Mahekalu ya Vigogo kuvunjwa ufukweni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahekalu ya Vigogo kuvunjwa ufukweni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikrapevu sungura, May 4, 2012.

 1. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  By Habari Leo

  Mahekalu ya Vigogo kuvunjwa ufukweni

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ametoa wiki mbili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, kutoa notisi kwa watu waliojenga ndani ya meta 60 pembeni mwa bahari na maeneo oevu, kuonesha hatimiliki zao.

  Katika agizo hilo, amesema ikiwa watakuwa na hatimiliki halali, Serikali itajadiliana nao na wakikutwa bila hatimiliki, watanyang’anywa maeneo yao bila fidia.

  Alisema hayo juzi alipofanya ziara katika Manispaa ya Kinondoni kwenye maeneo yenye malalamiko ya upangaji, upimaji na uendelezaji na kuagiza kubomolewa kwa baadhi ya majengo baada ya kukutwa yamejenga ndani ya barabara.

  Aidha, aliziagiza halmashauri zote nchini, kuondoa majengo yaliyojengwa kinyume cha sheria na kuhakikisha wanasimamia upangaji na uendelezaji miji, kama ilivyoainishwa katika sheria za nchi ya Mipangomiji ya mwaka 2007.

  “Maendelezo yote hapa ni batili, tunataka maeneo yote yaliyo ndani ya meta 60 yaondolewe bila ubaguzi, kwa sababu hakuna mtu aliye juu ya sheria.

  “Kama wana hati, tutazungumza ila kama hawana, wataondoka mikono mitupu, hizi fukwe lazima tuzifunge kwa maslahi ya vizazi vyetu,” alisema.

  Alisema kuwa uendelezaji na utumiaji wa ardhi ndani ya miji unatakiwa kuzingatia mpango uliopo ili kuleta uwiano mzuri wa maendelezo jirani au katika jamii na hivyo kuondoa mgongano wa matumizi ya ardhi.

  “Limekuwapo tatizo kubwa la miji yetu kuendelezwa kiholela kana kwamba hakuna sheria yoyote inayosimamia uendelezaji wa miji. Hali hii inachangia kuwepo kwa kero kwa jamii na uharibifu wa mazingira na hili limekuwa tatizo sugu katika miji yetu,” alisema.

  Alisema operesheni hiyo na ukaguzi wa maeneo ambayo hayajafuata utaratibu ni ya nchi nzima, ila ameamua kuanzia ziara yake Kinondoni kutokana na kwamba amekuwa akipokea simu si chini ya 50 kila siku za malalamiko ya uvunjwaji wa sheria ya mipangomiji katika manispaa hiyo.

  “Mipangomiji haifanyi kazi kwa sababu sheria mnazozisimamia hamzifahamu, kuna siku tutawanyang’anya madaraka na tutakuwa tunapanga kila kitu wizarani… sasa hivi ni wakati wa vitendo, lazima tufanye kazi Watanzania waelewe na waone,” alisema.

  Alisema kutokana na ujenzi holela, yapo maeneo ambayo kipindi cha mvua mafuriko yanazidi, kwa kuwa mikondo ya kupitisha maji imebadilishwa matumizi na watu wachache kujimilikisha na kujenga nyumba bila vibali.

  Katika ziara yake hiyo Mbezi-Kawe aliagiza eneo la kwa Msomali kiwanja namba 1057 karibu na kiwanja namba 944 ambalo limejengwa ghorofa livunjwe kwa kuwa mwendelezaji wa eneo hilo amejenga ndani ya meta 10 za barabara.

  Alisema wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika kuwa hawana barabara ya kuingilia, hivyo lazima haki itendeke bila kuangalia uwezo wa mtu.

  Aliagiza viwanja namba 2020 na 2021 vya Kawe Beach; viachwe wazi kwani ni sehemu ya kupumulia bahari, na wahusika wapewe hati ya kusimamisha ujenzi haraka.

  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alipongeza jitihada za Wizara hiyo na kutaka hatua stahiki zichukuliwe kwa maslahi ya Taifa.

