Siku hizi ram zina bei Sana huko Duniani, hio laki 5 anaweza hata ram hio 32GB asipate. Ila kibongo bongo desktop mtumba bado bei ipo vizuri.
Ushauri wangu tafuta workstation hapa hapa bongo za kina HP Na dell, ukipata workstation za Xeon itakua Mali Sana za karibuni ila hata hizi consumer Cpu ni Sawa, cha muhimu ni kutafuta desktop ambayo in power supply kubwa ili isikulimit kwenye GPU.
Dell Vostro za hio gen ya 10 rahisi kupata mtaani sometime chini ya laki 3, sema PSU itabidi ubadili mwenyewe.
Dell precision 3630 niliwahi ziona, hizi ni full workstation, zinakubali Xeon, ni gen ya 8 Ila zisikupe shida Sana sababu kuna Xeon equivalent ya i9 9900 ambazo zina nguvu kuliko gen ya 10 i7. Bei zake ni kwenye laki 3 Hadi 4.
Option nyengine ni kununulia Kenya hizo Ryzen, naona HP pro desk zenye PSU 400W na Ryzen 2600/2700/3600 around laki 4 ya kibongo, hio PSU haikubali GPU kubwa ila Rtx xx60 series zinakaa bila shida ama hio gtx 1660.