Mahari yazua kizazaa

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,726
19,874
Hivi mahari ina maana gani? Ina muhimu gani? Na je kiwango chake kinategemea kigezo gani? Na je imeanza lini kihistoria? Jamani hebu tulijadili hili swala maana linaelekea kuvunja mahusiano ya watu fulani.
 
labda ungeelezea kizaazaa chenyewe hata juu juu tu ili tujue nini cha kujadili

jamaa yangu kaambiwa apeleke milion 5 ili amuoe binti yao na jamaa ndo kwanza kapata kazi(bank teller) wazazi hawataki kulipwa nusu nusu.Jamaa amekasirika hadi kufikia kutaka kuamua kuvunja uhusiano.
 
jamaa yangu kaambiwa apeleke milion 5 ili amuoe binti yao na jamaa ndo kwanza kapata kazi(bank teller) wazazi hawataki kulipwa nusu nusu.Jamaa amekasirika hadi kufikia kutaka kuamua kuvunja uhusiano.

Hao wako kibiashara zaidi.

Kama matatizo yanaanzia kwenye mahari tu, wakwe wakitaka kupelekwa shopping Dubai itakuwaje?

Vijana tukikataa kuoa mnatushangaa.

Tafuta binti wa Kizaramo, utapewa vikorokoro viiingi vya kutoa kwa babu, bibi, shangazi, mama, baba, hesabu yake vyote na mahari hata laki tano havifiki.

Ila uwe tayari kwa ngoma kila mwezi kama unaoa kigori typical.
 
Wakwe ni WACHAGA anasema wanahisi anapata mshahara mkubwa kisa anafanya kazi bank
 
jamaa yangu kaambiwa apeleke milion 5 ili amuoe binti yao na jamaa ndo kwanza kapata kazi(bank teller) wazazi hawataki kulipwa nusu nusu.Jamaa amekasirika hadi kufikia kutaka kuamua kuvunja uhusiano.

inawezekana wazazi wa binti hawamtaki ndo maana wamemtajia kiasi kikubwa wanajua atashindwa........

Azungumze na mwenzie wajue wafanye nini
 
huyo dada ana uzuri gani au mwenzetu ana kitu special ambacho wengine hatuna mpaka wazazi wanadai mahari yote hiyo!
 
Kimsingi wazazi hawataki kumwoza binti yao kwa huyu jamaa, kwani kesi kama hii ilitokea chuo kikuu ambapo lecture alimpenda msichana wakati wazazi walikataa, jamaa aliambiwa atoe mahali million 3 wakidhani atashindwa lakini kumbe jamaa alikuwa kajipanga
 
Wakwe ni WACHAGA anasema wanahisi anapata mshahara mkubwa kisa anafanya kazi bank

Kama kweli yupo serious apeleke "mkia wa Simba".

"Mkia wa Simba" ni MTU ANAYEHESHIMIKA KATIKA FAMILIA...ambaye atazungumza kwa niaba ya Familia...

Huo ni mtihani mdogo sana...katika mchakato mzima wa kutafuta mwenza, provided hutaki "shortcut".

MKE ANATOKA MBALI KAKA!!!

Wengi wetu tunachukuana tu..ukizingatia na zama hizi no maadili...basi FUJO

NAUNGA MKONO APPROACH YA HAO WAKWE....MILIONI TANO UNAWEZA TAFUTA..... WENGINE WANADAI NGOZO YA CHUI kama unaakili ndogo utabaki UNALALAMIKA.

MAMBO HAYA YANATAKA CONSULTATION KWA "WATU WENYE KUYAJUA"

huyo dada ana uzuri gani au mwenzetu ana kitu special ambacho wengine hatuna mpaka wazazi wanadai mahari yote hiyo!

Mkulu
Ya huyo dada ni special, unaweza ukachukua na kufungia kwenye SAFE ukisafiri...LOL
 
Hivi mahari ina maana gani? Ina muhimu gani? Na je kiwango chake kinategemea kigezo gani? Na je imeanza lini kihistoria? Jamani hebu tulijadili hili swala maana linaelekea kuvunja mahusiano ya watu fulani.