   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama wana hati tutazungumza nao : hapo nimekerwa sana
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  unapo revoke right of occupancy lazima utoe fidia ya property iliyopo worth the value of the current market price .... hapa makosa yanakuwa yalishafanywa na serikali yenyewe
   
 4. c

  care New Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utekelezaji uwe wa kweli
   
 5. T

  Turbulence Senior Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Another insanity! Wakati wanajenga Serikali ilikuwa likizo?? All these years? Izi ni siasa tu, tena za kisanii, hao wanaofanya maamuzi ndio wenye hayo mahekalu huko beach.
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mama Jitahidi Kidogo na ongeza Kasi, Ila nadhani Unapambana na Makubwa sana Huku Madogo Ukiwa Umeyafumbia Macho!! Kuna maeneo Kama Sinza na Mikocheni yapo planned ila waharibifu Wachache Wamengoa bicon na Kujenga na Kubana Barabara!! Imekuwa maeneo mengi Barabara Zimefinywa!! Hivyo mama Waziri Huoni ni muda muafaka Kwenda kutambua Mipaka iliyofinywa na hawa wenye Uchu na public land!! Pia maeneo ya Kimara na kwingineko ujenzi holela unaendelea, ila hali sio Mbaya sana Huoni ni muda Mufaka kwenda kutambua Public Lands!! Dispensaries, Barabara, Schools Nk, Nk? Mama Fanya Hima bado hujachelewa sana!! - Nawasilisha
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hii serikali itakuambia itakulipa utasubiri miaka nenda rudi hupati hiyo pesa... Jiulizeni hii ni mara ya ngapi huyu mama ameagiza hizo nyumba zivunjwe na hazivunjwi?? mbona wakienda kariakoo kuvunja ni mara moja nyumba au vibanda vinabomolewa...tatizo safari hii wamekutana na kisiki...nyumba huko ni za wakubwa...
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  le mutuz nyumba yenu itapona kweli?
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  mama anajitahidi kumuiga maghufuli ila ataishiwa kuwa mdogo
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ilikuwaje wizara ikatoa hati kimakosa? Hapo watendaji wa wizara ndo wanapashwa kurudisha gharama za kurevoke hiyo right na siyo serikali maana watakuwa wanatumia kodi zetu kwa faida ya watendaji. Hati hizi mara nyingi huwa za magumashi kwa hiyo hata mwenye hati analijuwa hilo hata asipopata fidia moyoni anajua ukweli. Ikiwezekana mtendaji wizara aliyemdhibitishia kuwa kiwanja kile ni halali ndiyo amshitaki arudishe gharama zake
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Biashara moja huzaa biashara nyingine...hii ndo Tanzania yetu bwana
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  kuna mtu kanidokeza eti hiyo ni mali ya Rz1.
   
 13. p

  petrol JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kauli zinazotolewa humu jamvini zinanishutua kidogo kuhusu maamuzi ya Waziri Tibaijuka. Serikali ikikaa kimya tunaishutumu/tunalalamika. Serikali ikiamua kurekebisha makosa ya nyuma ili kuwa kwenye mstari unaoeleweka vile vile tunaikosoa/kulalamika. Sasa serikali ifanye nini ili turidhike. Tumekuwa kama mapunguani. Hii inasikitisha sana. Tujaribu kutoa mawazo ya kujenga, kukosoa/kulalamika tu hakutaleta tija.
   
 14. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hayo ni matamshi tu,hakuna kitakacho fanyika.
  Anatuelewa wa bongo tulivyo,habari mpya ikitoka na tunajua ni kiini macho tunashabikia kwa wiki moja
  baada ya wiki tumesahau na anaibuka kiongozi mwingine kutupa kiini macho kingine.
   
 15. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mkuu watu wanalalamika kwa sababu anasemea ambayo kwa sasa si priority za wananchi though yaweza kuwa ni muhimu......

  Unakumbuka tarehe ya mwisho ardhi kutoa tamko la viwanja kuuzwa kwa wananchi?????
  Maeneo ya wazi huku uswahilini yamejengwa watoto hawana pa kuchezea......amefanya nini????
  Watu wanataka ardhi ya kujenga....... haya ndo public hayo ya kuvunja kama anaweza na ana nia wala hayana haja ya kutangazwa naye......ye atekeleze tu sisi tutasikia kama habari baada ya.......

  Wananchi wanateseka na ardhi...kipaumbele kwa ecosystem????? Nani atanufaika kama walengwa wako hoi kwa taabu ya ardhi??
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nitaamini nitakapoona vifusi!
   
 17. M

  Marytina JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ajaribu aone
   
 18. M

  Moony JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mama anasoma JF?
   
 19. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Huyu mama amezinduka baada ya kurudisha gari...au inakuwaje???
   
 20. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  hilo nalo neno.
   
Loading...