Je, unaweza kumlipia mzazi (baba yako) wako mahari?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,223
1,117
Mambo vipi wanajamvi!

Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja!

Iko hivi, baba na mama yako walioana miaka mingi iliyopita bila ya hata baba yako kumalizia mahari ukweni. Ahadi ya baba mzazi kwa wakwe ni kuja kumalizia taratibu huku wakiwa wanaendelea kuishi na mkewe (mama mzazi).

Wakwe wanamkubalia baba kuishi na mkewe kwa kuwa tayari amekwishalipa sehemu ya mahari. Kwahiyo, wakwe wanaamini kwamba baba angelimalizia mahari siku zijazo kwa kuwa tu uchumi ni mgumu kwake. Maisha yanaanza kati ya baba na mama; unazaliwa wewe na wadogo zako kadhaa lakini mahari bado haijakamilishwa.

Mnakuzwa na kulelewa kiugumu ugumu hivyo huku mahari bado hajikamilishwa. Watoto mnakuwa wakubwa na kuanza shule, kisha kumaliza shule kwa ngazi ya msingi, sekondari, na pengine vyuo huku baba bado mahari hajakamilisha.

Watoto mnaanza kujitegemea kimaisha na pengine Mungu amewajalia hali nzuri kiasi ya maisha bora, lakini baba mzazi bado hajakamilisha mahari. Kumbuka kwamba, ninyi watoto tangu kuzaliwa na kukua kwenu, hamkuwahi kuambiwa na wazazi wenu suala la ukamilishaji wa mahari; yaani si baba wala mama mzazi ambaye amewahi kuwatamkia kwamba "Baba yenu hajakamilisha mahari".

Baada ya ninyi watoto kuanza kujitegemea, na Mungu kuwainua kiuchumi kwa kiasi chake, siku moja baba na mama wanakorofishana na hatimaye mama mzazi anaamua kurudi kwao (ukweni kwa baba mzazi). Ndugu wa mama wanamjia juu baba kwa unyama wa kipigo aliyomfanyia mama. Baba anaomba msamaha na kuomba/kuhitaji mkewe arudi nyumbani ili maisha yaendelee.

Ndipo ndugu wa mama wanafungua faili la madai na kukuta baba hakumaliza mahari ya mkewe; ndugu wanatoa sharti kwamba ili mkewe arudi, lazima kwanza mahari ikamilishwe, la sivyo mkewe hawezi kurudi na ataendelea kuishi ukweni kwa muda wote mpaka pale mahari itakapokamilishwa.

Baada ya baba kupewa sharti hilo, hali inakuwa ngumu kwake kutimiza takwa hilo kwa muda wa haraka. Mkewe anamuhitaji, kaomba msamaha wa kadhia ya kipigo alichompa mkewe, mkewe na ndugu zake wanaupokea msamaha, lakini, changamoto ni mahari bado hajakamilisha.

Sasa je, afanyeje ili kumkomboa mkewe? Pesa ya haraka hana, hata kama atadunduliza kwa muda wa miezi sita hawezi kufikia kiwango cha mahari alichobakiza. Hii ni kwasababu kazi anayofanya baba ni yenye kipato duni sana. Ndipo wazo linamjia baba kwamba msaada pekee wa kumkomboa mkewe ni kutoka kwa watoto.

Baba anakuja kwako kukueleza tukio zima la kukorofishana na mama yako, na pia sharti alilopewa la kumkomboa mkewe. Kisha baba anakuomba msaada wa pesa iliyobakia ya mahari ili akalipe kwaajili ya kumkomboa mkewe. Wewe binafsi unatahamaki kusikia baba hakuwahi kumaliza mahari, ndipo siku hiyo unajulishwa ili umsaidie kiasi hicho cha pesa akamalizie.

Wewe kama mtoto uwezo kiuchumi siyo mbaya sana, hali ya kiuchumi inakuruhusu kumsaidia kiasi cha mahari kilichobaki. Swali ni je, utakuwa tayari kumsaidia baba yako kiasi hicho cha mahari kilichobaki ili akamkomboe mama yako na kisha maisha yaendelee?

Karibu kwa mjadala.
 
Mambo vipi wanajamvi!
Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja...
Hapa hakuna mjadala wowote, mahari huwa haimaliziwi yote hata uwe na ukwasi kiasi gani.

