Mahitaji muhimu unapotaka kusajili kampuni yako

Mahitaji muhimu unapotaka kusajili kampuni yako

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,702
Reaction score
3,742
1*wyqEafNzdWrOcmCEjZz8MA.png

Vitu Vinavyohitajika Kumiliki Kampuni​

1. Jina la Kampuni
Kuchagua jina sahihi la kampuni ni hatua ya kwanza muhimu. Jina lako linapaswa kuwa huru kufanya biashara nyingi tofauti chini yake bila kujifunga kwenye sekta moja. Unapochagua jina lisilopendelea biashara fulani, kama ABC Company Limited badala ya ABC Transport Company Limited, unajipa nafasi ya kupata leseni mbalimbali na kupanua biashara yako kadri unavyotaka bila kubadilisha jina.

2. Shughuli za Biashara
Ni lazima uorodheshe shughuli zote unazotarajia kufanya kupitia kampuni yako. Kadri unavyopanua orodha hii, ndivyo unavyoongeza wigo wa fursa. Mara nyingi, wataalam wetu hukushauri kuongeza pia sekta zinazokupa nafasi ya mikataba na tenda zaidi, hata zile ambazo huenda hukuzifikiria awali.

3. Mtaji wa Kampuni (Share Capital)
Kila kampuni huanza na thamani ya mtaji wa awali, inayojulikana kama share capital value. Hii inaweza kuwa kuanzia milioni 1, milioni 5, milioni 20, milioni 50, au zaidi. Haumaanishi lazima uwe na fedha hizi benki; ni makadirio ya thamani ya kampuni yako kulingana na wazo lako, mali ulizo nazo, elimu na uzoefu wako. Thamani hii inaweza kuongezeka kadri kampuni inavyokua.

4. Wamiliki wa Kampuni (Shareholders)
Kampuni lazima iwe na angalau wamiliki wawili. Unaweza kumshirikisha ndugu au mtu wa karibu kama mmiliki mdogo, huku wewe ukiendelea kushikilia umiliki mkubwa. Hii inarahisisha taratibu za usajili na huongeza uthabiti wa kampuni.

5. Taarifa za Wamiliki
Unapaswa kutoa taarifa kamili za kila mmiliki, ikiwemo jina kamili, tarehe ya kuzaliwa, asilimia ya umiliki na anuani ya makazi. Hii ni sehemu muhimu ya mchakato wa usajili wa kampuni na inaleta uwazi na uaminifu mbele ya mamlaka husika na washirika wa kibiashara.

Mimi na timu yangu ya Victoria Agency tutakusaidia kila hatua kuanzia kuchagua jina sahihi, maandalizi ya nyaraka, hadi kukukabidhi cheti cha usajili wa kampuni yako, popote ulipo Tanzania.
Piga simu au WhatsApp +255693880325 sasa ili tuanze mchakato wako leo!
 
Back
Top Bottom