Mahekalu ya Vigogo kuvunjwa ufukweni

Kweli maana sio mara ya kwanza anatoa kauli km hz na hakuna kinachofanyika, na huko ni kwa vigogo atadondokea pua tu!
 
Olesaidimu,

Kuna aina ya ka ukweli katika maelezo yako. Matamshi yanakuwa mengi na marefu wakati utekelezaji unasuasua. Nenda hapo cocobeach kwa mfano. Nilielezwa na mjomba wangu kuwa mika zaidi ya kumi iliyopita kulikuwa na Mkurugenzi wa Jiji (kama sikukosea) kwa jina la Keenja akazuia magari kuegeshwa kwenye ufukwe wa bahari usije ukamomonyoka na kutishia barabara kama pale barabara ya magogoni/hospitali ya Agha Khana. Jiji (au serikali) wakati huo ikaingia gharama kubwa ya kuchimbia vizuizi. Nenda leo, wenzetu wanapaki magari hadi kwenye maji. Hilo tumelisahau, na hata gharama hizo tumezisahau. Pengine mama Tibaijuka angetupia macho huko pia. Na huko msasani miaka ya utawala wa Mwalimu Nyerere ulikuwa unaweza kutembea baharini ukipunga upepo mwanana kutoka msasani kwa mwamwinyi (enzi hizo maana naona sasa wamehama kiaina) hadi Silversands. Leo watu wamejitwalia na kujimilikisha maeneo yanayopakana na bahari. Huwezi kufika baharini kwa urahisi. Kwingine unatakiwa kulipia kupita tu. Mama Tibaijuka apanue macho zaidi. Tunamtakia kila la kheri. Lakini nasi tumuunge mkono.
 
.....kubomoa ni kazi nyepesi kuliko kujenga. Nakubaliana na amri hiyo itekelezwe, lakini pia ni vyema kukawa na utaratibu mzuri wa kudhibiti hali hiyo isijitokeze. Angalia kasi ya ujenzi holela inavyoendelea huko pembezoni mwa jiji. Baadaye tutaanza tena kazi ya kuwabomolea wananchi wakati serikali haionyeshi jitihada za kupima viwanja kwa sasa.
 
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ametoa wiki mbili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, kutoa notisi kwa watu waliojenga ndani ya meta 60 pembeni mwa bahari na maeneo oevu, kuonesha hatimiliki zao.

Katika agizo hilo, amesema ikiwa watakuwa na hatimiliki halali, Serikali itajadiliana nao na wakikutwa bila hatimiliki, watanyang’anywa maeneo yao bila fidia.

Alisema hayo juzi alipofanya ziara katika Manispaa ya Kinondoni kwenye maeneo yenye malalamiko ya upangaji, upimaji na uendelezaji na kuagiza kubomolewa kwa baadhi ya majengo baada ya kukutwa yamejenga ndani ya barabara.

Aidha, aliziagiza halmashauri zote nchini, kuondoa majengo yaliyojengwa kinyume cha sheria na kuhakikisha wanasimamia upangaji na uendelezaji miji, kama ilivyoainishwa katika sheria za nchi ya Mipangomiji ya mwaka 2007.

“Maendelezo yote hapa ni batili, tunataka maeneo yote yaliyo ndani ya meta 60 yaondolewe bila ubaguzi, kwa sababu hakuna mtu aliye juu ya sheria.

“Kama wana hati, tutazungumza ila kama hawana, wataondoka mikono mitupu, hizi fukwe lazima tuzifunge kwa maslahi ya vizazi vyetu,” alisema.

Alisema kuwa uendelezaji na utumiaji wa ardhi ndani ya miji unatakiwa kuzingatia mpango uliopo ili kuleta uwiano mzuri wa maendelezo jirani au katika jamii na hivyo kuondoa mgongano wa matumizi ya ardhi.