Hao wazazi wanatamaa tu na si kingine..
Nijuavyo mimi 'mahari' ni kitu kitolewacho na kijana, kwenda kwa wazazi wa binti aliyempenda,ikiwa ni Kama shukurani kwa hao wazazi.
Mahari si lazima wazazi wa binti waipange maana ni shukurani tu.
Umuhimu wa mahari ni kuonesha uthamani kwa mwenza wako, japo wengine wanafanya mahari kama mtaji au fidia ya matunzo kwa mabinti zao.

Wazazi wa aina hiyo inabidi wabadilike..
 
[FONT=times new
roman]Kama kweli yupo serious apeleke "mkia wa Simba".

"Mkia wa Simba" ni MTU ANAYEHESHIMIKA KATIKA FAMILIA...ambaye
atazungumza kwa niaba ya Familia...

Huo ni mtihani mdogo sana...katika mchakato mzima wa kutafuta mwenza,
provided hutaki "shortcut".

MKE ANATOKA MBALI KAKA!!!
[/FONT]

Wengi wetu tunachukuana tu..ukizingatia na
zama hizi no maadili...basi FUJO

NAUNGA MKONO APPROACH YA HAO WAKWE....MILIONI TANO UNAWEZA TAFUTA.....
WENGINE WANADAI NGOZO YA CHUI kama unaakili ndogo utabaki UNALALAMIKA.

MAMBO HAYA YANATAKA CONSULTATION KWA "WATU WENYE KUYAJUA"

Naunga mkono hoja,masharo waskuizi c wamezoea mteremko,wezenu walikua wanapigana mpk wanauana ndo wanapata mke,au wanapigwanisha na cmba kifanikiwa kumuua ndo apewe mke,waliwajali na kuwathamini kwakua wanajua tabu na adha walizozipata ktk kuwapata,nyie "KAMATA MWIZI MEN"Mnataka kuteremka.akachangishane na ndg aoe km amependa mtt.
 
Hao wazazi wanatamaa tu na si kingine..
Nijuavyo mimi 'mahari' ni kitu kitolewacho na kijana, kwenda kwa wazazi wa binti aliyempenda,ikiwa ni Kama shukurani kwa hao wazazi.
Mahari si lazima wazazi wa binti waipange maana ni shukurani tu.
Umuhimu wa mahari ni kuonesha uthamani kwa mwenza wako, japo wengine wanafanya mahari kama mtaji au fidia ya matunzo kwa mabinti zao.

Wazazi wa aina hiyo inabidi wabadilike..

Sasa kama ni zawadi kwa nini wanapanga bei?
 
Hivi mahari ina maana gani? Ina muhimu gani? Na je kiwango chake kinategemea kigezo gani? Na je imeanza lini kihistoria? Jamani hebu tulijadili hili swala maana linaelekea kuvunja mahusiano ya watu fulani.

Nafikiri mahari ni kama token of appreciation kwa kijana kwenda kwa wakwe zake kuwahsukuru kwa kumlea binti ambaye muda si mrefu anaenda kuwa mke wake. Kwa zamani ili kuwa ni maidadi ya kutosha ya ng'ombe na mbuzi na mpaka baadhi ya makabila ya kitanzani ilikuwa kuwa na mtoto wa kike ni "deal"!

Kwa siku za hivi karibuni mambo yamebadilika, mahari inachukua mfumo nilioulezea hapo juu, kama asante fulani kwa wazazi kumlea binti ambaye kijana anataka kumuoa. Kwa fikra zangu nafikiri haina kiwango maalum na haipaswi kuwa na kiwango maalumu, ila kiwe kiwango ambacho ni reasonable na siyo cha kukomoana na ambacho kijana anaweza kukilipa.

Ila wapo wazee wengine bado wana fikra za zamani na wanageuza suala la binti zao kuolewa ni kama mtaji kwao. Nafikiri kwa kesi kama hizo ni vyema wazee hao wakashauriwa na wazee wengine wenye uelewa mkubwa zaidi wa haya mambo.
 
Back
Top Bottom