Wanachomtendea baba yako ni mambo ya kihuni tu na kukosa ustaarabu na issue siyo mahari.

Angekuwa amekwenda ukweni na Prado kumfuata mke wake na kuwapiga offer za bia wajomba zako haya usingeyasikia, Tena mama yako angefukuzwa kwao arudi kwa mume wake haraka.

In short poverty is decease, kama una pesa za kumsaidia mpe, unampa pesa yeye si kwamba wewe ndio unamalizia mahari, elewa vizuri sentesi hii, msaidie baba yako pesa anayokuomba, na usimpangie matumizi ya pesa hiyo yeye ndio atapanga matumizi ya pesa hiyo.

Ni uchuro kusema eti unamlipia baba yako mahari unatafuta laana, hujui mpaka hapo ulipofikia baba yako amepambana vipi au ameuza asset zake ngapi kuhakikisha wewe unakuwa na unasoma.

Nimemaliza.
 
Hapa hakuna mjadala wowote, mahari huwa haimaliziwi yote hata uwe na ukwasi kiasi gani.

Wanachomtendea baba yako ni mambo ya kihuni tu na kukosa ustaarabu na issue siyo mahari...
Ni mjadala Kwa sababu si jambo la kawaida Mtoto kumlipia mahari mzazi wake. Au nakosea?
 
Wakwe wana njaa..kha!
Hawana issue siyo wakwe, wakwe hawajakwenda kumtwaa mwanamke kwa mume wake.

Hiyo ni economic weakness ya mume inatumika kumuadhibu mume.

Hata hao wakwe huko walipoowa hawajamaliza mahari.

Mimi mwenyewe binafsi ukweli kwangu sijamaliza mahari lakini nimeshasapoti vitu vikubwa zaidi hata ya mahari yote.

Kuna vitu vya kijinga kama hivi kwenye jamii iliyostaarabika kama wazungu huwezi kuvikuta.
 
Ni mjadala Kwa sababu si jambo la kawaida Mtoto kumlipia mahari mzazi wake. Au nakosea?
Unakosea, kuwa na akili, mpe pesa Baba yako yeye ndio atajuwa matumizi yake.

Hizi ni laana za kujitakia, atakuja kufa huyo siku utatamani hata umfufuwe umuombe radhi lakini haitowezekana na utapata tabu sana.
 
Unakosea, kuwa na akili, mpe pesa Baba yako yeye ndio atajuwa matumizi yake.

Hizi ni laana za kujitakia, atakuja kufa huyo siku utatamani hata umfufuwe umuombe radhi lakini haitowezekana na utapata tabu sana.
By the way! Hii ni story, na si mkasa halisi kutoka kwangu. Nimeleta kama sehemu ya tukio ambalo aidha lilikwishatokea zamani Kwa mtu yoyote yule au litamtokea yeyote yule.

Kwa hiyo, kunishambulia mimi kama ni tukio ambalo limenikuta, wakati si kweli, inakuwa si vizuri hata kidogo.
 
Mambo vipi wanajamvi!
Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja!
Hao wajomba ni wa hovyo. Babu/bibi wazazi wa mama yako hawakuwahi kumzuia binti yao.

Kama ni kumpa mzee fedha kwa ajili kumsaidia shida zake nyingi, ikiwemo na hiyo mpe akafanye. Lakini siyo wewe kushika pesa au ng'ombe kwenda kufanya shughuli hiyo.
 
Mambo vipi wanajamvi!
Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja...
Poleni kwa changamoto mnayopitia watoto. Vipi wewe unaonaje mama yako umemmiss au haujammiss tangu aende kwa babu yako?

Baba yenu anapitia kipindi kigumu sana, fanyeni kumsaidia ili mke wake/mama yenu arudi
 
Inategemea imani na mila za tamaduni zenu husika, kwa Imani yangu mahali ni deni na sharti limalizwe na hata mwanaume akiniacha nitaendelea kudai na akifa nitawadai ndugu zake, hiyo ni haki yangu.

Mahali maana ni ahadi yake kwangu na mahali ni yangu si ya wazazi.

Kwa upande wa kesi yako fanya kumpatia tu pesa kama msaada kwake mzazi wako ila yeye huo msaada atautumia kulipa mahari.
 
Back
Top Bottom