Mahojiano kati ya Jaji Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu

pcman

JF-Expert Member
Oct 9, 2008
742
186
Naamini Utajifunza kitu!

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Jaji Mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu

Jaji Mkuu: Nikuulize katika uelewa wako jopo la majaji watano wa mahakama ya rufani linakaa wakati gani?

AG: Majaji watano wanakaa baada ya majaji watatu kukaa na jopo hilo la majaji watano linafanyia marejeo uamuzi wa majaji watatu kama kulikuwa na malalamiko ya uamuzi uliotolewa na majaji watatu.

Jaji Mkuu: Kesi ikishafunguliwa Mahakama ya Rufani haikatiwi tena kitakachofanyika ni kufanyiwa mapitio ya uamuzi sasa sijui tatizo hapa linatoka wapi! Na Mgombea binafsi ni suala kubwa nchini na ndiyo maana mahakama yetu imepanga idadi kubwa ya majaji na Mahakama ya Rufani ina mamlaka hayo...sasa sijui tatizo linatoka wapi.

AG: Basi Jaji Mkuu nimekuelewa naondoa hoja.

Masaju alidai Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ndiyo iliyokata rufaa na waliwapatia hoja kwa vielelezo upande wa wadaiwa Ijumaa iliyopita na wao wakaturudishia majibu Jumamosi na aliyepewa ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Mwaimu, ambaye anauguliwa.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza, anayesaidiana na Mpale Mpoki alikiri kupatiwa vielelezo kwa maandishi na upande wa mkata rufani na kwamba wao waliitumia siku ya Jumamosi na Jumapili iliyopita kujiaandaa na wako tayari kuendelea kusikilizwa kwa rufaa hiyo.

Jaji Mkuu: Hivi course list (ratiba ya kikao cha Mahakama ya Rufani) ilitoka lini?

AG: Januari 28 mwaka huu.

Jaji Mkuu: Sasa kilichoifanya ofisi ya AG, muwa-‘save’ wadaiwa hivyo vielelezo vyenu Ijumaa iliyopita ni kitu gani? Na suala la Mwaimu kuuguliwa na baba yake tafadhari naomba liwekwe kando sasa.

AG: Mh! Mheshimiwa Jaji Mkuu hata jopo lako limekubali rufaa hii ni nzito....hivyo bado tunafanyia utafiti hoja zetu tutakazoziwasilisha katika rufani hii.

Jaji Mkuu: Hivi si ni serikali ndiyo iliyokata rufaa, ina maana siku zote hizo hamkufanya utafiti na kama leo hii (jana) mnadai bado hamjafanya utafiti na zile sababu sita mlizoziwasilisha kwenye rufaa yenu nazo ina maana pia hamkuzifanyia utafiti? Na mnakataje rufaa bila kufanya utafiti?

AG: Mhh (kimya).

Jaji Mkuu: Swali langu linabaki palepale inakuaje ofisi ya AG iu-‘save’ vielelezo upande wa mdaiwa Ijumaa iliyopita?

AG: Mhh! Tunaepuka malalamiko kwamba wanasheria wa serikali tumekuwa tukifungua kesi bila kufanya utafiti wa kutosha. Na tunaomba msajili wa Mahakama ya Rufani aipange rufaa hii katika kikao kijacho.

Jaji Mkuu: Kwani Msajili wa Mahakama ya Rufani atajuaje kama mmeishamaliza kufanya utafiti wenu? Kwani Msajili wa Mahakama ya Rufaa akiwa anapanga course list huwa anaihusisha ofisi ya AG?

AG: Hapana.

Jaji Mkuu: Inasikitisha sana kuona kauli hiyo inatolewa na Naibu Mwanasheria Mkuu anayetokea ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yaani nyie ndiyo mmekata rufaa halafu mnasema hamjajiandaa! Wenzenu wa utetezi mmewapatia vielelezo vyenu na wamejiandaa ndani ya siku mbili...halafu nyie wanasheria wa serikali ndiyo mnaoingoza bar (meza ya mawakili wa pande zote mbili) sasa sijui mnaongoza nini (watu wakaangua vicheko).

AG: Mi’ najitetea, mi’ niliteuliwa hivi karibuni kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jaji Mkuu: Hakuna cha kujitetea hapa. Jopo liko tayari kuahirisha usikilizaji wa rufaa hii sasa nyie semeni tuiahirishe hadi lini?

AG: Tunaomba miezi minne ijayo kuanzia leo.

Jaji Mkuu: Tunaiarisha rufaa hii hadi April 8.


Source:Tanzania daima,
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12889
 
huyo jaji nkuu anafurahisha baraza tu. mahakama ni chombo cha dola na ipo kwa ajili ya dola. mahakama huundwa na serikali kwa ajili ya kuiwezesha serikali ufanya kazi zake japo nadharia ya mahakam imejenga matumaini makubwa kwa raia wa kawaida kupatiwa haki. ndio maana wajuavo wa mambo ya mahakama wanasema , mahakamani hakuna haki bali kuna sheria, na kama mjuavyo wte sheria hutungwa na serikali na kugongwa mhuri na bunge

mwisho wa siku serkali itashinda na wanaojiandaa kugombea kama wagombea binafsi waanze kuanzia sasa kujihesabu wameumia!
 
Msiwe kama Thomaso. Mpeni ya Kaisari yaliyo ya Kaisari. Jaji Mkuu kaonyesha uwezo wake kama kiongozi wa Mhimili wa Mahakama/Sheria kwa kumbana na kudhihirisha ubovu uliopo kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
 
huyo jaji nkuu anafurahisha baraza tu. mahakama ni chombo cha dola na ipo kwa ajili ya dola. mahakama huundwa na serikali kwa ajili ya kuiwezesha serikali ufanya kazi zake japo nadharia ya mahakam imejenga matumaini makubwa kwa raia wa kawaida kupatiwa haki. ndio maana wajuavo wa mambo ya mahakama wanasema , mahakamani hakuna haki bali kuna sheria, na kama mjuavyo wte sheria hutungwa na serikali na kugongwa mhuri na bunge

mwisho wa siku serkali itashinda na wanaojiandaa kugombea kama wagombea binafsi waanze kuanzia sasa kujihesabu wameumia!

Actually ingawa sikubaliani na maelezo yako lakini kwa hili naomba nikiri kuwa kwa uamuzi uliotolewa mahakama imepotoka.

Ukisoma kifungu kifuatacho cha sheria ya Basic Duties and Enforcement Act kumbe mahakama haina uwezo wa kusema kuwa mgombea binafsi anaruhusiwa. Najua hapa si jukwaa lake. mjadala naupeleka jukwaa la sheria.

Section 14(3):Notwithstanding the provisions of the Civil Procedure Code or of any other law to the contrary, where in proceedings under this Act which do not involve continuous breach or personal injuries, the Government files a notice of intention to appeal against any decision of a court, the notice shall, when entered, operate as a stay of execution upon the decision sought to be appealed against.
 
Back
Top Bottom