“Limekuwapo tatizo kubwa la miji yetu kuendelezwa kiholela kana kwamba hakuna sheria yoyote inayosimamia uendelezaji wa miji. Hali hii inachangia kuwepo kwa kero kwa jamii na uharibifu wa mazingira na hili limekuwa tatizo sugu katika miji yetu,” alisema.

Alisema operesheni hiyo na ukaguzi wa maeneo ambayo hayajafuata utaratibu ni ya nchi nzima, ila ameamua kuanzia ziara yake Kinondoni kutokana na kwamba amekuwa akipokea simu si chini ya 50 kila siku za malalamiko ya uvunjwaji wa sheria ya mipangomiji katika manispaa hiyo.

“Mipangomiji haifanyi kazi kwa sababu sheria mnazozisimamia hamzifahamu, kuna siku tutawanyang’anya madaraka na tutakuwa tunapanga kila kitu wizarani… sasa hivi ni wakati wa vitendo, lazima tufanye kazi Watanzania waelewe na waone,” alisema.

Alisema kutokana na ujenzi holela, yapo maeneo ambayo kipindi cha mvua mafuriko yanazidi, kwa kuwa mikondo ya kupitisha maji imebadilishwa matumizi na watu wachache kujimilikisha na kujenga nyumba bila vibali.

Katika ziara yake hiyo Mbezi-Kawe aliagiza eneo la kwa Msomali kiwanja namba 1057 karibu na kiwanja namba 944 ambalo limejengwa ghorofa livunjwe kwa kuwa mwendelezaji wa eneo hilo amejenga ndani ya meta 10 za barabara.

Alisema wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika kuwa hawana barabara ya kuingilia, hivyo lazima haki itendeke bila kuangalia uwezo wa mtu.

Aliagiza viwanja namba 2020 na 2021 vya Kawe Beach; viachwe wazi kwani ni sehemu ya kupumulia bahari, na wahusika wapewe hati ya kusimamisha ujenzi haraka.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alipongeza jitihada za Wizara hiyo na kutaka hatua stahiki zichukuliwe kwa maslahi ya Taifa.

Chanzo:HabariLeo
 
Wewe uko usingizini, kwani baraza la mawaziri limeisha tangazwa??????????

Sea cliff ya karume family,golden tulip ya mwinyi family pia kuna police officers mess waanza hizo kwanza kama kweli
 
Serikali leo asubuhi imeanza kubomoa nyumba zilizojengwa kando kando ya bahari kinyume cha sheria jijini Dar es salaam.Kiasi cha majengo zaidi ya 100,yakiwemo mahekalu ya watu wazito yanatazamiwa kubomolewa bila fidia yoyote.
source: Mwananchi online
Send to a friend

hamna kitu hapo mzee,kiini macho!!!Ulisikia wapi kigogo wa tz anaguswa au ana "ngoma?"
 
Bado sana hizi ni mbwembwe tu

NI KWELI ONA HAPA. Si unaona hapo jamaa kashetapeliwa kiwanja na sasa analizwa angalia hapo. mambo yaenda yakibadilika mzee

RL8YtqzET5gK2uNjJeEkB7fwFGBDQzgd1CyH9YsKOs0umoiZMykWM29b+LzeHFD1h+Px7AAAAAElFTkSuQmCC

00000001bomoapic.jpg

Serikali leo asubuhi imeanza kubomoa nyumba zilizojengwa kando kando ya bahari kinyume cha sheria jijini Dar es salaam.Kiasi cha majengo zaidi ya 100,yakiwemo mahekalu ya watu wazito yanatazamiwa kubomolewa bila fidia yoyote.
 
Yale majengo ya Rostam Aziz pale Masaki, alikonyakulia hoteli ya umma na kuibomoa na kujenga mansions za ajabu kwenye eneo letu hilo kifisadi, nayo yapo kwenye orodha au??

Na rushwa walizopokea serikali wakati wa kuuza viwanja viliviopo ndani ya mita 200 toka ufukwe wa bahari, kinyume na maelekezo ya sheria, nayo wanatangulia kurudisha kwa wale walowapa hizo rushwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom