuu kwa nini umekariri hako kakifungu kamoja toka kwenye Bible halafu umekimbia kuja kuuliza swali ambalo ni jibu?! Nenda kasome Bible hiyohiyo uone. Siyo tu hao bali wote wamwaminio Yesu wanakuwa miungu... Na kwa wanaodhani kuitwa mwana/mtoto wa fulani lazima awe amejamiiana na mwanamke: Twambieni kwenye wimbo wa Taifa mnapotaja watoto wa Africa, ni lini Africa aliwaoa mama zenu?![/QUOTE]

You really made my day, i laughed. Nadhani umemjibu vizuri Bajabiri na bila shaka ataelewa kuwa YESU kuwa Mwana wa Mungu sio katika normal context. Na akisikia YESU ni Mungu mwenyewe ndio atachanganyikiwa zaidi.

2 corinthians 4:4 "The god of this age has blinded the minds of unbelievers, so that they cannot see the light of the gospel of the glory of Christ, who is the image of God."
 
1samweli 10:6-7.
Huyu anatumia haki hii hapa kwenye hii mistari, na kama hii haki haipo basi hatuna yeyote anaeweza kudai kuongea na Mungu. Na kwa namna hiyo Mungu atakuwa hayupo.
Kuna watu wanajiita mitume na na manabii na wanatumia vitu mbali mbali kuwauzia watu kama usaidizi wa uponyaji wa kiungu tena kwa bei mbaya.
Vitu hivyo ni kama, maji, sabuni, mafuta ya mizetuni, vitambaa, chumvi na vingi vya namna hiyo na wanadai ukila utapokea uponyaji.
Sasa hawa utawatofautisha vipi na babu? Kinachoonekana hapa ni babu kuwabana katika biashara zao za injili, kwani yeye kikombe ni sh. 500 na anayafanyia haya nyumbani kwake.
Hawa manabii na mitume wanazifanyia hizi biashara kwenye nyumba za ibada na kufanya hiyo shughuli kuwa sehemu ya neno.
.
 
Hapo sasaaaa!!!! Mpaka mtunza hazina Mungu kamfunilia atakuwa ni yupi, Inaonyesha Mungu anajua mahesabu maana amempangia kabisa, kuwa wageni ni dollar 1,

Yeye haulizi jina,umri,ugonjwa,uraia nk,hiyo dollar anacharge vp?
 
Back
Top Bottom