pcman
JF-Expert Member
- Oct 9, 2008
- 742
- 186
Naamini Utajifunza kitu!
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Jaji Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu
Jaji Mkuu: Nikuulize katika uelewa wako jopo la majaji watano wa mahakama ya rufani linakaa wakati gani?
AG: Majaji watano wanakaa baada ya majaji watatu kukaa na jopo hilo la majaji watano linafanyia marejeo uamuzi wa majaji watatu kama kulikuwa na malalamiko ya uamuzi uliotolewa na majaji watatu.
Jaji Mkuu: Kesi ikishafunguliwa Mahakama ya Rufani haikatiwi tena kitakachofanyika ni kufanyiwa mapitio ya uamuzi sasa sijui tatizo hapa linatoka wapi! Na Mgombea binafsi ni suala kubwa nchini na ndiyo maana mahakama yetu imepanga idadi kubwa ya majaji na Mahakama ya Rufani ina mamlaka hayo...sasa sijui tatizo linatoka wapi.
AG: Basi Jaji Mkuu nimekuelewa naondoa hoja.
Masaju alidai Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ndiyo iliyokata rufaa na waliwapatia hoja kwa vielelezo upande wa wadaiwa Ijumaa iliyopita na wao wakaturudishia majibu Jumamosi na aliyepewa ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Mwaimu, ambaye anauguliwa.
Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza, anayesaidiana na Mpale Mpoki alikiri kupatiwa vielelezo kwa maandishi na upande wa mkata rufani na kwamba wao waliitumia siku ya Jumamosi na Jumapili iliyopita kujiaandaa na wako tayari kuendelea kusikilizwa kwa rufaa hiyo.
Jaji Mkuu: Hivi course list (ratiba ya kikao cha Mahakama ya Rufani) ilitoka lini?
AG: Januari 28 mwaka huu.
Jaji Mkuu: Sasa kilichoifanya ofisi ya AG, muwa-save wadaiwa hivyo vielelezo vyenu Ijumaa iliyopita ni kitu gani? Na suala la Mwaimu kuuguliwa na baba yake tafadhari naomba liwekwe kando sasa.
AG: Mh! Mheshimiwa Jaji Mkuu hata jopo lako limekubali rufaa hii ni nzito....hivyo bado tunafanyia utafiti hoja zetu tutakazoziwasilisha katika rufani hii.
Jaji Mkuu: Hivi si ni serikali ndiyo iliyokata rufaa, ina maana siku zote hizo hamkufanya utafiti na kama leo hii (jana) mnadai bado hamjafanya utafiti na zile sababu sita mlizoziwasilisha kwenye rufaa yenu nazo ina maana pia hamkuzifanyia utafiti? Na mnakataje rufaa bila kufanya utafiti?
AG: Mhh (kimya).
Jaji Mkuu: Swali langu linabaki palepale inakuaje ofisi ya AG iu-save vielelezo upande wa mdaiwa Ijumaa iliyopita?
AG: Mhh! Tunaepuka malalamiko kwamba wanasheria wa serikali tumekuwa tukifungua kesi bila kufanya utafiti wa kutosha. Na tunaomba msajili wa Mahakama ya Rufani aipange rufaa hii katika kikao kijacho.
Jaji Mkuu: Kwani Msajili wa Mahakama ya Rufani atajuaje kama mmeishamaliza kufanya utafiti wenu? Kwani Msajili wa Mahakama ya Rufaa akiwa anapanga course list huwa anaihusisha ofisi ya AG?
AG: Hapana.
Jaji Mkuu: Inasikitisha sana kuona kauli hiyo inatolewa na Naibu Mwanasheria Mkuu anayetokea ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yaani nyie ndiyo mmekata rufaa halafu mnasema hamjajiandaa! Wenzenu wa utetezi mmewapatia vielelezo vyenu na wamejiandaa ndani ya siku mbili...halafu nyie wanasheria wa serikali ndiyo mnaoingoza bar (meza ya mawakili wa pande zote mbili) sasa sijui mnaongoza nini (watu wakaangua vicheko).
AG: Mi najitetea, mi niliteuliwa hivi karibuni kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jaji Mkuu: Hakuna cha kujitetea hapa. Jopo liko tayari kuahirisha usikilizaji wa rufaa hii sasa nyie semeni tuiahirishe hadi lini?
AG: Tunaomba miezi minne ijayo kuanzia leo.
Jaji Mkuu: Tunaiarisha rufaa hii hadi April 8.
Source:Tanzania daima,
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12889